Lowassa kuanza kampeni wiki ijayo

anataka akafunike kule.? Ngoja aende labda ataropoka baadhi ya mambo kwa faida ya taifa maana jamaa hata akikohoa wapambe wanaripoti.!!
 
Kwa kweli natamani nimsikie atasema nini kwenye hiyo kampeni; I hope hatochambuliwa wapinzani au upinzani au personalities maana....
 
Hawana ubavu kiaje??
Kwani kampeni ni pesa au sera?
Kwa Arusha Lowasa hana chake huku si km sehemu nyingine arifu....kisiasa Arusha iko next level

Ni kweli ni next level, nikumbushe kidogo kwani mkoa wa Arusha kuna wabunge wangapi toka upinzani?
 
Hata Hitler alikuwa Hero wa kundi fulani la watu, na bado kuna watu miaka zaidi ya 65 baadaye bado wanamuona Hero.
Amina alikuwa Hero.
Mobuto alikuwa Hero.
Hata Ian Smith alikuwa Hero

Hii si mentality ni Truth Mheshimiwa huyu Edward Lowassa ni FISADI.
Ila kuna watu UFISADI wanaita kuchangamka.

Mtabaki na hiyo mentality kuwa Lowasa ni fisadi..
Wameru wanamkubali Lowassa. He is their hero!
 
Wazazi CDM inabidi ipange kikosi upya Arumeru,mtu mzima ELule ni uwanja wake wa nyumbani Dr Silaa na Mbowe mpo wazazi;Madogo Nassary na Nyerere huo mziki wa EL hawatauweza......................tusije nyang'
 
Habari za kuaminika kutoka kwa mmoja wa watu walio karibu na Lowassa zimedai kuwa Mbunge huyo wa Monduli, wiki ijayo ataanza rasmi kumpigia kampeni za nguvu mgombea waChama cha Mapinduzi (CCM), Sioi Sumari, mara baada ya kurudi kutoka Ifaraka atakakohudhuria sherehe za kumsimika rasmi askofu wa jimbo jipya la Ifaraka la kanisa Katoliki, Salitarus Libena, Machi 19, mwaka huu.

Imedaiwa kuwa Lowassa ataendesha kampeni akipita kila kata za jimbo la Arumeru Mashariki,katika kile kilichoelezwa ni kuhakikisha kuwa mgombea huyo wa CCM ambaye ameoa mtoto wa mbunge huyo, Pamela Lowassa, anashinda katika uchaguzi huo.

MY TAKE Aangalie asiropoke kama Mkapa.

Atakuwa amepotea njia lowassa ana mvuto kwa wameru na akienda ajiandae na haya:
1. Aliukana umeru
2.akiwa waziri wa maji alikwepesha mradi wa maji ambao ulikuwa uwanufaishe wameru yeye akapeleka monduli
 
Lowassa anakubalika kwa pesa zake; si mnaona anakoalikwa? Ni kwenye uzinduzi wa ujenzi au katika hafla yoyote inayohitaji mchango wa pesa, na kweli jamaa anamwaga mamilioni. Watu si wajinga kihivyo - wanakula pesa yake tu.
Akiingia arumeru kwenye kampeni cdm wawakumbushe wananchi ripoti ta mwakyembe iliyomlazimisha kujiuzuru, Huyu kamwe si waziri mkuu mstaafu bali ni waziri mkuu aliyelazimishwa kujiuzuru kwa kashfa ya ufisadi. Pesa anayotoa kama mchango katika hafla hizo anadhani anawanunua wananchi, lakini wananchi waelezwe kuwa hiyo ni fedha zao anazoendelea kukwapua kupitia mikataba mibovu aliyoiasisi.
Je BAE tuwashukuru na kuwaenzi kwa kurudisha pesa waliyotuibia? Wana tofauti gani na EL anayerudisha kwa njia ya michango? Wote ni wa kushtakiwa kwani ni ufisadi tu!
Je hili la kumkampenia mkwe limekaaje? Yaani familia ya EL tu ndiyo inafaa kwa kuongoza? Baba mkwe, mkwe nk. Kuna msemo kuwa usiweke mayai yote katika kapu moja, leo EL anataka kuweka ndugu zake wote katika biashara ya siasa, siku hilo kapu likianguka! Mkumbuke ya Gadaffi na familia yake
 
Hawana ubavu kiaje??
Kwani kampeni ni pesa au sera?
Kwa Arusha Lowasa hana chake huku si km sehemu nyingine arifu....kisiasa Arusha iko next level

Hawana ubavu kwakuwa Mh Lowassa anakubalika sana nchi nzima especially Arusha.
 
Huyu mzee angepumzika tu kuliko kutafuta idhara kama pesa anayo anahangaikia nini? aibu!
 
Lowassa anakubalika kwa pesa zake; si mnaona anakoalikwa? Ni kwenye uzinduzi wa ujenzi au katika hafla yoyote inayohitaji mchango wa pesa, na kweli jamaa anamwaga mamilioni. Watu si wajinga kihivyo - wanakula pesa yake tu.
Akiingia arumeru kwenye kampeni cdm wawakumbushe wananchi ripoti ta mwakyembe iliyomlazimisha kujiuzuru, Huyu kamwe si waziri mkuu mstaafu bali ni waziri mkuu aliyelazimishwa kujiuzuru kwa kashfa ya ufisadi. Pesa anayotoa kama mchango katika hafla hizo anadhani anawanunua wananchi, lakini wananchi waelezwe kuwa hiyo ni fedha zao anazoendelea kukwapua kupitia mikataba mibovu aliyoiasisi.
Je BAE tuwashukuru na kuwaenzi kwa kurudisha pesa waliyotuibia? Wana tofauti gani na EL anayerudisha kwa njia ya michango? Wote ni wa kushtakiwa kwani ni ufisadi tu!
Je hili la kumkampenia mkwe limekaaje? Yaani familia ya EL tu ndiyo inafaa kwa kuongoza? Baba mkwe, mkwe nk. Kuna msemo kuwa usiweke mayai yote katika kapu moja, leo EL anataka kuweka ndugu zake wote katika biashara ya siasa, siku hilo kapu likianguka! Mkumbuke ya Gadaffi na familia yake
Hakika wewe ni tank la giza.
 
Atakuwa amepotea njia lowassa ana mvuto kwa wameru na akienda ajiandae na haya:
1. Aliukana umeru
2.akiwa waziri wa maji alikwepesha mradi wa maji ambao ulikuwa uwanufaishe wameru yeye akapeleka monduli
Thibitisha hili povu lako.
 
Habari za kuaminika kutoka kwa mmoja wa watu walio karibu na Lowassa zimedai kuwa Mbunge huyo wa Monduli, wiki ijayo ataanza rasmi kumpigia kampeni za nguvu mgombea waChama cha Mapinduzi (CCM), Sioi Sumari, mara baada ya kurudi kutoka Ifaraka atakakohudhuria sherehe za kumsimika rasmi askofu wa jimbo jipya la Ifaraka la kanisa Katoliki, Salitarus Libena, Machi 19, mwaka huu.

Imedaiwa kuwa Lowassa ataendesha kampeni akipita kila kata za jimbo la Arumeru Mashariki,katika kile kilichoelezwa ni kuhakikisha kuwa mgombea huyo wa CCM ambaye ameoa mtoto wa mbunge huyo, Pamela Lowassa, anashinda katika uchaguzi huo.

MY TAKE Aangalie asiropoke kama Mkapa.
Lowassa ni Chief of Politics no one like him. Fuatilia kwa makini siasa zake na ndipo utagundua kuwa kwanini Watanzania wanamhitaji Lowassa awe rais wao 2015.
 
Hawana ubavu kiaje??
Kwani kampeni ni pesa au sera?
Kwa Arusha Lowasa hana chake huku si km sehemu nyingine arifu....kisiasa Arusha iko next level

nawasiwasi na uwezo wetu kwenye kuelewa sera, nawasiwasi sana. Sidhani kama kuna sera ishasemwa mpaka sasa, sidhani. Tumezoea ahadi basi
 
Hebu wataalamu tupeni tofauti ya Monduli, A Town na Arumeru. Kama ingekuwa linear intepolation basi nafikiri CCM ina wakati mgumu Arumeru. Hebu nisaidieni. Na kama unamwaga pesa halafu ukashindwa vibaya basi ni bora kulinda afya kwanza.
 
Kitu ambacho kinanifurahisha Lowassa ana watu wake kila chama cha siasa, ukienda CDM kuna kundi lake ukienda CUF ndiyo usiseme, ukienda NCCR Mageuzi ana kundi lake mtu kama huyu kupambana nae ni kazi.
 
Back
Top Bottom