LOWASSA kukosa mkutano wa kesho Jagwani 8.06.2012

Kachanchabuseta

JF-Expert Member
Mar 8, 2010
7,269
675
lowassa-important.JPG

Habari zilizonifikia hivi punde ni kuwa Jemedali kaptani The great LOWASSA
amesusia mkutano wa ccm utakaofanyika kesho jagwani

Je hii inaashilia nini kwa wana ccm wenzangu?

Kwanini mzee huyu amekaa katika malengo ya kukizoofisha chama?

Kwanini Mikutano mingi inayoandaliwa na Nape mzee huyu huwa anaisusia?
 
Lowasa ana kaccm kake mfukoni. Ccm ya akina Nape ni ya kinafiki na inashindwa kuchukua maamuzi magumu.
 
Kama hakuna harambee basi hawezi kuja. Yule ni mtu wa kugawa pesa!
 
Lowassa hawezi kwenda kwenye mikutano cheap kama hii anayoaandaa Nape na JK...yaani mkutano hauna motive yoyote basi tu wanaiga iga tu ..kwelimaji yamezidi unga
 
anapanda jukwaa moja na nape anapokuwa na maslahi kama arumeru,..nashindwa kuelewa vipi hiki chama bado kinasurvive wakati ni vipandevipande!
 
anapanda jukwaa moja na nape anapokuwa na maslahi kama arumeru,..nashindwa kuelewa vipi hiki chama bado kinasurvive wakati ni vipandevipande!

Mkuu nikumbushe. Hivi huko Arumeru Laigwanan alipanda jukwaa moja na Nape? Nape alitia timu Arumeru kweli?
 
Mkuu nikumbushe. Hivi huko Arumeru Laigwanan alipanda jukwaa moja na Nape? Nape alitia timu Arumeru kweli?
Kimbunga Nape alikwenda na Mkapa kufunga kampeni na Lowasa siku hiyo alikuwepo, Nape akaongea kauli za kujikosha kwa Lowasa, inshort Nape ni sisimizi tu kwa Lowasa.

[h=3]MKAPA ATUA ARUMERU KUFUNGA KAMPENI ZA CCM[/h]
[h=3][/h]
Rais na Mwenyekiti Mstaafu wa CCM, Benjamin Mkapa (kushoto) akiwa kwenye chumba cha kufikia kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) baada ya kupokewa na Katibu Mkuu wa CCM, Wilson Mukama (kushoto) leo asubuhi. Wa pili kulia ni Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye.
 
Last edited by a moderator:
tanesco wakitaka wavuliwe magamba wakate umeme. hahahaaaa...hii nchi bana!. chadema tanesco wanatukatia umeme lakini ccm umeme unakuwepo mwanzo mwisho.
 
Ameshasoma alama ya nyakati nini?
Kisiasa Lowasa ana macho ya kuona mbali kuliko akina "Mwape". Nasali na kuomba mkutano wao upate watu wa kutosha, kinyume chake itasemwa Mzee mzima katia kono lake kuuhujumu mkutano!
 
Hizi ni dalili za mpasuko mkubwa ndani ya magamba. Enzi za Mwalimu hali kama hii asingeiruhusu kabisa. Angefukuza wahusika wote wanaosababisha mpasuko huo....lakini kama tujuavyo CCM hii ya leo ni tofauti sana na ile ya enzi za Mwalimu...Kikwete anajijua ni mchafu hivyo hana ubavu wa kumkemea au kumfukuza yeyote ndani ya magamba anabaki anakenuakenua tu kama kila kitu ndani ya magamba kiko shwari huku magamba ikiendelea kujifia taratibu.

Back
Top Bottom