Lowassa apanda chati kuelekea uchaguzi mkuu 2015

Naona mnapiga ngoma na kucheza wenyewe, mnakubali mgombea wa chama chenu kutoka kaskazini, kwa vyama vingine sio haruhusiwi mgombea wa uraisi kutoka kaskazini? shame on them, sasa mmehanza kucheza kiduku, alafu kumbukeni Lowasa ni mkristo so mahakama ya kazi haiwezi patikana ktk utawala wake

Mkuu Lowassa kiongozi pekee aliyeongoza kwa mafanikio makubwa Kituo cha Mikutano (AICC) katika kipindi ambacho Jumuiya ya Afrika Mashariki ilikuwa ikikabiliwa na changamoto nyingi za kisiasa, kiuchumi, na kijamii.
 
Katika uteuzi wa mgombea urais kutoka Chadema italeta mtafaruku mkubwa, Dr Slaa ambaye ameishapata uzoefu wa kugombea nafasi hiyo hatarudishwa tena na chama chake, huo ndio ukweli. Kwa maana nyingine Chadema watalazimika kumtafuta mgombea mwingine ambaye kwa wakati huo hatokuwa na uzoefu wa mikiki katika nafasi ya urais.

Mbali na kumtafuta mgombea mbadala wa Dr Slaa, viongozi wa kanda zingine hawataafiki mgombea atoke eneo moja tu kila chaguzi unapofika. Mparaganyiko huu utasababisha Chadema kuvutana na ikifika hatua hiyo.

Jamii ya Watanzania wataogopa kumchagua mgombea kutoka upinzani hususani katika nafasi ya urais.

Achana na Lowassa, weweeee !!
Andrew Chenge for President !!!
Hapo vipi ??
 
Nilikuwa namsikiliza JK Leo wakati anafungua kikao cha kamati kuu. Alisema kuwa wajumbe kuwa kamati ya maadili wamekaa kwa siku tatu badala ya siku moja katika kupitia majina ya wagombea kwa sababu waliamua kuachana na ripoti za secretariat za mikoa na wilaya na kuamua kupitia majina ya wagombea moja baada ya jingine.

Lengo ni kuhakikisha kuwa chama kinakuja na timu ya watu ambao hawatumikii maslahi Fulani Bali maslahi ya Chama. Anasema kuna uwezekano watu wengi waliodhaniwa kuwa watapenya wakaondolewa kwa sababu hawakuangalia umaarufu wa mtu AU sura., Lowassa, AU mtum mwingine anaweza kudhani sasa kuwa amepenyeza majina yake lakini Mwisho wa siku akaambulia patupu.

Tusubiri tuone mchujo utaishia vipi
 
Mkuu Lowassa kiongozi pekee aliyeongoza kwa mafanikio makubwa Kituo cha Mikutano (AICC) katika kipindi ambacho Jumuiya ya Afrika Mashariki ilikuwa ikikabiliwa na changamoto nyingi za kisiasa, kiuchumi, na kijamii.


Anakulipa kiasi gani kumsemea haya?
 
Kwanini wewe usiende kumfungulia kesi kama ushahidi unao. Kwanini usubiri mkuu wa nchi amkamate wakati hata wewe unayo haki ya kumshitaki?

Ushahidi gani na ww,au ww mgeni hapa tz?uliona wapi kesi ya nyani akapewa ngedere
 
......tofauti na viongozi wengine wa kisiasa amekuwa mtu tegemeo katika shughuli za kijamii iwe za kanisani au msikitini.
Ukitaka kumjua Lowassa ni kiongozi wa namna gani, tembelea jimboni kwake Monduli ukaone namna alivyowezesha makundi ya vijana na wazee kiuchumi.


Hapo kwenye red,
Lowassa ni mbinafsi sana.Alitoa maji Arumeru mpaka Monduli lakini kule yalikopita hawana maji.
Angekuwa kiongozi makini angeelekeza nguvu zake mikoa yote wakati akiwa waziri mkuu na sio
monduli tu.Hebu jiulize wakati akiwa waziri mkuu aliwahi kutoa michango kwenye kanisa au msikiti upi?
Na ni kwanini iwe sasa?Je akiwa raisi bado ataendelea na huo moyo?





 
Moja ya kashfa inayoenezwa na wabaya wake wa kisiasa ni ile iliyomkumba mwaka 2008 na kulazimika kujiuzulu kutoka na kile ambacho yeye mwenyewe alikiita ni kwa manufaa ya chama na serikali yake, kamati ya teule ya Bunge kumhusisha katika sakata la kampuni tata Richmond.

Hata hivyo hivi karibuni baadhi ya waheshimiwa wabunge waliwahi kukaririwa wakisema kuwa Lowassa hakuwa ametendewa haki katika sakata la Richmond.

Haiwezekani kila watati marais wa CCM watoke ukanda wa mashariki ya Tznzania (Mwinyi, Mkapa, Kikwete !!).
Safari hii lazima rias wa CCM atoke nyanda za juu kusini !! Lazima !!
Upo hapo ??
 
Kwa vyovyote vile dhambi ya ubinafsi, tamaa ya madaraka, uroho wa mali na kuwatesa watanzania kwa mgawo wa umeme uliotengenezwa kiujanja ujanja kwa faida yake binafsi na maswahiba wake wachache haitafutika kamwe ndani ya Lowasa hadi pale Mwenyezi Mungu atakavyo amua vinginevyo juu ya mustakabali wake kimaisha hapa duniani
 
Wewe unasema ni mwizi, leta ushahidi basi sio unaleta stori za vijiweni. Hivi wewe unamjua Lowassa vizuri au ndio unamuona kwenye gazeti, hata hao viongozi wenu kina Slaa wanamsujudia.

kumbe Lowasa siku hizi naye ni jembe?

Enewei ni bora mtuwekee na sisi tunaosali KKKT tupate Rais alafu aendelee kufadhili miradi ya kanisa letu kwani si mnajua tunataka kujenge chuo kikuu before 2020!

Teh teh teh teh teh...............!
 
Hivi hii thread Nape kaiona, nijuavyo mimi Nape na Lowasa ni kuku na mtama, akiiona hii thread hakika huyu ritz kapoteza mshahara wa leo
 
kumbe Lowasa siku hizi naye ni jembe?

Enewei ni bora mtuwekee na sisi tunaosali KKKT tupate Rais alafu aendelee kufadhili miradi ya kanisa letu kwani si mnajua tunataka kujenge chuo kikuu before 2020!

Teh teh teh teh teh...............!
Ndiyo ni jembe, si anachomekwa mpini we hujui
 
'Prince' wa Bagamoyo (a.k.a RitzOne) alishasema kuwa rais ajaye hatatoka kaskazini !! Sasa wewe unapingana naye ??

Tunaongelea kiongozi ambae ni tegemeo la Wanzania ambae ni mahiri hayo mambo ya Bagamoyo hayana nafasi katika Watanzania 10 saba kati yao wanamtaja Lowassa amrithi JK wanasema ni "jembe" linalopigania haki na maendeleo ya kila Mtanzania.
 
Ritz, nakushauri uwe unapima upepo kabla ya kuandika jamani, umeona hapo juu English Leaner alivyoshusha counter-measures. Wana JF (akiwemo Ritz, English Leaner na wengine), inabidi kwanza tukubali kuwa nchini Tanzania bado kuna tatizo kubwa la rushwa. Swali linalobaki wazi ni kwamba je, Mh. Lowassa (atapokuwa Rais wetu) anaweza kweli kuwatizama watanzania usoni na kuwahakikishia kuwa ana uwezo wa kupambana na rushwa kwa nguvu zake zote? Na sio kupambana na rushwa tu; je, ataweza kuwaambia Watanzania kwa macho makavu kuwa anakerwa kweli na tatizo hilo moyoni mwake? Itapendeza sana akituhakikishia hayo ili tuweze kumpa kura zetu, vinginevyo tutafakari ujumbe huu hapa chini:

" Watanzania wanataka mabadiliko ya kweli ya uongozi na utendaji wake, wasipoyaona CCM, watayatafuta nje ya chama hicho." - Mwalimu Nyerere
 
Mkuu Lowassa kiongozi pekee aliyeongoza kwa mafanikio makubwa Kituo cha Mikutano (AICC) katika kipindi ambacho Jumuiya ya Afrika Mashariki ilikuwa ikikabiliwa na changamoto nyingi za kisiasa, kiuchumi, na kijamii.

Acha uongo mimi niko AICC,Lowasa hakuwa mkurugenzi wakati wa jumuia ya Afrika mashariki iwe ile ya mwanzo
wala ya sasa.Aliyekuwa mkurugenzi wakati wa jumuiya ya sasa inaanzishwa ni marehemu Sammy Mdee na akifuatiwa na Maj.Herman Lupogo kisha Patrick Tsere na huyu wa sasa Elishilia Kaaya.Kadanganye wengine.
 
Tunaongelea kiongozi ambae ni tegemeo la Wanzania ambae ni mahiri hayo mambo ya Bagamoyo hayana nafasi katika Watanzania 10 saba kati yao wanamtaja Lowassa amrithi JK wanasema ni "jembe" linalopigania haki na maendeleo ya kila Mtanzania.

Hawa jamaa ni hatari kwa propaganda-By Mbowe
 
ccm hawaangalii uadilifu kwenye teuzi zao,hayo yalikufa na mwalimu Nyerere,sasa hivi ni money power!

Mleteni EL ili hoja za udini,ukabila na ukanda ziishe.

Siwachagulii magamba,lakini mleteni tu,tukutane 2015.
 
Pasco na Ritz,

Hivi munauhakika na afya ya Lowassa? Hata kama itafika 2015 akawa hai' je ni kweli anaweza himili mikiki mikiki ya kampeni
kutokana na afya yake?
 
Tunaongelea kiongozi ambae ni tegemeo la Wanzania ambae ni mahiri hayo mambo ya Bagamoyo hayana nafasi katika Watanzania 10 saba kati yao wanamtaja Lowassa amrithi JK wanasema ni "jembe" linalopigania haki na maendeleo ya kila Mtanzania.

Mtoto wako akishika nafasi ya tatu katika darasa zima lenye watoto watatu tu utasema amefaulu?
CCM mnamuona Lowassa anafaa kwa kuwa hamna mwingine zaidi ya huyu anayechekacheka tu.
 
Back
Top Bottom