Lowassa Kuanzisha ABC Television Arusha

Kwa kweli kama ni kwa nia njema, hakuna ubaya kwa Lowassa kuanzisha TV popote iwe Dar ama Arusha. Lakini jambo moja ambalo lazima tuliangalia kwa makini ni kwamba hawa jamaa wamepania kuchukua nchi. Mind you "kuchukua nchi" na hawatanii, mnataka ama hamtaki. Kilichompata Lowassa na wenzake, wameona ni kutokana na nguvu ya media. Wameamua sasa na mumesikia ama kuona, magazeti kibao yakiongozwa na ununuzi wa New Habari. Wamenunua Channel Ten. Hatua itakayofuata na ambayo mchakato umeanza ni kuwadhibiti wamiliki wa vyombo wanavyoona itakuwa kikwazo kwao ikiwamo IPP Media.

Kwa ufupi ni kwamba kama tukiwa makini kidogo tu tutabaini kwamba, Tanzania yetu inaelekea kubaya. Tunajua kila mtu ana haki ya kutawala, lakini si urithi Mwalimu Nyerere aliotuachia kwamba uongozi ni kwa wenye fedha na vizazi vyao. Nawaambia hata ndugu zangu humu (Nawafahamu) ambao wana nia njema ya kuja kuingia katika siasa kihalali (wakiwamo wanaoshabikia EL kuanzisha TV) wajue kwamba bila fedha (za rushwa) hawatashinda kutokana na mfumo uliojikita na unaoendelea kuimarika vinginevyo wawe vibaraka wa wenye fedha. Hii ni HATARI sana na hapa tukijadili mambo tuangalie huko (2010-2020) maana wenzetu wamejipanga hivyo na kwa gharama zozote zile ikibidi hata za HATARI (nitajadili kwa wakati).
kwani kuna tatizo gani EL kuhitaji uongozi wa juu wa taifa letuu?? kama anazo sifa za kutushawishi basi tukimkubalia ni haki yake kidemokrsia. tuache personality katika kujadili hojaaaa...Rushwa ndo msingi wa CCM kututawalaaa sasa kama wachagua watu fulani fulani tuuu kwa hisia zako bado hujengi hoja endelevu...

afterall EL is better than current boss in vision, thinking, implimentation and decsion. achilia mbali intelligence level.
 
Najua sana na anasaidiwa sana na Tido kuanzisha hata doc zote amewasaidia sana.....sana..nae TIDO anataka ubunge wa Muheza aweze kutulia na kula kilaini....anawategemea sana kwenye kupitishwa kura maoni.....wanalipana fadhila....tuangalie maana Media Control hakuna tena wenye Media ndio watakuwa waamua wafanye nini na wanamtaka nani....sio vikao halali wala utaratibu wetu kuchaguana na kupendekeza.....duu haya naisubiria sana niiione TZ baada 2010 na baada 2015.....
 
Mkuu Superman nimekuaminia,wewe ni Superman kweli,maana kwa ma risechi na ma uchunguzi,mmmhhh!
 
Niliposema mafisadi watashinda.... sikuwa natania.. sisi wengine ni mabingwa wa kulalamika mno; aidha tuwekeze nguvu zetu kwenye urithi wetu au tuwaache watutawale wapendavyo!
Kama tukitaka, hawatashinda. Tarime wameonyesha hivyo na Busanda wanakaribia kuonyesha hivyo. Inabidi tusonge mbele na Biharamulo Magharibi
 
Hii intelligence ya JF nimeikubali! Nakubaliana na bwana Halisi. These people are determined to rule. Folks we better be real...haya yanatokea machoni mwetu tukiwa tunaangalia..ikifika siku ya siku..tusiendelee kulalamika tuu..I think we also have to learn their tricks otherwise..watu watafanya mambo hapa ambayo yatakuja kutu-cost at some point. Kama alivyosema Halisi...TZ inakoelekea ni kubaya. Na I can assue you these people have money stolen from us to do anything they want. NI sisi kuamua..kuendelea kubishana au tuamue na sisi kama wananchi wenye stake katika hili taifa tushikamane tupambane na hawa jamaa. Utatu wa RA, EL na wapambe wao...unatishia uhai wa taifa letu.
 
Kwa hiyo waanzishe TV, that's fine lakini wafuate maadili ya uandishi wa habari. Wakiendekeza ya New Habari Corporation then hakuna ambaye atafungua channel(s) yao.
I see,

Watawapata "Ze Komedi" wengine na kuwatumia! Subiri uone. Vipindi vitakuwa merged na Televisheni yenu ya Taifa. Mtaangalia mtake msitake!

Wamejipanga mkuu...
 
I see,

Watawapata "Ze Komedi" wengine na kuwatumia! Subiri uone. Vipindi vitakuwa merged na Televisheni yenu ya Taifa. Mtaangalia mtake msitake!

Wamejipanga mkuu...
Ok, waache wafanye hivyo. Wanaweza kudhani kuwa 'wanatupata' lakini watakuwa wanajiharibia kwa sababu watu siku hizi wameamka. See how their next moves are revealed even before they make them
 
Nadhani lengo ni kuteka makabila yenye ushawishi ya Kaskazini mwa Tanzania, Kanda ya Ziwa watatumia Star TV na Radio free!!
 
Ok, waache wafanye hivyo. Wanaweza kudhani kuwa 'wanatupata' lakini watakuwa wanajiharibia kwa sababu watu siku hizi wameamka. See how their next moves are revealed even before they make them

Mi kila siku huwa najiuliza ...haya tumeshafahamu haya yote sasa tunafanya nini! Au ndio yale mambo ya mwenye nguvu mpishe?
Hizi nchi zetu ukishakua na vijihela,ukapta kuwaweka kwenye payroll watu wanaofikiria kidogo zaidi ya wengine na kjua njia sahihi za kuwakamata wananchi it is so easy to rule and to rule forever.... Kwani watu huwa wanataka vitu vikubwa basi! Doti ya kanga,pilau na hotuba zenye kusemana ushamaliza
 
Ok, waache wafanye hivyo. Wanaweza kudhani kuwa 'wanatupata' lakini watakuwa wanajiharibia ....


Wanajiharibia!!!???

Hiyo TV inataweza tumika kwenye kampeni za CCM Arusha, na pengine Manyara na Kilimanjaro. Usishangae majimbo yote ya pande hizi yakaenda kwa CCM.

Kalaghabahoooooo.
 
Wakuu,

Source inaonyesha kuwa application for licence ilitoka kwenye Daily News, Friday, 24th October 2008, Page 22. kwa hiyo issue yenyewe sio siri kama tunavyotaka kuipresent hapa, na kama kuna mtu alikuwa na objection angefuata the necessary procedure. Hatuhitaji kulalamika sasa wakati tulipewa that chance October 2008, lakini tulikaa kimya.

We dare to talk openly. Tukate issues!
 
You are a super human kwa kutuletea haya majamboz. Watu wanajiandaa kwa kampeni wakielewa kwamba 2010 mambo yatakuwa magumu. Hebu wakaazi wa Arusha watueleze hao Richard na Lucumay wana uwezo kiasi gani cha kufungua TV station? Au ndio vivuli?
 
Source:

Daily News, Friday, 24th October 2008, Page 22.

Public Notice

Application for Content Services Licences (Broadcasting Licences) to TCRA.

Name of Station:
ABC Television
P.O. Box 11843
Arusha

Shareholders:
Robert Francis Lowassa (Tanzanian) - 60%
Elias Stephen Kordun Lukumay - 40%


Who is Robert Francis Lowassa and Elias Lukumay?

Source: www.parliament.go.tz/Polis/PAMS/Docs/HS-4-44-2006.pdf


BUNGE LA TANZANIA
________
MAJADILIANO YA BUNGE
________
MKUTANO WA NNE
Kikao cha Arobaini na Nne – Tarehe 16 Agosti, 2006
(Mkutano Ulianza Saa Tatu Asubuhi)
. . . . . .
SPIKA: Sina shaka mtakubaliana nami Waheshimiwa Wabunge kwamba, hiyo ni hoja kabambe ya kuahirisha Bunge. Kabla sijawahoji, kuna matangazo mafupi yafuatayo:-


Napenda tutambue kuwepo kwa familia ya Mheshimiwa Waziri Mkuu, Mheshimiwa Mama Regina Lowassa, Bwana Fred Lowassa, Bwana Robert Lowassa na Master, kwa hiyo, huyu ndiyo mdogo mdogo tu Richard Lowassa. Wale ambao mmeshiriki vizuri kwenye Bunge na mnahudhuria mara kwa mara, mtakumbuka kwamba, Richard si mgeni sana, hapa kwa sababu mara kwa mara tunaonana naye pale nje, sielewi Mwenyezi Mungu, mambo haya sijui yanakuwaje? Hatujui hatma ya Richard, lakini Mungu aendelee kumsaidia inaelekea anapenda sana Bunge. Pia marafiki zao Bwana John Bakilana na Bwana Elias Lukumai. Karibuni sana na ahsante kwa ushiriki wenu.
. . . . . . . . . . . .


Last week ABC Television waliitwa na Bodi ya TCRA kwa ajili ya Interview ya Kupewa Leseni . . . . .


Habari ndo hiyo . . . . . .

Huku Arusha kuna Studio ya TANMEDIA imeanza kujengwa, ni ghofa tatu maeneo ya Njiro na ni studi ya Radio na TV na inasemekana ni ya Lowasa, pengine ndo maandalizi ya Redio hiyo ambayo baadaye itakuwapo na TV pia.
 
mwizi akikuibia ng'ombe akaenda akamtunza vizuri na hatimaye ng'ombe akawa na ndama, halafu mwizi huyo huyo akaja kukuuzia maziwa na ndama yule wakati unajua ng'ombe mwenyewe alikuwa wa kwako utashukuru kwa ukarimu wake?

majibu yanaelekea kuwa ni 'Ndiyo' kwa sababu tu hakumchinja yule ng'ombe!

Kama ni kweli itakubalika kuanza, nampa hongera sana EL kwa juhudi zake kaunzisha ABC TV. Ningeshukuru zaidi kama itakuwa na cover up kubwa hadi kufika mkoa wa Kili. Nakuunga mkono Mzee Mwanakijiji
 
- Lowassa alipokuwa Waziri Mkuu, alikuwa anahaingaika kumjibu kuanzia kwenye magazeti, mpaka humu JF kumjibu member mwenzetu Mwanakijiji, ilikuwa ni kwa sababu haaminiki, haeleweki, na hana msimamo!

- Na juzi Rostam, alikuwa anahaha kumtafuta Mwanakijiji apunguze mashambulizi, kwa sababu haeleweki, haaminiki, na hana msimamo!

- Mkulu Mwanakijiji, I hope hukatishwi tamaa wala kuogopeshwa na hizi kelele za mlango, sio siri kwamba kuna wasioweza kuelewa masilahi ya taifa na ya binafsi, lakini kwenye demokrasia hatuna jinsi ila kuwa nao tu, lakini mapambano yanaendelea. Kuna ishu ambazo sikubaliani na Mwanakijiji, lakini sio kupiga vita ufisadi, kwenye hili tupo pamoja mkuu MMJ, na job welldone keep it up!

Respect.

Wazee wa sauti ya umeme FMES!

hivi wewe unamjua Mwanakijiji vizuri kweli? kwa taarifa yako Mwanakijiji ni Ndumilakuwili achelewi kukugeuka mda wowote,pia anatumiwa na baadhi ya watu kwenye shughuli zao.Hivyo kuweni makini nae sana hasa Thread zake anazo anzisha ilikupima upepo wenu then anapeleka report kwa wahusika.be care full guys.
 
Last edited:
Acheni roho mbaya ya chuki,mbona fisadi nyangumi anamiliki televisheni 3,redio 3 na magazeti lukuki na hamzungumzi habari zake?Kuweni wabunifu katika masuala ya kuendeleza Taifa letu si kuangalia fulani kala nini!
 
Hao ni wajasiliamali na tena ni Watanzania wazalendo wenzetu tu. Kama Mengi ana TV na redio, Joseph Kusaga naye anataka kuanzisha ya kwake, mimi sioni ubaya. Ni vema na haki! Tatizo ukishaingia kwenye tope la ufisadi na ukachafuka, kila unachofanya watu wanaona kama vile unajitengenezea njia bora ya kuwa fisadi zaidi!
 
3 Reactions
Reply
Back
Top Bottom