Lowassa for CHADEMA, mpokeeni

Ni mtendaji mzuri sana tena mjue ni safi akipewa uenyekiti CHADEMA.


M tendaji mzuri katika unyang'anyi wa rasimali za nchi kwa manufaa yake.......
M richmond mzuri....... na baadae Dowans
M ccm mzuri aletolewa kama kondoo wa sadaka!!
Hawezi kuwa Chadema!
Yeye alizoea vya haramu na vya haramu vip ccm tu
 
Ni mtendaji mzuri sana tena mjue ni safi akipewa uenyekiti CHADEMA.


M tendaji mzuri katika unyang'anyi wa rasimali za nchi kwa manufaa yake.......
M richmond mzuri....... na baadae Dowans
M ccm mzuri aletolewa kama kondoo wa sadaka!!
Hawezi kuwa Chadema!
Yeye alizoea vya haramu na vya haramu vip ccm tu
 
Inawezekana kuja CDM kwa sharti moja dogo. Atueleze kile ambacho Mwakyembe na wenzake walidai kuwa hawakukisema ili kuepusha serikali yote kuanguka. Sema Lowasa sema, hiyo ndiyo njia pekee ya kujisafisha, vinginevyo fia huko huko kwenye magamba

You are really thinking big!! This is what we term as great thinking. Asante mkuu
 
Mkuu, amekutuma ili kupima upepo au haya ni mawazo yaliyokujia wewe mwenyewe kichqwani mwako?
Mkuu yanatumwa majini, washabiki na wabeba kadi wa vyama vyenu sio mimi. Mi ukizingua hata we nakuchana tu hata bila wese.
 
E.L ni m2 wa michongo ya pesa, mnakumbuka ule mchongo wa mvua kutoka thailand eti inyeshe mtela tu! mshkaji ni kiboko yule. Ogopen watu walio ona loop za kuiba enzi za nyerere!.
 
CHADEMA hawataeleweka endapo watampokea EL. Ikumbukwe kwamba vita dhidi ya ufisadi ni moja ya ajenda kubwa ya CDM. Katika vita hivyo El amekuwa mmoja wa watuhumiwa. Itakuwaje wampokee mtu huyo wanayemtuhumu? Haiwezekani.
 
Aweke mambo yote wazi kwa ushahidi ili kuwaridhisha wananchi kuwa tuhuma za ufisadi ni za uzushi.
Akithibitika kuwa ni msafi basi atapokelewa.
 
Acheni zenu we apply alternatives, wamewezakuwaongoza maelf ya Watz katka maandamano sembuse lowasa!, samaki mkavu wanamloweka katika maji ya uvuguvugu akishalainika tu mnapika akiiva analiwa wamoto hamjui?
Harufu ya uvundo itaitoaje sasa? au nayo itailowekakwenye maji ya uvuguvugu? Au itaipiga pafyumu?
 
Hey!CHADEMA ninyi ni wanaharakati na waalimu wazuri nawashauri jambo moja gumu,pamoja na kuchafuliwa kisiasa babu yetu Lowasa fanyeni mpango mumpe offa ya kadi, atawasaidia sana maana pamoja na mchango wake huko kijiwe cha CCM wamememnyima heshima yake kwaualimu wenu mumfundishe uzalendo na jinsi yakutumikia taifa na kuirejesha heshima yake kisha mumpe wajibu na majukumu. Maana kazi kubwa ya wanaharakati ni kuleta mabadiliko katika mambo mbalimbali. Go ahead CHADEM WAR FRONT, CCM WILL FOLLOW!
shibuda tu kimeo, ndo iwe mamvi? Loh! Hatutaki
 
Hey!
CHADEMA ninyi ni wanaharakati na waalimu wazuri nawashauri jambo moja gumu,
pamoja na kuchafuliwa kisiasa babu yetu Lowasa fanyeni mpango mumpe offa ya kadi, atawasaidia sana maana pamoja na mchango wake huko kijiwe cha CCM wamememnyima heshima yake kwaualimu wenu mumfundishe uzalendo na jinsi yakutumikia taifa na kuirejesha heshima yake kisha mumpe wajibu na majukumu. Maana kazi kubwa ya wanaharakati ni kuleta mabadiliko katika mambo mbalimbali. Go ahead CHADEM WAR FRONT, CCM WILL FOLLOW!


Mwe!! Hapo ni sawa na kumwambia Osama akaimbe nyimbo za Injili!
 
anakaribishwa sana tu, lakini magamba ayatoe kabisa na kuyatupa akifika kwenye geti la CDM maana huku CDM hatuvui magamba bali tunayapoteza kabisa.
 
kweli cdm ni wapumbavu ss hv mnataka lowasa fisadi ilihali nyie mnapinga ufisadi.tatizo lenu cdm nyie ni ma opportunist hilo ndo linalowasumbua na nawaambia watanzania hawatokaa waiweke cdm madarakani labda wote tuwe wendawazimu km nyie.
 
Mi nafikiri kama Lowasa akitubu toba ya ukweli. Yaani akayasema yote aliyoharibu na kurudisha alichochukua kwa hila. Kiisha akasaliwa asirudie tena maisha hayo bali aanze upya carrier yake ya kisiasa nadhani anaweza kufaa bado. Mtu hawezi kuwa mbaya milele maadamu bado anaishi. Mwaonaje wana jf?
 
Aweke mambo yote wazi kwa ushahidi ili kuwaridhisha wananchi kuwa tuhuma za ufisadi ni za uzushi.
Akithibitika kuwa ni msafi basi atapokelewa.

Kamwe hawezi kuthubutu kufanya hivyo, TISS wanaushahidi wa uvundo wake file kumi nzima, ajaribu aone kitachomtokea...
Alikua anauma na kupuliza kwa kutumia sana media ili imuoneshe anafanya sana kazi na anafuatilia mambo...jambo ambalo hata
Mizengo Pinda anafanya ila tofauti ni kuwa yeye hatumii media kujionesha, anaacha watu waone wenyewe, mfano ni kwa waziri mkuu
kutumia Landcruiser Gx badala ya Vx kama ilivyozoeleka. Mpaka juzi kuna mbunge kamtolea mfano bungeni. Ingekua ni Lowassa kesho
yake ungeona kwenye kila gazeti na jioni yake kila Tv inaongelea Waziri mkuu kapanda Gx na ndo ingekua headline story kwa siku hiyo.
 
LOWASA karibu,kwa kipindi kifupi ulichokaa madarakani walau ulionyesha kuwajali watz,ulisimamia shule zikajengwa,mradi wa maji victoria mpaka kahama,mradi wa maji wachina dar bomba zilitandazwa lakini ulivyoondoka mpaka leo bomba zile hazijtumika.eti source ya maji haitoshelezi.barabara kama ya shekilango ilijengwa etc.karibu tuwaletee watz maendeleo!yaliyopita si ndwele!tunajua tatizo lilikuwa ni uwaziri mkuu

hapo ndipo watz tunapokosea na kujikuta tunachagua viongozi wa kujutia milelel. Tunasahau mapema mno kwa kukumbuka machache mazuri aliyofanya Lowassa ambayo ni moja tu ya majukumu na wajibu wake kama kiongozi wa nchi. Kwani hayo maendeleo uliyotaja hapo aliyatoa kama zawadi? tena alipaswa kufanya vizuri zaidi ila tu hujui.

Watanzania tuache huruma za ki jinga kwa viongozi wazembe na mafisadi. Wewe unamuonea huruma fisadi??!!!!!!
 
Sina hakika kama CHADEMA iko kwa ajili ya kuangalia celebrity status ya mtu zaidi ya kuangalia uadilifu wake. Huyo Morani hawezi hata kupewa ulinzi wa ofisi za shina CHADEMA, amekwishachafuka na hawezi kusafishika.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom