Lowassa awakumbuka vijana uzeeni

MAMA POROJO

JF-Expert Member
Nov 22, 2007
4,974
785
HAKUNA ubishi, ajira ni tatizo kubwa nchini. Tena, vijana ndio waathirika wakubwa wa tatizo hili. Wapo wasiokubali hili, wao wanawaangalia vijana kama ndio tatizo.

Edward Lowassa, waziri mkuu aliyejiuzulu kwa shinikizo za Bunge lililomtuhumu kukiuka maadili ya uongozi katika sakata la mkataba wa kifisadi wa Richmond, “ameisimamia vidole” hoja hii. Amefikia hatua ya kulifananisha tatizo na bomu linalosubiri kulipuka.

Lowassa (59) amenukuliwa katika matukio manne tofauti kuanzia mwishoni mwa mwaka, akionya tatizo la ajira kwa vijana linahitaji kupatiwa ufumbuzi wa haraka.

Tarehe 15 Novemba 2011, akiwa katika harambee ya ujenzi wa Kanisa Katoliki la Mtakatifu Joseph Makasa, Parokia ya Nyakato, Mwanza, alililitaka kanisa lisaidie kujenga vyuo vya ufundi ili kuajiri vijana.

Harambee nyingine ya kusaidia Kanisa, safari hii la Kiinjili la Kilutheri (KKKT), Usharika wa Amani Sabasaba, Singida, 29 Novemba, 2011, Lowassa aligusia suala hilohilo.

Hata alipokutana na waandishi wa habari mkoani Arusha mwaka jana, Lowassa alizungumzia tatizo hilo la ajira. Ni hapa alilifananisha na bomu.

Kwenye sherehe za uzinduzi wa Jimbo jipya la Kanisa Katoliki Ifakara, aliwasihi maaskofu watoe kipaumbele kusaidia kutatua tatizo la ajira kwa vijana.

Inavyoonekana, Lowassa ameamua kulifanya suala hili mtaji mzuri wa kisiasa.

“(Yeye Lowassa) alifanya nini kuondoa tatizo la ukosefu wa ajira kwa vijana alipokuwa Waziri Mkuu, naye waziri Kabaka anastahili kuulizwa, “alichelewa wapi kutoka na kueleza mikakati ya serikali katika kutegua bomu la ajira kwa vijana.”Pia Lowassa angeweza kuulizwa alikuwa wapi katika utumishi wake wa muda mrefu serikalini? Tukumbuke, tatizo hili si la leo wala jana. Mwana-CCM huyo amekuwa katika serikali za awamu zote, hajapata kulieleza namna anavyolieleza sasa.

Au tuseme alishindwa kuwatetea vijana wenzake wakati huo, akasubiri hadi azeeke ndipo awaone vijana wa sasa anaosema ni bomu kwa taifa? Au kwa umri wake huu (wa kustaafu) ndio uwezo wake wa kubaini matatizo yanayowakabili Watanzania umeongezeka?

Lowassa, amekuwa kiongozi katika chama kinachotawala, CCM, tangu ujana wake baada ya kuhitimu Chuo Kikuu, wakiwa ngazi za chini. amepanda hadi kuingia vikao vya juu vya maamuzi vya CCM. Ameshika nafasi za uwaziri hivyo kuwa mjumbe wa Baraza la Mawaziri. amepanda hadi ngazi ya uwaziri mkuu, lakini kipindi chote tatizo la ajira limekuwapo na limekua.

Kimsingi, tatizo hili si jipya nchini.

source: Gazeti la Mwanahalisi tarehe 28 March - 3 April 2012.

My take: Lowassa ameamua kutegua bomu akiwa nje ya system kulikoni?
 
HAKUNA ubishi, ajira ni tatizo kubwa nchini. Tena, vijana ndio waathirika wakubwa wa tatizo hili. Wapo wasiokubali hili, wao wanawaangalia vijana kama ndio tatizo.

Edward Lowassa, waziri mkuu aliyejiuzulu kwa shinikizo za Bunge lililomtuhumu kukiuka maadili ya uongozi katika sakata la mkataba wa kifisadi wa Richmond, "ameisimamia vidole" hoja hii. Amefikia hatua ya kulifananisha tatizo na bomu linalosubiri kulipuka.

Lowassa (59) amenukuliwa katika matukio manne tofauti kuanzia mwishoni mwa mwaka, akionya tatizo la ajira kwa vijana linahitaji kupatiwa ufumbuzi wa haraka.

Tarehe 15 Novemba 2011, akiwa katika harambee ya ujenzi wa Kanisa Katoliki la Mtakatifu Joseph Makasa, Parokia ya Nyakato, Mwanza, alililitaka kanisa lisaidie kujenga vyuo vya ufundi ili kuajiri vijana.

Harambee nyingine ya kusaidia Kanisa, safari hii la Kiinjili la Kilutheri (KKKT), Usharika wa Amani Sabasaba, Singida, 29 Novemba, 2011, Lowassa aligusia suala hilohilo.

Hata alipokutana na waandishi wa habari mkoani Arusha mwaka jana, Lowassa alizungumzia tatizo hilo la ajira. Ni hapa alilifananisha na bomu.

Kwenye sherehe za uzinduzi wa Jimbo jipya la Kanisa Katoliki Ifakara, aliwasihi maaskofu watoe kipaumbele kusaidia kutatua tatizo la ajira kwa vijana.

Inavyoonekana, Lowassa ameamua kulifanya suala hili mtaji mzuri wa kisiasa.

"(Yeye Lowassa) alifanya nini kuondoa tatizo la ukosefu wa ajira kwa vijana alipokuwa Waziri Mkuu, naye waziri Kabaka anastahili kuulizwa, "alichelewa wapi kutoka na kueleza mikakati ya serikali katika kutegua bomu la ajira kwa vijana."Pia Lowassa angeweza kuulizwa alikuwa wapi katika utumishi wake wa muda mrefu serikalini? Tukumbuke, tatizo hili si la leo wala jana. Mwana-CCM huyo amekuwa katika serikali za awamu zote, hajapata kulieleza namna anavyolieleza sasa.

Au tuseme alishindwa kuwatetea vijana wenzake wakati huo, akasubiri hadi azeeke ndipo awaone vijana wa sasa anaosema ni bomu kwa taifa? Au kwa umri wake huu (wa kustaafu) ndio uwezo wake wa kubaini matatizo yanayowakabili Watanzania umeongezeka?

Lowassa, amekuwa kiongozi katika chama kinachotawala, CCM, tangu ujana wake baada ya kuhitimu Chuo Kikuu, wakiwa ngazi za chini. amepanda hadi kuingia vikao vya juu vya maamuzi vya CCM. Ameshika nafasi za uwaziri hivyo kuwa mjumbe wa Baraza la Mawaziri. amepanda hadi ngazi ya uwaziri mkuu, lakini kipindi chote tatizo la ajira limekuwapo na limekua.

Kimsingi, tatizo hili si jipya nchini.

source: Gazeti la Mwanahalisi tarehe 28 March - 3 April 2012.

My take: Lowassa ameamua kutegua bomu akiwa nje ya system kulikoni?
Lowasa kachoka anataka tu kujisafisha na ufisadi wake.
 
Mpeni pole amepoteza dira kama ni meli ilikuwa ikielekea kazini imejikuta ipo kusini mashariki wakumtoa wamemgeuka
 
Huyu mzee angekuwa na washauri wazuri wangemshauri apumzike aachane na siasa. Hakuna cha tatizo la ajira hapa ni kutafuta mtaji wa kisiasa.
 
Nimesoma gazeti la mwanaharisi la jana nimeshangaa kusikia siku hizi ameanza kulazimisha kutoa hotuba kila anapoenda hata kama hakuwa kwenye ratiba.
 
Back
Top Bottom