Lowassa Kuhojiwa Na Kamati?

Kamati kamati kamati, mimi binafsi nimechoka kusikia hili suala la kamati.

Kila kitu siku hizi kinaundiwa kamati na mwisho wake huwa hatuuoni. Operation ya muhimbili imeundiwa tume, Richmond Imeundiwa tume, Mkataba wa madini umeundiwa tume... na tume nyingi zilizokwisha undwa mwisho wake unakuwa ni nini. Wakati tume hizo zote zikiundwa huwa na usemi usemao " tutaanika kila kitu hadharani, haijalishi hata kama kuna kigogo alihusika"

Hebu tujiulize hizi tume zina faida gani????????

Tangu Kikwete aingie madarakani tume ngapi zimeshaundwa????????

Na Je HIZO TUME ZILIZOUNDWA ZIMEKUJA NA JIBU GANI???????????
 
Napata wasiwasi na kigugumizi kama EL hatahojiwa.. kwani mengine yoote tunayafahamu ila sababu ya yeye kushinikiza richmond ndio ipewe hiyo tenda ndio hatulifahamu.. Je ilikuwa kwa mslahi ya Taifa au Maslahi Binafsi?? Kama yalikuwa maslahi ya Taifa je waliposhidwa hilo yeye kama kiranja mkuu wa serekali alichukua hatua gani? au hana ubavu wa kuwawajibisha wahusika? Halafu baadhi ya majina hapa sii wale waliotajwa kwenye orodha ya mafisadi?
 
Re: Breaking News: Lowassa Kuhojiwa Na Kamati?

--------------------------------------------------------------------------------

Quote: Mzee Mwanakijiji
Haya majina mbona kama nimewahi kuyasikia mahali... Gray Mgonja.. Rutabanzibwa... mmh..

sina uhakika 100% ila nathani ni kweli mkataba wa IPTL ya umeme wa Songosongo. Yule msemaji wa IPTL alikuwa na jina kama hili Rutabanzibwa..

Msemaji wa IPTL anaitwa Rugemarila ila Rutabanzibwa alishiriki mchakato na anatajwa kuwa alikataa rushwa, pia Rutabanzibwa anatajwa kuwa katika sakata la Meremeta na Tangold anakoonekana kama Mkurugenzi, kama ilivyo kwa Gray Mgonja na Andrew Chenge,, hapo utaona Johnson Mwanyika ameingia badala ya Chenge
 
Nilishauliza ni wapi katika sheria ya manunuzi ya Serikali (public procurement) panapo mpa Waziri Mkuu uwezo wa kuingilia utoaji na upatikani wa tenda za serikali.

kwa sheria iliyokuwepo na iliyopo hivi sasa ni kweli Hicho kipengele hakipo kabisa kaka...
 
Hivi wakati kamati ya Bunge ikiendelea na uchunguzi, inawezekana kwa vyombo vya habari kuendelea kuanika stori za Richmond? Maana naona magazeti mengi yamekuwa kimya sasa, na hawaibui maswala ya Richmond.
 
News ni kamati ya Bunge kufanya kazi yake kwa umakini na uadilifu ikiweka mbele maslahi ya taifa. kuhojiwa kwa Lowasa siyo issue, issue ni pale itakapothibitika kuwa kulikuwa na mkono wake. Na kama kweli aliunda task force na through that task force akashinikiza waipe Richmond anahusika, ni mtuhumiwa
 
Kama nilivyosema kwenye thread nyingine inayohusina na swala hili, tunapoteza muda.

Tuelewe, siasa ni uwongo, nani anaebisha?

Tuelewe, kamati ni system, nani enaebisha?

Tuelewe, serikali ni system, nani anaebisha?

Tuelewe, nchi inaendeshwa na system, nani anaebisha?

Tuelewe, vyama vyote vya siasa ni system, nani anaebisha?

Tuelewe, hakuna tutaloweza kufanya kuibadili system, nani anaebisha?

Jee, unaijuwa system ni nini?
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom