FDR.Jr
JF-Expert Member
- Jun 17, 2008
- 1,359
- 353
Tatizo letu nini sisi wa-tz? Kwanini tuhoji uwezo wa mtu eti kwa sababu kajitokeza kuwekeza humu nchini! Kwani kuna wateule wa ktk kumiliki media au kisa ni lowasa's family? Tumeona hapa ndani zain wamesulubu wa-tz na jamvi ndio venue ya kwanza kulalamikia hili jambo, sasa mmasai/mmeru amewekeza na kuashiria ajira kwa wenzetu wenye taaluma hizo imekuwa soo na minong'ono isiyo na tija.
Binafsi naipongeza familia ya lowasa kwanza kwa kuthubutu kwa ujasiri kuishi ktk maisha ya kawaida na kujihusisha na shughuli za kawaida kama watanzania wengine walio na fursa.
Pili kitendo cha kuanzisha stesheni ya runinga hilo jambo jema na ukombozi wa kijamii hususani pale tunapotaka huduma za msingi za kijamii ziwasogelee wananchi wote.
Mzee edward ngoyayi lowasa, simama ktk kile unachoamini kwa faida ya wote. Kila la heri abc tv