Lowassa apanda chati kuelekea uchaguzi mkuu 2015

Tunakumbuka wakati Lowassa baada ya kuhamishwa kutoka Wizara ya Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu na kupelekwa Wizara ya Ardhi na Maliasili alikuta madudu mengi na kuanza kupambana nayo kwa ujasiri mkubwa wa ajabu.

Kulikuwa na wajanja wachache ndani ya halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam walitaka kuuza viwanja vya Mnazi Mmoja kwa mfanyabiashara mmoja maarufu, Lowassa alitoa tamko la serikali akiwa bungeni Dodoma akitaka mfanyabiashara huyo aondoke haraka eneo hilo kwa kuondoa uzio alikuwa ameujenga na ndipo wananchi wakavamia na kuchukuwa mapati yote.

Watanzania wanamuitaji "jembe" Lowassa.

Haki ya nani njaa mbaya na wewe tayari umelipwa kuja kusafisha fisadi hapa jamvini. Haiwezekani mtu ukageuka ghafla kiasi hiki kama sio fedha za kifisadi zimekuzukia. Wewe kula hizo pesa kwa kuwa hakuna atakeyekuja kukudai kuwa hukufanikisha kile mlichokubaliana!
 
Lowassa ndio kiboko yenu nyie, ndio maana hofu limewajaa, mkwe wake kushindwa haihusiani kabisa, nikuulize,wewe dada yako akiposwa na wewe unavishwa pete?

hujui alichofanya na nguvu alizotumia huelewi ndo maana unakurupuka! i think we need him, to me he is a very wrong contender!i can bet on this kama hamuamini! kinachombeba san sana ni pesa anazohonga, ikumbukwe hizo pesa aliziiba akiwa mtumishi wa serikali, itafika muda atatueleza alipata wapi hizo pesa!
 
Hivi hii thread Nape kaiona, nijuavyo mimi Nape na Lowasa ni kuku na mtama, akiiona hii thread hakika huyu ritz kapoteza mshahara wa leo

Sio mie ni Watanzania ndio wanamkubali Lowassa rekodi yake ya utendaji ndio inambeba hata ukimchukia ni kazi bure mkuu katika Watanzania 10 wakihojiwa saba kati yao wanamkubali.
 
Ritz hili ndo tatizo la kukurupuka! alipotoka huko kaacha madudu na alipoingia akaongeza madudu, lowasa kajimilikisha viwanja vingapi akiwa waziri waardhi?je migogoro mikubwa ya ardhi imeanza kipindi gani na kwa nini?viwanja vingapi vimeuzwa mara mbili akiwa wizarani pale?ninawashangaa, yule hana busara sema anakurupuka, ndo maana hata juzi alikimbia kusema nchi ipo tayari kwenda vitani wakti wa mzozo wa ziwa nyasa!njia tatu mliona zilivyoua watu! shortly he is not a leader instead ni mtawala! na hii nchi tumechoka watawala tunataka viongozi!
 
Last edited by a moderator:
Haki ya nani njaa mbaya na wewe tayari umelipwa kuja kusafisha fisadi hapa jamvini. Haiwezekani mtu ukageuka ghafla kiasi hiki kama sio fedha za kifisadi zimekuzukia. Wewe kula hizo pesa kwa kuwa hakuna atakeyekuja kukudai kuwa hukufanikisha kile mlichokubaliana!

Mkuu wangu hivi saizi una viwanda vingapi vya kutunga uongo.
 
hili ndo tatizo la kukurupuka! alipotoka huko kaacha madudu na alipoingia akaongeza madudu, lowasa kajimilikisha viwanja vingapi akiwa waziri waardhi?je migogoro mikubwa ya ardhi imeanza kipindi gani na kwa nini?viwanja vingapi vimeuzwa mara mbili akiwa wizarani pale?ninawashangaa, yule hana busara sema anakurupuka, ndo maana hata juzi alikimbia kusema nchi ipo tayari kwenda vitani wakti wa mzozo wa ziwa nyasa!njia tatu mliona zilivyoua watu! shortly he is not a leader instead ni mtawala! na hii nchi tumechoka watawala tunataka viongozi!

Mkuu wang JF sio sehemu ya porojo ebu leta ushahidi wa hivyo viwanja alivyojimilikisha, mkuu bila Lowassa viwanja vya mnazi mmoja vingekuwa havipo vilikuwa vimeishauzwa na Halmashauri ya Jiji Lowassa kavirudisha kwa wananchi dogo hilo.
 
Wanabodi,

Wakati mchakato wa Uchaguzi ndani ya Chama cha Mapinduzi CCM unaendelea kuanzia ngazi ya shina hadi taifa. Mbunge wa Monduli Edward Lowassa anaonekana kupanda chati kwa kasi ya ajabu na kuonekana ana nafasi kubwa katika mbio za urais 2015.

Uchambuzi wa kisiasa unaonesha karibu kila kona ya nchi hii, katika watanzania 10 utakaowahoji kuhusu ni nani hasa anayefaa kumrithi Rais wa sasa Kikwete, saba kati yao wanamtaja Lowassa wakidai ni "Jembe" linalopigania haki na maendeleo ya kila Mtanzania.

Makundi makubwa yanayotajwa katika mnyukanakano huo ni pamoja na kundi la Lowassa, Samwel Sitta, na Bernad Membe. Kila mmoja anapambana kufa na kupona kuhakikisha kwamba wanaingiza watu wao muhimu katika vikao vya (NEC) na ndani ya Jumuiya za chama hicho, UVCCM, UWT, na Wazazi, katika makundi yote hayo Lowassa anaonekana kuwa ni mtu makini ana nafasi kubwa ya kupenya na kupererusha bendera ya chama hicho.

Kusimama kwa Lowassa kama mgombea Urais ni pigo kubwa kwa vyama vya siasa hasa Chadema, CUF na NCCR Mageuzi. Kutokana na rekodi ya Lowassa, ni mtu wa kufuatilia kila jambo analoamini katika dhamira yake kwamba linafaa kwa ajili ya maendeleo ya wananchi ni mwenye hulka ya kusaidia na kuchangia shughuli za kijamii bila kujali itikadi za kisiasa wala dini, tofauti na viongozi wengine wa kisiasa amekuwa mtu tegemeo katika shughuli za kijamii iwe za kanisani au msikitini.

Ukitaka kumjua Lowassa ni kiongozi wa namna gani, tembelea jimboni kwake Monduli ukaone namna alivyowezesha makundi ya vijana na wazee kiuchumi.

Sasa nimeamini Ritz na Pasco ni mtu mmoja!! Hongera sana Pasco aka Ritz!
 
Hivi kwa nini misaada na michango mingi anayotoa Lowasa inakuwa kwa pesa taslimu tofauti na ilivyozoeleka kwa watoa misaada wengi kutumia hundi.

Lowasa+mufti.JPG

Waziri Mkuu Mstaafu Edward Lowassa (kulia) akimkabidhi fedha za mchango Mwenyekiti wa Bodi ya Shule ya Sekondari ya Edward Lowassa Muft wa Tanzania Issa Shabaan bin Simba (katikati) kwa ajili kumarisha miundo mbinu ya shule hiyo. Kulia ni Mjumbe wa Bodi wa shule hiyo Alfred Tibaigana

mo%2Bakikabidhi%2Bcheque%2B1.jpg

Mwenyekiti wa kamati ya ushindi Taifa Stars Mh.(MB) wa Singida Mjini Mohammed Dewji (kushoto) akikabidhi hundi ya shilingi milioni 15 kwa Waziri wa Habari,Utamaduni na Michezo Dk.Emmanuel Nchimbi ikiwa ni ahadi aliyoitoa kwa timu ya Kilimanjaro Stars baada ya kutwaa ubingwa wa Kombe la Chalenji katika hafla iliyofanyika jijini Dar es Salaam.Katikati ni Kapteni wa timu ya Kili Stars Shadrack Nsajigwa akishuhudia makabidhiano hayo

Tumewahi mno kumpamba kwa kudhani tunamsaidia. Kasafishwa na nini mpaka uchafu alionao watanzania wasiuone? Kama ni hela zake kuleni mkijua kuwa WaTZ wa leo sio kama wale wa jana
 
Huyu mleta mada ni mjanja sana ,nadhani kwa kuleta hoja hii ndio anaanza kupima kukubalika kwa EL .Ila ushauri wangu naona kama kawahi sana kuanza kuwapima hao watarajiwa ,nibashiri baada ya EL atakuja na uzi mungine kama sio SIX basi utakuwa wa EMBE .Kwa taarifa yako yapo mengi utayapata kwenye utafiti wako uliouanza subiri cku zifike tutasikia mengi,tutaona mengi na watatenda mengi.
 
Tunakumbuka wakati Lowassa baada ya kuhamishwa kutoka Wizara ya Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu na kupelekwa Wizara ya Ardhi na Maliasili alikuta madudu mengi na kuanza kupambana nayo kwa ujasiri mkubwa wa ajabu.

Kulikuwa na wajanja wachache ndani ya halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam walitaka kuuza viwanja vya Mnazi Mmoja kwa mfanyabiashara mmoja maarufu, Lowassa alitoa tamko la serikali akiwa bungeni Dodoma akitaka mfanyabiashara huyo aondoke haraka eneo hilo kwa kuondoa uzio alikuwa ameujenga na ndipo wananchi wakavamia na kuchukuwa mapati yote.

Watanzania wanamuitaji "jembe" Lowassa.

Na baada ya kuwa-fool waTZ kuwa yeye ni mzalendo wa kweli, baada ya kunywea yeye ndo akakamata ardhi kwa kasi kuzidi sauti!!!

Lowasa nahisi anamiliki viwanja na mashamba at premium areas in TZ kuzidi mtu yeyote!!!

Na baada ya yeye kuambiwa aliiba toka Richmond na kugeukwa na mkulu, anataka nafasi alipize kisasi na si kuwahudumia waTZ.
 
Sio mie ni Watanzania ndio wanamkubali Lowassa rekodi yake ya utendaji ndio inambeba hata ukimchukia ni kazi bure mkuu katika Watanzania 10 wakihojiwa saba kati yao wanamkubali.

MTENDAJI WA WAPI?? KAMTENDEA/ KAMTENDA NANI?? NATUMAI MTENDWAJI MZURI, I OP NI MSWEET LAZIMA NI MWANAE WA KIKE ANAYETENDWA KILA SIKU NA SIOI SUMARI, WE NAMNA GANi???
 
Haya makubwa... Ritz umeamua kumeza matapishi yako? Umeamua kumtosa mzee wa mambo ya kigeni? Umesahau azimio lako la Bagamoyo? Natamani nishuhudie ujio wa mwaka 2016.
 
Tatizo la Chadema ambalo ndio linatawaangusha, Chadema baada ya kupata mafanikio katika uchaguzi mkuu uliopita wamejikuta wakihodhi wajibu wa jamii kisiasa kwa niaba ya vyama vingine wakihisi kwamba wao ni bora zaidi mbele ya jamii kuliko vyama vingine vyote nchini.
 
Na baada ya kuwa-fool waTZ kuwa yeye ni mzalendo wa kweli, baada ya kunywea yeye ndo akakamata ardhi kwa kasi kuzidi sauti!!!

Lowasa nahisi anamiliki viwanja na mashamba at premium areas in TZ kuzidi mtu yeyote!!!

Na baada ya yeye kuambiwa aliiba toka Richmond na kugeukwa na mkulu, anataka nafasi alipize kisasi na si kuwahudumia waTZ.

Mkuu usitoe shutuma kwa watu kwa kuhisi weka ushahidi zaidi ya hapo utakuwa unajenga kiwanda cha uongo.
 
Back
Top Bottom