Lowassa aunguruma Bungeni: "Bora kufanya maamuzi na kulaumiwa, kuliko kutofanya!"

Nimependa hapo penye nyekundu. Tunataka rais anayeweza kufanya maamuzi. Mpaka leo mashirika mengi ya serikali/umma hayana watendaji kwa sababu ya kutofanya maamuzi.
Mtoa mada, subject ni tofauti na ulivyoandika. Ungetoa mada kuwa kasemaje bila kuweka feeling zako halafu ukaacha tuchangie nawe pia uchangie. Ingekuwa vizuri ungenukuu vyote alivyosema na siyo kuchukua tu zile sehemu ambazo wewe unataka kukataa. Weka maelezo yake yote ili ituwezeshe kufanya maamuzi katika kuchangia na siyo utulazimishe wachangia mada au wasomaji kuamini mawazo au kuchangia mawazo yako. Otherwise thread uitume kama mawazo yako au maoni yako kuhusu Lowassa.



Nafikiri wakuu haya ni maoni ya mweka mada na wala sidhani yeye amechukua mawazo ya watu wote humu. Ana uhuru wa kumsifia Lowassa the way anavyotaka ila kwa maoni yangu sidhani kama kuna mtu anayefaa kuwa rais kwa upande wake. Kama anafaa kuwa kiongozi atuambie ni kwa nini nchi ni maskini hadi muda huu na utajiri wa rasilimali tulio nao na atuambie kama viongiozi wamefanya nini kuhakikisha kuwa rasilimali zinatumika kuwaletea maendeleo wananchi na asitupe porojo za makaratasi kuwa uchumi unakua kwa kasi wakati kwa hali halisi umaskini ndo unazidi kuongezeka miongoni mwa watanzania. Wasituletee porojo za kwenye makaratasi ya kukua kwa uchumi wa mifukoni mwao na kufananisha na maisha ya babu na bibi zetu huko vijijini ambako mlo mmoja ni shida na huduma za muhimu kama maji, huduma za afya ni kama anasa kwao
 
kwani ccm wanachaguaje mgombea wao wa urais? si kwa kupiga kura!! im telling you guys jamaa akipigiwa kura tu anapita jinsi alivyo na influence or otherwise watanzania mchague chama kingine 2015! na ukitaka kujua watu makini na sekta zao ndio maana EL humkuti kuongea ongea ovyo na akiongea watu wote wanavutiwa kusikia ataongea nini thats charisma guys. Nape namuhurumia huu mziki hauwezi mzito na kama hajijui anatumiwa na JK kumzima EL kama walivyofanya akina Mwakyembe!
 
Lowassa amemaliza kuchangia hotuba ya Waziri mkuu kwa mbwembwe za kusifia mafanikio ya CC-Magamba kwa miaka 50. Amejidai kusema kwamba tuna maendeleo makubwa sana na hayo ni mafanikio ya Magamba na mtu asiwabeze. Amemshauri Jk kutoogopa kufanya maamuzi mazito kwani ni bora kufanya maamuzi ukakosea kuliko kutofanya kabisa.Ameendeleza porojo za uchumi kuwa unakuwa kuliko nchi nyingi duniani lakini hajaeleza kwa nini mtu wa kawaida kijijini anazidi kuwa maskini. ameshindwa kujua kwamba uchumi unapokua hau-trickle down bali unakingwa juju kwa juu na mafisadi akiwemo yeye kiasi kwamba haufiki kwa bibi na babu zetu kule vijijini.Anazungumzia kuwa barabara zimejengwa nyingi na madarasa bila kueleza hayo madarasa yamezaa vitu gani. Anaangalia quantity bila kuelezea quality kuonyesha kuwa bado ile tabia ya uVIVU WA KUFIKIRI NA KUTOKUWA REALIST KWA VIONGOZI WETU KUNA ENDELEA.Ameni fanya hata kufuta lile wazo kuwa anaweza kufikiriwa kuwa the next presidee 2015 kwani bado ana magamba mengi kuliko wanamagamba wenyewe. Anaonyesha hata kero za wananchi hazijui tena halafu anataka urais sijui kwa ajili ya kitu gani. Nilifikiri pia atakuja na kitu tofauti na Magamba kumbe yake yeye ni makubwa zaidi.

Hapo kwenye RED maamuzi magumu atayajuwa baada ya zile siku 90 alizopewa na Nec ya ccm.
 
Lowassa has 9 lives!
Wabunge wameshangilia mbaya! ......watanzania wanajua na dunia inajua.

I have to admit, he has scored some points with respect to 2015. Huyu jamaa hawawezi kumvua gamba.

9 lives! - nimeipenda hiyo!

attachment.php
 
mambo ya mgao wa umeme huku mitaa ya ubungo bunge lilipoanza tu tanesco wakachukua umeme wao nasikitika sikumuona lowasa akichangia maana ni siku nyingin sana sijamsikia akiongea bungeni.
 
Si ajabu ikawa mara yake ya mwisho kuongea bungeni! Gamba halitaishia kwenye NEC baada ya NEC watasema na Ubunge pia!!
 
anashangiliwa ile mbaya, huyu jamaa anafaa kuwa president, tujenge reli ya kati, tupanue bandari tanga, dsm pesa tunazo, tumejenga udom kwa pesa zetu wenyewe

Mkuu umesahau bibi kiroboto a.k.a matoto ya ndege alisema si kila wakati wabunge wakipiga makofi wanashangilia, wakati mwingine wanazomea!!
 
anashangiliwa ile mbaya, huyu jamaa anafaa kuwa president, tujenge reli ya kati, tupanue bandari tanga, dsm pesa tunazo, tumejenga udom kwa pesa zetu wenyewe

Sijui ni watu wangapi wanapiga kura kwa vigezo kama vyako,..
siwezi sita kuwaita wapumbavu
 
bila shaka safari ya lowasa kule naigeri imeanza kuzaa matunda. Kwa kweli wabunge wa ccm wameanza kumkubari tunako elekea huenda asiwe ghamba tena na gamba labda awe mkuu mwenyewe, na losatam atakuwa ameenda huko huko naigeria make haonekani mjengoni.
Naigeria si mchezo ndo mwisho wa kila kitu.
Lakuvunda Halina ubani. Ndio maana tunashauriwa kuchunga ndimi, kuchunga vitendo vyetu, na kuchunga haiba zetu wakati wote ili kwa wanaowania madaraka ya umma, wasije wakatayahali wanapopumbazwa na mwangwi wa matendo yao ya nyuma....na ukiwa na uroho wa vijisent usio na staha..ukigundulika umeumia kwani hutatakasika hata ukiogea sabuni ya unga.
 
Si ajabu ikawa mara yake ya mwisho kuongea bungeni! Gamba halitaishia kwenye NEC baada ya NEC watasema na Ubunge pia!!
Hii sasa ni ndoto ya machana kwa jinsi navyoifahamu CCM haiwezi kufanya maamuzi magumu kama hayo!!
 
bila shaka safari ya lowasa kule naigeri imeanza kuzaa matunda. Kwa kweli wabunge wa ccm wameanza kumkubari tunako elekea huenda asiwe ghamba tena na gamba labda awe mkuu mwenyewe, na losatam atakuwa ameenda huko huko naigeria make haonekani mjengoni.Naigeria si mchezo ndo mwisho wa kila kitu.
Nitarudi badae kidogo acha kwanza nilitafakari hili jambo
 
quote_icon.png
By MVUMBUZI Amemshauri Jk kutoogopa kufanya maamuzi mazito kwani ni bora kufanya maamuzi ukakosea kuliko kutofanya kabisa.
Subiri siku 90 ziishe JK ataufanyiakazi ushauri wako.
 
Back
Top Bottom