Jombi Jombii
Senior Member
- Jun 4, 2011
- 185
- 10
Eerrrr!!Where is my pistol!!!
Mhadhiri wa Chuo Kikuu Dar es Salaam (UDSM), Dk Benson Bana, alisema ingawa uamuzi huo wa Bunge utazua maswali mengi kwa wananchi, sheria za Tanzania zinaeleza wazi kuwa mtuhumiwa sio mkosaji.
"Mbona Lowassa anakwenda kanisani na kuchangisha mamilioni ya fedha watu hawasemi lolote?" Alihoji Bana na kuongeza:
"Watanzania wasimhukumu mtu kwa hisia, sidhani kama hata hiyo kamati yake ina watu wasafi…, Lowassa kisheria na kisiasa yuko safi ila kihisia si safi, tunatakiwa kufanyia kazi hali halisi si hisia,".
Hata hivyo, alisema pamoja na Bunge kupeleka suala hilo kwa kamati inayoongozwa na Lowassa, Serikali pia inaweza kuunda tume yake ya kuchunguza ufisadi huo
Mhadhiri mwingine wa chuo hicho, Bashiru Ally alisema kuwa unyeti wa Kamati ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama unaweza kufanya majibu ya uchunguzi huo yakawa wazi au kuwa siri.
Mbona hawakupinga hasiwe mwenyekiti wa hiyo kamati! Maana kazi imepewa kamati siyo Lowasa.