Lowassa azungumzia kuanguka kwa Hosni Mubarak

Yeye ni fisadi. Hayo anmwambia nani kwenye luninga? Si awapigie cm mafisadi wenzie waachie ngazi kabla hayajatokea ya Misri?
 
ngoja tutawajibu sasa nadhani hili wengine tumeliacha kwa muda hadi linaanza kuwa ni ukweli. Lowassa hana nafasi ya uongozi wa taifa la Tanzania. NONE. Not while he doesn't want to apologize to Tanzanians and own up his failures as a leader. Not a chance.

Mwanakijiji siasa za Tanzania ni za ajabu. Kuna watu wengi sana ni failures as leaders lakini wanaendelea kuwepo na wamekuwepo kwa muda mrefu. Lowassa ni mmoja tu, uunaweza kuandika orodha ndefu sana, ukiangalia unaweza kuona kuwa kwenye uchaguzi wa mwaka jana kuna wengi tu walifaa kuachwa, lakini waliruhusiwa na kupigiwa kampeni. Kwa hiyo sitashangaa kuona kuwa Lowassa anarudi tena kwenye uongozi.
 
Hivi kwa nini Serikali inatumia nguvu nyingi kumsafisha EL, kama nchi ingekuwa makini na yeye mwenyewe kama angekuwa ni makini hata huo ubunge hasingegombea

Yaani kelele zote hizo ni kutaka kurudi Ikulu 2015
 
Safari ya EL imeanza upya kwa udhaifu wa JK nafikiri EL labda ataweza kuisafisha CCM na kuivusha kulee kwenye maono ya wachache wanaoona mbali la sivyo CCM bye bye..kama tukipata mtu ataesema hii siitaki kwa faida ya wananchi na waoiga kura!!
 
Ndugu Zangu,

Ni fundisho kwa watawala wetu. Tusingependa vurugu za Tunisia na Egypt zifike kwetu, maana zina madhara makubwa ya kijamii na kiuchumi............

Kabla sijamaliza sijui kama nimemuelewa maggid . anapoandika hii ha bari yeye anasimamia upande gani ? wa kati au wa serikali au wa wananchi.? Kwa nini atumie neno "vurugu" za tunisia na egypyt. Wao wenyewe wanasema "mapinduzi"

  • Je madhara ya kiuchumi waliyopata watunisia na na wa misri yana gharama gani kulinganisha na faida yahizo alizoita vurugu. kama yanafaida basi sio vurugu.
Edward Lowassa ameonyesha ujasiri wa kujitokeza hadharani na kukiri , kuwa kuna mapungufu ya kimfumo, kwamba ubepari huu ndio umewafanya WaMisri waingie mitaani. Utajiri wa Mubarak unasemwa unaweza kuvuka utajiri wa Bill Gates. Wakati huo huo watu wa kawaida wa Misri wamekuwa wakiishi katika maisha magumu sana. Na Lowassa alionyesha hatari inayoweza kutokea kwetu . Amefikiri juu ya kipi kifanyike.
Huu ni unafiki kusingizia ubepari.Mpungufu makubwa yaliyopo Tanzania sio mfumo wa ubepari . tatizo ni viongozi wanaosimamia mfumo huo wa ubepri kuweka ubinafsi mbele na hivyo kusababisha ufisadi. Kwa nini EL anakwepa kutaja neno Ufisadi . Botswana inatumiamfumo huohuo wa unaitwa wa kibepari. Tatizo la tanzania sio mfumo tatizo ni viongozi full stop

Kama ni mfumo ni huu mfumo unaofanya mbunge kuwa na kipato kikubwa kuliko afisa elimu mifugo,RPC na mganga mkuu wa wilaya ndio unaleta matatizo.

Kama ni mfumo wenye tatizo basi ni huu mfumo ambao wanasiasa wanakuwa miungu watu kuliko watendaji wengine. ndio unatakiwa kubadilishwa na sio ubepari.

Tuliimb nyimbo hiii zamani
ilitundeleee tunahitaji mambo manne. WATU, ARDHI, SIASA SAFI na UONGOZI BORA.

Kama ilivyo kwa wamisri na watunisia tanzania UONGOZI BORA ni tatizo kubwa. sasa ukijumlisha na Katiba ya chama kimoja wakati nchi inavyama vingi pia SIASA SAFI ni tatizo lingine
 
Ndugu Maggid:
Ninaheshimu sana michango yako, na kile unachokiamini bila kuyumbishwa na kauli za Wale wasiokubaliana na wewe.
Lakini nina haya yafuatayo ya kukuuliza:

(1) Hivi Wananchi wa Tanzania wako tayari kumchagua mtu kwa sababu ya utaalamu wa sanaa ya mawasiliano na si uwezo wa kusimamia sheria na kanuni za nchi yetu kama vile sheria za Procurement?, ambazo zilivunjwa na hatimaye kutuletea kampuni feki ya Richmond?
(2) Wewe Maggid unazungumzia Umuhimu wa Ujamaa lakini unafahamu huyo Lowassa ni Bepari Mzuri tu , hivi unadhani Bepari akichukua nchi hii atasimamia sera za kijamaa zenye manufaa? mbona unajicontradict Mkuu?!
(3)Unasema Lowassa aliwavuta anaowasiliana nao, Mkuu hii conclusion umeipata wapi?, hizi statistcs umezipata wapi?.. hebu tuambie ni wangapi uliowahoji wameonekana kuvutiwa na hayo maelezo ya Lowassa na wangapi Hawakuwa impressed?.

Mkuu Maggid, Watanzania wa leo siyo watanzania wa Jana, Kilichomvua Uwaziri mkuu Lowassa ndio hicho hicho kitakamchomfanya asiwe Raisi wa Jamhuri ya Muungano w Tanzania!.
Kama ni uwezo wa Kuvuta watu, Bingwa alikuwa nduli Iddi Amini Dadaa, huyo alikuwa Comedian Mzuri, lakini si kiongozi mzuri!, Hitler naye alikuwa bingwa wa kuongea na kuvuta watu, lakini naye hakuwa kiongozi mzuri! mimi ninadhani kwamba UWEZO WA KUJENGA HOJA BILA UADILIFU HAKUTOSHI KUMFANYA MTU AKAKUBALIKA KWA WANANCHI, LABDA NA WANANCHI WENYEWE SIJUI WAWE NI WATU WA NAMNA GANI!.
 
Nimesoma maelezo yako, lakini yanaonekana kuwa na ushabiki ndani yake. Nilitegemea ungesema hasa alichoongea Rich wa Monduli na sio maneno yako binafsi kama ulivyojipambanua.

Nanaijiwa na hisia kuwa wewe ni kibaraka wa Lowasa na unafanya kazi ya kumtangaza au kumuuza. "It is too late to repaint Lowasa image". Lowasa hana uzalendo wowote kwa watanzania hata kama atajikosha kwa kiasi gani bado watanzania tuna maumivu na makovu aliyotupa Lowasa pamoja na rafiki zake.

Haingii kichwani mwa watanzania kwa Lowasa kuongelea swala la watawala kujilimbikizia mali ni bora angekaa kimya kwa hilo. Kumbe ni kweli "NYANI HAONI KUNDULE LAKE"

Naungana na Mzee Mwanakijiji kuwa Lowasa has no chance to lead this country as a President.

Poor Maggid Mjengwa You dont Get it and you will never get it.

Meen!! You are so cheap!

Unaleta ushabiki wa kijinga mbele ya kazi?

Kuanzia leo mimi nimekuunganisha na Mafisadi wa Tanzania, lolote usemalo au wao wasemalo wewe nimshiriki na siku ikifika anza kuandaa makazi mapya ukweni.
Hayo maneno angesema Rostam Azizi bila aibu ungetoa makala kama hi nakumsifiai sana.
Nakuona mtu hatari upendaye maumivu kuliko kwamba wewe ni mtu wa kujipendekeza.
Hivi unajua kitakacho wapata Mandundami kama wewe kule Egypty?

unajua ni lini upepo ule toka kaskazini utafika huku??
Lowassa kasoma Tamthiria pala UDSM kwake maisha yetu ni mchezo wa kuigiza, cha ajabu wewe unadiriki kukaa upande wake na kuramba matapishi ya NUNDA huyu.

Wamekukatia ngapi kiasi cha kuuza utu wako wote??

Ole Maggid.

Ndugu Zangu,

NDANI ya saa 24 baada ya tukio la Mapinduzi ya Umma kule Egypt, Edward Lowassa ,Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama ameonekana kwenye runinga akitoa tafsiri ya kilichotokea Egypt , nini cha kujifunza na kipi cha kufanya.

Lowassa alianza kwa kuwapongeza wanaharakati wa Misri. Akazungungumzia madhara ya viongozi kujilimbikizia mali, umuhimu wa viongozi kusoma alama za nyakati, athari za ubepari, umuhimu wa viongozi kusikiliza matatizo ya watu wao na mengineyo. Kimsingi, Edward Lowassa alizungumzia masuala yanayowahusu ‘ People On The Streets’- Watu wa mitaani, na kwa lugha inayoeleweka na watu wa mitaani.

Na kwa hakika, yanayotokea sasa ni Mapinduzi ya Umma wa Kijamaa barani Afrika. Kilio cha mamilioni ya Waafrika ni kilio cha kutaka uwepo wa Haki za Kijamii- Social Justice. Sera za Kibepari hazijali haki za kijamii. Ndio maana, Wajamaa wa Afrika tumeyapokea yalitokea Tunisia na Misri kwa mikono miwili. Ni fundisho kwa watawala wetu. Tusingependa vurugu za Tunisia na Egypt zifike kwetu, maana zina madhara makubwa ya kijamii na kiuchumi.

Hata hivyo, tunataka watawala wetu wasome sasa alama za nyakati. Waongoze mabadiliko ya amani ikiwamo mabadiliko makubwa ya Katiba ili tuepushe watu wetu kupoteza maisha na mali zao mara vurugu za kisiasa zitakapotokea. Na tusijidanganye, kuwa tuna amani, yetu ni amani ya vurumai.

Edward Lowassa ameonyesha ujasiri wa kujitokeza hadharani na kukiri , kuwa kuna mapungufu ya kimfumo, kwamba ubepari huu ndio umewafanya WaMisri waingie mitaani. Utajiri wa Mubarak unasemwa unaweza kuvuka utajiri wa Bill Gates. Wakati huo huo watu wa kawaida wa Misri wamekuwa wakiishi katika maisha magumu sana. Na Lowassa alionyesha hatari inayoweza kutokea kwetu . Amefikiri juu ya kipi kifanyike.

Mwanafalsafa Benjamin Disraeli anasema; “A good leader knows himself and the times”- Ndio maana pia ya kiongozi kuwa na uwezo wa kusoma alama za nyakati. Na kiongozi mzuri, hata katika nyakati ngumu, mara zote hujiweka katika nafasi ya ushindi.

Kwenye ulingo wa myeleka, hubaki katikati ya duara, atapigwa, ataanguka, atasimama. Atapigwa tena, ataanguka, atasimama. Hutokea kwa adui kuingiwa na mashaka na woga kutokana na ustahimilivu wa anayepigwa. Kwenye mchezo wa myeleka jitupe katikati upambane, kamwe usisimame kando ya duara, utaharakisha kazi ya adui kukutupa nje ya ulingo.

Na sifa moja ya mwanasiasa ni kuwa na uwezo wa kufanya yale ya kuwashangaza wengine, inahusu timing, inahusu wakati. Hata kabla ya Waziri wetu wa Mambo ya Nje hajaongea na wanahabari, Edward Lowassa , kwa nafasi yake ya uenyekiti wa kamati husika na mambo ya Ulinzi, Usalama na Nje ameongea na wanahabari.

Na hakuongea kwa kukurupuka, Lowassa alionekana kuifanyia kazi taarifa yake. Si ndio, wanaomjua Edward Lowassa wanasema, kuwa jamaa ni workalcoholik, ana ulevi wa kuchapa kazi. Anafanya kazi kwa saa nyingi. Na kuna ujumbe aliutuma jana, kuwa Edward Lowassa amerudi. Baada ya kimya kirefu.

Lowassa huyu anaonekana kuwa bado ana nguvu na ushawishi ndani ya Bunge na Serikalini. Si tumeona, amechaguliwa kuwa Mwenyekiti wa Kamati nyeti bungeni bila kupingwa. Na kama ana dhamira ya kusimama, kugombea Urais 2015, basi, Edward Lowassa ana kazi moja kubwa inayomkabili ; kurudisha image yake ya zamani kwa umma, in principio, ya kama mwanzoni. Huu ni mtihani mgumu kwa Lowassa, akifaulu, 2015 hakamatiki.

Maana ni ukweli, kuwa Edward Lowassa wa sasa ni ’ libero’ uwanjani, hana wizara, lakini anaongoza Kamati nyeti na yenye nguvu kuliko zote bungeni. Lowassa huyu ni hatari kwa wapinzani wake katika kuelekea 2015 kuliko Edward Lowassa aliye Waziri Serikalini. Naam. Kuna burudani ya kisiasa inakuja.

Na kuna watakaoshika tama na kusema, kumbe, Edward Lowassa hajamalizwa kisiasa! Je, akina Mwakyembe hawakufahamu, kuwa simba humwui kwa risasi ya kumpapasa masikioni. Kama ni mchezo wa ngumi, basi, kwa mpinzani wa Lowassa, akubali, kuwa kummaliza Lowassa , awe tayari kucheza raundi zote 12.

Ndio, siasa inahusu pia sanaa ya mawasiliano, kwa mwanasiasa, kama huiwezi sanaa ya kuwasiliana na wananchi, basi, ni sawa na mtu anayejiita fundi mekanika , lakini hawezi kushika spana.

Tunayasema mabaya mengi ya Edward Lowassa, lakini, ni ukweli, kuwa Lowassa anaijua siasa na sanaa ya mawasiliano katika siasa. Katika mahojiano yale ya jana kwenye TBC, Lowassa aliwavuta anaowasiliana nao kwa kuanzia na mada husika na mahali alipochagua kufanyia mahojiano, palionekana kuwa ni nyumbani kwake, kule Dodoma.

Kwa muonekano, Lowassa alionekana yuko simple. Alikaa kwenye kochi karibu kabisa na mwandishi anayemhoji. Na mwandishi naye alikaa kulia kwa Lowassa kwenye kochi linalofanana na la Lowassa.

Tulimwona Lowassa akiongea kwa utulivu na kwa mpangilio, Edward Lowassa ni mahiri wa rhetorik, sanaa ya kuongea. Katika dakika chache zile, Lowassa aliweza kuunganisha yaliyotokea Egypt na ya ’binadamu wadogo’ wa hapa kwetu na mahitaji yao, akiwa na maana ya mahitaji ya watu wadogo. Lowassa ni Mmasai, labda Umasaini kuna ng’ombe na binadamu tu!

Na hapa mtaona tofauti, miezi kadhaa iliyopita tuliona kupitia TBC, mahojiano ya Ben Mkapa na mwandishi Edson Sanga. Mkapa alikuwa akitoa maelezo kuhusu kazi yake kule Sudan, mahojiano yale hayakuwa na mvuto, ni kuanzia kwenye upangaji wa scene ya mahojiano. Mkapa alikaa kwenye kochi akiongea huku akiangalia chini na huku anayemhoji akiwa kushoto kwake amekaa kwenye kito tofauti na Mkapa na umbali wa mita kadhaa. Ni heri mwandishi angemhoji Mkapa kwa njia ya simu.

Naam, siasa ni burudani pia, tusubiri ya usiku wa leo, kwenye TBC1. ITV na kwingineko!
Maggid
Iringa,
Jumapili, Februari 13, 2011
mjengwa
 
Majjid acha kutupumbaza watanzania, awe ana sanaa ya mawasiliano, awe sijui na upuuzi gani unaosema, kwa kifupi HATUMTAKI LOWASSA, mie Rais Dr. Slaa kwisha kazi hawa CHUI wanaovaa ngozi ya kondoo kipindi hiki ili tuwaone wema hawana nafasi kwetu. Inamaana Majjid wewe umesahau Richmond na Dowans mpaka uandike haya leo hii? Mbona siye bado machungu ya dowans yanaichoma mioyo yetu, huyu hata aseme nini, hatumtaki full stop!
 
Njaa mbaya , ili lishida lililopo la umeme we majid hulioni.? Chanzo chake nani......? Huyo bwana angetekereza wajibu wake kikamilifu na kuacia kampuni iliyoshinda zabuni ya umeme wa dharula leo hii hali ingelikuwa hivi..........? Nimekudharau kuanzai jana. Nenda kijijini kwenu iringa kawahadae.
 
Ndugu Zangu,

Lowassa alianza kwa kuwapongeza wanaharakati wa Misri. Akazungungumzia madhara ya viongozi kujilimbikizia mali, umuhimu wa viongozi kusoma alama za nyakati, athari za ubepari, umuhimu wa viongozi kusikiliza matatizo ya watu wao na mengineyo. Kimsingi, Edward Lowassa alizungumzia masuala yanayowahusu ' People On The Streets'- Watu wa mitaani, na kwa lugha inayoeleweka na watu wa mitaani.

mjengwa
Is Lowassa in the state of delusion??

cant believe he talks about himself katika third party mode
 
hata kama ni jamaa ni fisadi,anaposema ukweli basi anasitahiri pongezi.
Hakuna binadamu mkamilifu duniani, hilo ni lazimatuliellewe.
Mbona viongozi wengine akiwemo Membe wamekaa kimya na wizara zao?
Jamaa kaongea ukweli, hata mkikataaa huo ndio ukweli.
Nakumbuka hata kule Arusha jamaa alitoa tamko kali sana la kuomba CCM na CDM watafute njia ya kukaa pamoja ili wamalize tofauti zao.
huyo ndio mwenyekiti wa kamati ya mambo ya nje, leo amesema kutosikiliza wananchi na kutosoma alama za nyakati ndio sababu ya viongozi kuchokwa na kuondolewa madarakani.
Lakini pia tofauti kubwa ya kipato kati ya walionacho na wasionacho ametaja kama mojawapo ya sababu.

TBC1

My take:
Siamini kama anayosema yanatoka moyoni.
Nimeamini Lowasa yuko mbioni kugombea urais, hizi movie anazocheza sijui kama zitamsaidia tusubiri tuone.
 
Jamani huyo Mggid sio kwamba hayo ni mawazo yake jamani?
yeye amendika kulingana na yeye alivyokuwa akimwona mhusika sasa anatatizo gani?
ni mwandishi wa habari na anauhuriu wa kuchambua kwa mtazamo wake.
Lazima tukubali kutofautiana kwa hoja
Ndugu Maggid:
Ninaheshimu sana michango yako, na kile unachokiamini bila kuyumbishwa na kauli za Wale wasiokubaliana na wewe.
Lakini nina haya yafuatayo ya kukuuliza:

(1) Hivi Wananchi wa Tanzania wako tayari kumchagua mtu kwa sababu ya utaalamu wa sanaa ya mawasiliano na si uwezo wa kusimamia sheria na kanuni za nchi yetu kama vile sheria za Procurement?, ambazo zilivunjwa na hatimaye kutuletea kampuni feki ya Richmond?
(2) Wewe Maggid unazungumzia Umuhimu wa Ujamaa lakini unafahamu huyo Lowassa ni Bepari Mzuri tu , hivi unadhani Bepari akichukua nchi hii atasimamia sera za kijamaa zenye manufaa? mbona unajicontradict Mkuu?!
(3)Unasema Lowassa aliwavuta anaowasiliana nao, Mkuu hii conclusion umeipata wapi?, hizi statistcs umezipata wapi?.. hebu tuambie ni wangapi uliowahoji wameonekana kuvutiwa na hayo maelezo ya Lowassa na wangapi Hawakuwa impressed?.

Mkuu Maggid, Watanzania wa leo siyo watanzania wa Jana, Kilichomvua Uwaziri mkuu Lowassa ndio hicho hicho kitakamchomfanya asiwe Raisi wa Jamhuri ya Muungano w Tanzania!.
Kama ni uwezo wa Kuvuta watu, Bingwa alikuwa nduli Iddi Amini Dadaa, huyo alikuwa Comedian Mzuri, lakini si kiongozi mzuri!, Hitler naye alikuwa bingwa wa kuongea na kuvuta watu, lakini naye hakuwa kiongozi mzuri! mimi ninadhani kwamba UWEZO WA KUJENGA HOJA BILA UADILIFU HAKUTOSHI KUMFANYA MTU AKAKUBALIKA KWA WANANCHI, LABDA NA WANANCHI WENYEWE SIJUI WAWE NI WATU WA NAMNA GANI!.
 
MAJJID,umeanzia JF then uende kwenye magazet,LOWESER amesomea sanaa pale udsm,cshangai kwa hilo,lakini umeonyesha UKASUKU wako kwa kumpamba,hakuna mtu asiyejua nia ya LOWESER lakini usijifanye wewe ndo wakala wake kwa kumzungumzia,kwni ye kukaa karibu na mwandish ndio nini?mbona unaleta hoja nyepenyepe?nikikuita KANJANJA nimekosea?kama EL ni workalcoholic ni yeye lakini ufisad hautamwacha,hata apewe kamat gani,haijalish,bado ni mchafu,yeye atuambie je cyo TAJIRI?
 
Majjid acha kutupumbaza watanzania, awe ana sanaa ya mawasiliano, awe sijui na upuuzi gani unaosema, kwa kifupi HATUMTAKI LOWASSA, mie Rais Dr. Slaa kwisha kazi hawa CHUI wanaovaa ngozi ya kondoo kipindi hiki ili tuwaone wema hawana nafasi kwetu. Inamaana Majjid wewe umesahau Richmond na Dowans mpaka uandike haya leo hii? Mbona siye bado machungu ya dowans yanaichoma mioyo yetu, huyu hata aseme nini, hatumtaki full stop!
hivi hata mwizi pindi anapoongea mazuri na yenye maana ni lazima yapingwe tu?
tuache mchezo wa kutaka kupinga kila kitu kisa ni Lowasa, kweli hapo tutakuwa tunapotoka sana.
We criticize kunapokuwa na madudu kama hayo ya RICH,DOWANS etc lakini kunapokuwa na mazuri lazima pia yasemwe(Praise on good thing).
Ukeli utabakia pale pale tu jamaa anauwezo wa kuthubutu wa kufanya maaamuzi makali na yenye mzingi kuliko hao wenzake.
yuko wapi Membe? si hiyo ndio wizara yake?
 
Jimmy Cliff mwanamuziki maarufu wa REGGAE aliwahi kuimba katika moja ya riwaya zake muziki wa "TIME WILL TELL". Zama hizi hatuhitaji maelekezo au mtizamo wa mmoja wetu ili tupate mhemko. MUDA UKIFIKA mambo yatakuwa dhahiri kama huko kwenye nchi ya zama za FARAO. Mungu Ibariki Afrika na viongozi wake, bila kuwasahau watu wake
 
Nyie BINADAMU WADOGO WADOGO kelele zenu haziwezi kumuumiza kichwa BINADAMU MKUBWA [Mvi]
 
hata kama ni jamaa ni fisadi,anaposema ukweli basi anasitahiri pongezi.
Hakuna binadamu mkamilifu duniani, hilo ni lazimatuliellewe.
Mbona viongozi wengine akiwemo Membe wamekaa kimya na wizara zao?
Jamaa kaongea ukweli, hata mkikataaa huo ndio ukweli.
Nakumbuka hata kule Arusha jamaa alitoa tamko kali sana la kuomba CCM na CDM watafute njia ya kukaa pamoja ili wamalize tofauti zao.
 
hivi hata mwizi pindi anapoongea mazuri na yenye maana ni lazima yapingwe tu?
tuache mchezo wa kutaka kupinga kila kitu kisa ni Lowasa, kweli hapo tutakuwa tunapotoka sana.
We criticize kunapokuwa na madudu kama hayo ya RICH,DOWANS etc lakini kunapokuwa na mazuri lazima pia yasemwe(Praise on good thing).
Ukeli utabakia pale pale tu jamaa anauwezo wa kuthubutu wa kufanya maaamuzi makali na yenye mzingi kuliko hao wenzake.
yuko wapi Membe? si hiyo ndio wizara yake?
Yaani ndugu yangu unakubali EL ni mwizi halafu unasema tumsikilize, we hujui matapeli huwa wana lugha kama za Lowasa, yeye ni mwizi na ataendelea kuwa mwizi, hatumtakiiiiiiiiiii!
 
Back
Top Bottom