Lowassa kuongea na vyombo vya habari

Alisema mkoa wa Arusha na Kanda ya Kaskazini wanahujumiwa na kikundi kidogo cha watu wenye uchu wa madaraka na wenye lengo la kulinda maslahi yao binafsi ya sasa na ya baadaye.

Alitoa mfano wa tamko lililotolewa na Baraza la UVCCM Mkoa wa Pwani kwamba Rais wa 2015, kamwe hawezi kutokea Kanda ya Kaskazini kuwa ni uthibitisho kwamba vijana hao walitumiwa.

"Mbali na kwamba hili ni tusi kwa watu wa kaskazini wenye haki yao kikatiba kuwania nafasi ya uongozi wa juu wa nchi yetu, ni tusi pia kwa wapiga kura wa Tanzania wanaoamini katika demokrasia ya kuchagua na kuchaguliwa," alisema.

Alisema cha kushangaza mpake leo hakuna chombo chochote cha Serikali ambacho kimewahi kutoa tamko la kukanusha taarifa hiyo iliyounganishwa na taasisi moja ya juu serikalini.

Kwa hiyo Raisi atatoka kanda gani? kweli ccm haituhitaji watu wa Kaskazini.
 
Hawa alikuwa nao hapa vipi?

normal_Edward_lowassa_156.jpg
 
Baada ya hapo tunaweza sema tumelala maskini na leo tumeamka matajiri (Wapinzani), Mamnvi mwaga kila kitu toka moyoni mwako watu wachambue mchele na pumba, waandishi nanyi msilaze damu kwa kumpatia maswali makini ili muuze magazeti kiuhalali na sio mtuletee ngonjera zenu kwani tunasikia kuwa mnajali sana mishiko siku hizi

ila jamani tukiacha chuki ambazo hazina msingi, ni halali lowasaa kuandamwa hivi? Tukumbuke na mema alioifanyia nchi yake
 
Nasubiria kwa hamu maana yawezekana amepewa kamba kwa muda mrefu na sasa ameamua kuitumia. Yote itategemea sana na vitu viwili.

a. Atakubali makosa yake kuhusu Richmond au atafafanua kwanini hakukosea; akikubali ataomba radhi?
b. Ataamua kuachia Ubunge wa CCM ili aendelee mbele na shughuli zake kwa namna ya kuzira kama alivyofanya kwenye Uwaziri Mkuu?

Tusubiri maana akifanya jambo la tatu - kwenda kwenye offense - maana yake ni kuwa anatangaza mgongano rasmi kati yake na wale walio kinyume naye. Je hekima itashinda?
 
Kitufe cha thanks sikioni.
Hivi Lowassa alijiuzulu kwasababu gani halisi?Wengi tumekuwa tukisema tu alijiuzulu ili kuilinda serikali.Ma hivyo hatujajisumbuwa kujiuliza kuwa,je sababu hizo zilizotumika kuilinda serikali ni zipi?
 
CCM ni kama meli inayoyumba na kukaribia kuzama baada ya kupigwa na mawimbi makali ya ufisadi na uchafu,abiria asiyechukua tahadhari atazama nayo na kupotea milele...wanachama na wapenzi wa hiki chama wenye akili timamu wataondoka mapemaaaa!! na huu ndio muda muafaka kutoka CCM hakuna usalama tena....
 
Haya mlioko karibu na nyumbani kwake jamaa atasemea Arusha au Dar ?
 
jaman anaongea mda gani naomba kujua.....maana nimeongeza hata mda wa kulalal hapa nilipo ndo saa tano na dakika moja usiku...huko home najua mda huu ni saa tatu na dakika 1.......huyu bwana nina hamu ya kujua kauli yake.....
 
Atakanushakanusha tu vituhuma vidogovidogo vya Nape vya hivi karibuni basi. Lowasa, kuliko mtu mwingine yeyote anajua kinga yake kubwa ni JK kuendelea kuwepo madarakani kote, kwenye Urais na Uenyekiti wa CCM.
 
Wacha azungumze maana ni haki yake kimsingi.Hatujawahi kusikia moja kwa moja kutoka upande wake,nasubiri kwa hamu maana inawezekana akatoa yale ambayo wote tulikuwa hatuyajui so tumpe nafasi.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom