lowassa azidi kunena kuhusu amani

regam

JF-Expert Member
Jan 4, 2011
269
51
Ndugu wana jf wenzangu naangalia mawaidha ya fisadi wetu lowasa wakati wa uzinduzi wa studio ya wasanii wa tz. Anaendelea kusisitiza eti tz inaongoza kwa kuwa na amani ukilinganisha na majirani zetu. Sasa ninachojiuliza hivi hii amani tunayoambiwa tunayo watz ni ipi? Hivi ni vigezo gani vinavyoonyesha kwamba mtu ana amani? Hivi amani ina maana gani kama hali ya maisha ni ngumu? Mafuta juu, gesi juu, ajira ngumu, mazingira ya kuanzisha biashara magumu? Hivi hii ni amani kweliiiii?
 
It could make sense if he convince the government to stop paying Dowans. Otherwise kwangu hii amani ambayo inaambatana na dhuluma na wizi wa waziwazi kwa watu maskini wa Tanzania ni uongo usio na kipimo.
 
Inategemea uelewa wa mtu wa maana ya amani. Yeye akishakuwa na vyote anavyohitaji basi, amani imepatikana. Ni vigumu kubadilisha akili za mwanasiasa wa namna hiyo katika Taifa lenye umaskini wa kiwango chetu Tanzania. Pia ni kupoteza muda kumjadili kipofu aliyeamua kupingana na wenye macho.
 
AMANI? kwani Tanzania kuna au UTULIVU, hawa wajinga mafisadi AMANI ndio umekuwa wimbo wao wa taifa wa kutuibia au kukwapua mali za nchi yetu na makodi yetu. Amani wakati Mtanzania haujui atakula nini asubuhi, mchana, usiku au kesho yake. Ukweli ni kuwa tanzania hawana Amani mpaka Mafisadi wakimbizwe na mikwaju maana tumeshachoka na wimbo wao wa amani. Wapumbavu sana Hawa mafisadi wanatuibia halafu wanatuambia kuwa tuwe kimya ili wazidi kuiba vizuri. :frog:
 
Mpenda TZ nakupa 5. Umekata kiu ya wengi. Yeye anatafuta Amani kwani vurugu lolote litasambaratisha mali zake alizochuma kwetu. Sisi vurugu kwetu ni neema ya kupata katiba mpya. Akitaka urais 2015 amtaje mmiliki wa Richmond
 
Hata mimi nimemuona lakini hotuba ile ilikuwa kama hadhari juu ya vuguvugu la kisiasa linaloendelea na ndiyo maana aligusia katiba. Ni kama alitaka kujibu mapigo lakini akagundua moto utawaka, akaamua kugusia amani maana hilo ndiyo changa la macho la watanzania!!!!!
 
Anabembelezea Urais 2015. Kweli watanzania wakimpatia huyo jamaa urais, nitajua kweli tumerogwa
 
Ni kiongozi asiye mwonga, ana vision na nafikiri angetufaa sana kama angebakia kuwa waziri mkuu kuliko huyu wa sasa anayetoa machozi mambo yakimzidia.

Tatizo la Lowassa ni tamaa ya pesa tu, hapa tunapoongea kashafungua redio yake binafsi inatwanga vibaya mno maeneo ya arusha. nafikiri itatumika kwenye kampeni zake za urais 2015. kaeni mkao wa kula.

Lowassa ukitaka uraisi wa nchi hii ni vere simpo:-

1. Kama uliiba / au kulaghai pesa za umma kwa watanzania basi warudishie mara nne
2. Tangaza nusu ya mali yako kwa maskini kisha Chukua form za urais.
 
Lowassa ukitaka uraisi nchi hii ni simpo sana

1. Kama uliiba / au kulaghai pesa za umma kwa watanzania basi warudishie mara nne
2. Tangaza nusu ya mali yako kwa maskini kisha Chukua form za urais - tutakupa.

Sasa atatufaaje wakati anatamaa ya pesa?
 
Ni kiongozi asiye mwonga, ana vision na nafikiri angetufaa sana kama angebakia kuwa waziri mkuu kuliko huyu wa sasa anayetoa machozi mambo yakimzidia.

Tatizo la Lowassa ni tamaa ya pesa tu, hapa tunapoongea kashafungua redio yake binafsi inatwanga vibaya mno maeneo ya arusha. nafikiri itatumika kwenye kampeni zake za urais 2015. kaeni mkao wa kula.

Lowassa ukitaka uraisi wa nchi hii ni vere simpo:-

1. Kama uliiba / au kulaghai pesa za umma kwa watanzania basi warudishie mara nne
2. Tangaza nusu ya mali yako kwa maskini kisha Chukua form za urais.

Kuendesha ama kuongoza nchi ni sawa na kufanya biashara kwa faida ya wananchi wote, sasa kama LOWASA ana tamaa ya kusaka pesa kwa faida ya wote (nchi) angetufaa sana lakini kwa kua ni kwa faida yake binafsi hatufai kabisa huyo. Tena hata anaposifia amani iliyopo TZ anatuzuga tu, maana amani ndio imemfanya atuibie sana.
 
Back
Top Bottom