Lowassa aponda nguvu ya umma

...my bro Edo you'r press the wrong button...NGUVU YA UMMA ISIKIE KITU USIOMBE IKUSHUKIE,KAMA HAUTAAMINI HAYA MANENO YANGU BASI JARIBU KUGOMBE URAIS 2O15,NDO UTAJUA NGUVU YA UMMA NI NINI...
 
Lowassa anaponda nguvu ya umma? kwa mtaji upi alionao Lowassa mpaka aone nguvu ya umma ni bure? Lowassa anapata wapi hiki kiburi cha kuhoji nguvu ya umma? Au kwa sababu ameshawanunua maaskofu na wachungaji? Kwani hela anazochanga si mali ya watanzania? Viongozi wa makanisa wameguka Yuda Eskarioti kwa kupokea vipande 30 ili tuwe mikononi mwa himaya ya bwana pesa!

Kama ambavyo wanamtandao wameivuruga kabisa CCM, sina shaka hata kidogo kuwa hawa mabwana watavuriga kanisa. Kwa sasa watu wanaongea kichinichini lakini muda utafika waumini watapaza sauti. Hela shetani!
 
lowasa ni mnafiki sana , hivi sasa hivi yeye siasa anafanya makanisani tu? karibu atahamia miskitini na vyuoni, hapo kiama kinakuja
 
Kwa swala la harambee nadhani ni vizuri taasisi zikaendelea kumtumia maana yeye na wezi wenzie wanatoa hela walizokwapua ambazo mzee wa kaya hawezi kuwalazimisha kuzirudisha. Nji hii ya yeye na marafiki zake kurudisha japo tone la zile walizoiba si wazo baya. Nadhani taasisi nyingine ziige huo mfumo. URAISI ATAUSIKIA KABURINI ILA KWA TANGANYIKA YETU NOOOOOOOOOOOOOOOOOO.
Wale wapambe wake wa humu JF mwambieni EL kuwa nguvu ya umma hawezi kuipinga sasa maaana ufahamu wa wananchi juu ya shida zao na anayezisababisha ni mkubwa mpaka vijijini nowadays. He is too late japo mdomo ni mali yake anaruhusiwa kusema tu.
 
Teh teh HAYO MAKANISA ndio vinara wa ufisadi unafikiri itamtupa mkono? MOU KAILETA LOWASA,makanisa mengi yanajengwa kwa pesa za ufisadi,
 
lowasa ni mnafiki sana , hivi sasa hivi yeye siasa anafanya makanisani tu? karibu atahamia miskitini na vyuoni, hapo kiama kinakuja

Mkuu hapo kwenye green mbona tayari alishaichangia BAKWATA, yeye anaponda nguvu ya umma kwa vile anategemea nguvu ya uchawi wa ki -Nigeria. ALAANIWE FISADI LOWASA NA MTANDAO WAKE UNAOJIITA FRIENDS OF LOWASA.
 
pamoja na kumsifu lowassa kutumia lugha ya staha kuliko magufuli, namweleza kuwa cdm imeshaanza kufanya mchakato wa kukusanya maoni ya wananchi kuhusu kero na maendeleo
 
Teh teh HAYO MAKANISA ndio vinara wa ufisadi unafikiri itamtupa mkono? MOU KAILETA LOWASA,makanisa mengi yanajengwa kwa pesa za ufisadi,

Usisahau kuwa na BAKWATA nao wameshalamba hela ya huyu fisadi , sijui hapo unaelezaje usaadh Pachoto,
 
BOOKMARK THIS PAGE

bot_tabimg.gif

Lowassa aponda nguvu ya umma Send to a friend
Tuesday, 10 January 2012 21:07
0diggsdigg

Anthony Kayanda, Kigoma
WAZIRI Mkuu aliyejiuzulu, Edward Lowassa, ameibuka na kukemea matumizi ya nguvu ya umma, yanayoendeshwa na baadhi ya vyama vya siasa nchini kushinikiza mambo mbalimbali, akisema hayalifikishi taifa popote.

Akizungumza katika harambee ya kuchangia ujenzi wa Sekondari ya Kanisa la FPCT Bigabiro, mkoani Kigoma, Lowassa alisema nguvu wanazotumia wanasiasa kuhamasisha nguvu ya umma, ingefaa kutumika kushiriki kazi za maendeleo ili kuliletea taifa maendeleo endelevu.
Ingawa Lowassa hakutaja chama cha siasa kwa jina, lakini Chadema ndicho ambacho kimekuwa kikitumia kauli mbiu ya Nguvu ya Umma (Peoples Power) kushinikiza mambo mbalimbali.

"Badala ya kuonekana wakihamasika kufanya maandamano ya kupambana na Serikali, jambo ambalo halitasaidia taifa kuondokana na umasikini, nguvu hiyo ingetumika kushiriki kazi za maendeleo," alisema Lowassa.

Alisema miradi mingi ya maendeleo imekuwa ikikwama kutokana na wananchi kukataa kushiriki kujitolea nguvu zao kwa kufanya kazi, badala yake, wanataka kulipwa fedha kutekeleza miradi maeneo yao.

“Nguvu ya umma tunayoshuhudia kwenye maandamano ya baadhi ya vyama vyetu, ingekuwa inatumika kwa kiwango kilekile kufanya kazi za kujitolea kwenye miradi ya maendeleo kama ujenzi wa sekondari zetu, hakika taifa lingepiga hatua kubwa ya maendeleo, lakini linapokuja suala la kufanya kazi nguvu ya umma hutoweka,” alisisitiza Lowassa.


Harambee
Katika harambee hiyo, Lowassa na rafiki zake walichangia Sh60.5milioni taslim na kufanya michango yote kufikia Sh125 zikiwamo ahadi.

Lowassa alisema elimu ikitiliwa umuhimu ni wazi taifa litajikomboa kutoka kwenye hali duni kwa kuwa litakuwa na watu wenye uelewa wa kutosha juu ya mabadiliko na mifumo mbalimbali ya dunia, kiasi kwamba itakuwa rahisi kufundishwa na kuelekezwa mambo muhimu.
“Baada ya kubaini hakuna usawa katika taifa, tulilazimika kutembea nchi nzima kuhamasisha ujenzi wa sekondari za kata ili kila eneo watoto wasome. Watoto wa Kigoma wawe kama wenzao wa Kilimanjaro au mikoa mingine iliyopata mwanga wa elimu mapema, ndiyo maana angalau watoto wengi wanafika kidato cha nne sasa ikilinganishwa na miaka ya nyuma,” alisema Lowassa.

Ajira
Lowassa alitumia harambee hiyo kurejea kauli yake kuhusu tatizo kubwa la ukosefu wa ajira kwa vijana nchini, ambao wamehitimu masomo yao ngazi mbalimbali lakini wanaishia mitaani bila kupata kazi zinazoeleweka.
Alisema tatizo la ajira kwa vijana ni bomu linaloweza kulipuka wakati wowote na kuleta shida kwa taifa, kwa vile ndiyo nguvu kazi inayohitajika zaidi kujenga uchumi imara wa nchi, hivyo kusaidia kuondokana na umaskini, mfumko wa bei na hata kudorora kwa uchumi.

“Nimekuwa nikilisemea sana suala hili la ukosefu wa ajira kwa vijana, kiasi kwamba kuna watu walinibatiza jina la Yohana Mbatizaji, lakini bado natoa mwito kama jamii tutafakari kwa makini jambo hili,” Lowassa alirejea kauli hiyo na kuongeza:
“Kila tunapokutana kwenye semina na makongamano tulijadili kwa kina, vinginevyo tutakuja kujilaumu siku moja kwa sababu hata wanaohitimu vyuo vikuu, wanaopata ajira ni asilimia tano tu kwa mwaka.”

Alimtaka Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Luteni Kanali mstaafu Issa Machibya, kusaidiana na kanisa hilo kuwashawishi watu wanaomiliki eneo inapojengwa sekondari hiyo, wapunguze gharama za fidia ya ardhi na mazao yao ya kudumu, inayofikia Sh75milioni kwa madai kwamba ni nyingi ikilinganishwa na thamani ya mradi unaotekelezwa.

Mchungaji
Awali, katika risala yao iliyosomwa na Mchungaji Kiongozi wa Kanisa hilo la FPCT Bigabiro, David Nkone, alisema wameamua kujenga sekondari ya kidato cha kwanza hadi sita kutokana na uhaba mkubwa wa sekondari za ngazi hiyo mkoani Kigoma, hususan zenye michepuo ya sayansi.

Mchungaji Nkone aisema Chuo cha Theolojia cha FPCT Bigabiro kinachotoa mafunzo ngazi ya stashahada pia kinakusudiwa kupanuliwa na kufikia kutoa Shahada, hivyo kuongeza fursa za elimu na ajira kwa baadhi ya Watanzania.

Kanisa hilo lilimteua Lowassa kuwa mlezi wa sekondari hiyo aliyowekea jiwe la msingi ambayo kwa sasa ina madarasa matatu yaliyofikia hatua ya rinta, lengo likiwa ni kujenga madarasa ya kidato cha kwanza hadi sita.

Katika hatua nyingine, mjumbe wa Halmashauri Kuu (Nec) ya CCM Mkoa wa Kigoma, Muhsin Abdallah Sheni, aliahidi kuchangia Sh10 milioni na kompyuta mbili, huku Mbunge wa Kigoma Mjini, Peter Serukamba akiahidi Sh3 milioni, Mbunge wa Viti Maalumu, Josephine Ngenzabuke aliahidi kutoa Sh2 milioni na Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Luteni Kanali Machibya akiahidi Sh2.5 milioni.

hv bado analipwa kama waziri mkuu mstaafu?
 
Yeye si kiongozi wa chama chake? Kama kweli anaamini katika kujitolea nguvu ngazi kunaweza kusababisha mabadiliko kwa nini yeye anajitolea fedha? Au kwa nini hahamasishi wana CCM kujitolea hizo nguvu kazi?
Natamani sana maneno haya yangemfikia
 
Ole wenu viongozi wa dini mnao endekeza pesa kuliko uadilifu!!!
Ole wetu watanzania tukimruhusu EL kuingia ikulu kama rais;atalipa vipi fadhila za hawa ndugu zake wanaomwaga mamilioni makanisani?
"Niwezalo nimefanya,kufundisha na kuonya,
Ole wake Tanzania,tusipoisaidia!!!!",MWL JK NYERERE
 
God forbid, Lowassa will NEVER be the next president of this nation. Never!

Inavoonekana Lowassa kweli amekamia URAHISI 2015. Waswahili husema mkamia maji hayanywi!Hatakuwa Rais hata kama atawahonga Watanzania wote kwa hela zake chafu zaufisadi.

Lowassa kama ana BUSARA anatakiwa ajihoji mara mbililimbilikama kweli anaweza kuwa Rais wa Tanzania wakti kuna TUHUMA lukuki zinazo mwandama.Mbali na UFISADI kwa sasa Lowassa anapaswa ajibu hoja ya KUHUSU UGONJWA TATANISHI WA DR.MWAKYEMBEmaana kuna tetesi kuwa yeye ndo amehusika kum-mwakyembe maskini Mwakyembe.
Mimi nawashangaa hata hawa mapdre na maaskofu wanao mwalikamakanisani kuchangisha pesa za harambee. Bila shaka inavyo elekea hizi ni mbinu mkakati za kujiimarisha na kutaka kutambulika kwa watu ili ifikapo 2015 awe na wafuasi wengi. Ni wajinga tu kama yeye huko CCM ndo wataweza kumpa Urahisi wa nchi hii.
 
BOOKMARK THIS PAGE

bot_tabimg.gif

Lowassa aponda nguvu ya umma
Send to a friend
Tuesday, 10 January 2012 21:07
0diggsdigg



“Nguvu ya umma tunayoshuhudia kwenye maandamano ya baadhi ya vyama vyetu, ingekuwa inatumika kwa kiwango kilekile kufanya kazi za kujitolea kwenye miradi ya maendeleo kama ujenzi wa sekondari zetu, hakika taifa lingepiga hatua kubwa ya maendeleo, lakini linapokuja suala la kufanya kazi nguvu ya umma hutoweka,” alisisitiza Lowassa.


Ni kweli kabisa nguvu ya umma itumike kwenye maendeleo si migomo na maandamano tu.Kenya wenzetu wanaita HARAMBEE.Wanaweza kusanya nguvu ya umma kuchangia mtoto kwenda kusoma best univercity nje ya nchi.

Nguvu ya umma ingetumika kuokoa wahanga wa mafuriko Dar es salaam ingekuwa na maana sana na muda mfupi tu kusingekuwa na mtu juu ya bati au Miti kwenye yale mafuriko.Lakini unakuta hao watu wanaitisha nguvu ya umma na huo umma wao uchwara wako wanaitizama tu serikali inavyohangaika kuokoa wakirekodi udhaifu wa uokoaji kwenye vimemo ili waitishe baadaye nguvu ya umma kuizomea na kuilaani serikali baada ya watu kufa na kuathiriwa na mafuriko na kujifanya wanapeleka vimisaada koko kwa wanusurika kufa na mafuriko waliookolewa na serikali wakawekwa kwenye makambi.Siasa za majitaka za kiwango cha juu.Nguvu gani ya umma inapenda kuwatembelea kwenye makambi nchi kavu badala ya kuingia kwenye mafuriko kuwaokoa? Hii ni Stupid peoples power.

Niseme tu kuwa Lowasa kwa hilo la shule za kata kajitahidi mno.Mijini kuna watu wanadharau hizo shule kwa kuwa wana altenative nyingi lakini vijijini hizo shule ni mkombozi mkubwa na watu wanajivunia uwepo wake.Nilimkuta mkenya mmoja akasema watanzania mnatuacha nyuma wakenya yaani sekondari za day ziko hadi vijijini maporini kabisa kuhudumia wanavijiji.Kenya sekondari nyingi ziko karibu na market maeneo ya wenye nazo wawezao lipia tofauti na hizi za kata.Kenya ukiona shule iko porini nyingi za bweni za watoto wa wenye nazo ambao wanataka watoto wao wasome maeneo tulivu mbali na kelele za ma-prado na ma-benz yao.

Mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni.

kingadvisor@yahoo.com
 
Mnashangaa nini fisadi kukerwa na nguvu ya umma? Mnategemea apendezwe na nguvu ya umma inayopinga usifsadi.

Jamaaa Nyerere alimtoa nishai...akaachia kimya kimya kinyang'anyiro cha urais 1995...baadaye Mwakyembe akamuumbua akaachia uwaziri mkuu...watu bado wanaona anafaa kuwa rais wao! Ama kweli watz tunapenda kuendelea kunyonywa.
Lowassa ni condemed fisadi...atakuwa Mobutu wa bongo...oooh!
Nalaaani madhehebu ya dini yanayofaidi kwa harambee za ufisadi....hakika hayafanyi kazi ya Mungu bali ya matumbo yao.
 
Back
Top Bottom