Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Lowassa Kufukuzwa Uongozi wa Mila

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by mmaroroi, Jan 20, 2009.

 1. m

  mmaroroi JF-Expert Member

  #1
  Jan 20, 2009
  Joined: May 8, 2008
  Messages: 2,534
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  Jamii ya Kimasai hasa wazee wa Mila wamestushwa na vurugu mbalimbali zinazotokea katika jamii hiyo na hivyo kuona kuna haja ya kumvua uongozi wa mila hiyo Mbunge wa Monduli Mh.Edward Ngoyai Lowassa ambaye hata hivyo ni wa kabila la wameru.Tangu apewe cheo hicho kumekuwa na magomvi mbalimbali tofauti na maana ya nafasi hiyo ambapo mhusika hutakiwa kuleta mapatano katika jamii.Mfano ugomvi wa Ole Sendeka na Millya kiongozi huyo alitakiwa asuluhishe ugomvi huo kwani ndiye aliyeitisha kikao kilizaa ugomvi huo lakini alikataa kwa kusema hawezi kuingilia jibu hilo moja kwa moja ni kielelezo cha kushindwa kazi hiyo kwani itamaanisha kuchochea ugomvi huo badala ya kupatanisha wahusika.Maana ya Laiguanani na kazi zao wa JF mnaofahamu mtufahamishe.
   
Loading...