Ungesema kati ya watanzania wana CCM 10 siyo kati ya Watanzania 10. Hiyo ratio ya kimagamba haiapply kwa watanzania wote wenye vyama tofautitofauti na wasio na vyama.
Eti katika kila watanzania kumi saba wanamuunga mkono Lowasa! Tatizo lenu Watu wa CCM mambo ya kwenye vikao vyenu mnachukulia ndio maamuzi ya Watanzania wote.
Jana tuu mlikuwa mnapita nchi nzima mnamwita gamba na kwamba lazima ajivue mwenyewe la sivyo mtamvua. Kikao cha NEC kamuumbua Mwenyekiti wenu kuwa mbona naye alihusika kwenye Richmond mkaona ohho! mambo yameharibika sasa tumwite JEMBE! loh mna mambo nyie!
Kweli ukizama baharini hata unyasi utaukimbilia ukidhani utakuokoa. RIP CCM
Ninaamini kama Lowassa angekuwa Waziri Mkuu bado hadi leo, ule mradi wa maji wa Ziwa Victoria usingekuwa umeishia Shinyanga pekee, bali ungekuwa umeishafika katika wilaya za Nzega, Igunga na mikoa ya Singida na Dodoma.
Lowassa ndio kiboko yenu nyie, ndio maana hofu limewajaa, mkwe wake kushindwa haihusiani kabisa, nikuulize,wewe dada yako akiposwa na wewe unavishwa pete?
Rais ajae hata kama ni baniani muhimu atatokea CCM.
Ninaamini kama Lowassa angekuwa Waziri Mkuu bado hadi leo, ule mradi wa maji wa Ziwa Victoria usingekuwa umeishia Shinyanga pekee, bali ungekuwa umeishafika katika wilaya za Nzega, Igunga na mikoa ya Singida na Dodoma.
Ritz,
Ukitaka kumjua Lowasa nenda Richmond
Wanabodi,
Wakati mchakato wa Uchaguzi ndani ya Chama cha Mapinduzi CCM unaendelea kuanzia ngazi ya shina hadi taifa. Mbunge wa Monduli Edward Lowassa anaonekana kupanda chati kwa kasi ya ajabu na kuonekana ana nafasi kubwa katika mbio za urais 2015.
Uchambuzi wa kisiasa unaonesha karibu kila kona ya nchi hii, katika watanzania 10 utakaowahoji kuhusu ni nani hasa anayefaa kumrithi Rais wa sasa Kikwete, saba kati yao wanamtaja Lowassa wakidai ni "Jembe" linalopigania haki na maendeleo ya kila Mtanzania.
Makundi makubwa yanayotajwa katika mnyukanakano huo ni pamoja na kundi la Lowassa, Samwel Sitta, na Bernad Membe. Kila mmoja anapambana kufa na kupona kuhakikisha kwamba wanaingiza watu wao muhimu katika vikao vya (NEC) na ndani ya Jumuiya za chama hicho, UVCCM, UWT, na Wazazi, katika makundi yote hayo Lowassa anaonekana kuwa ni mtu makini ana nafasi kubwa ya kupenya na kupererusha bendera ya chama hicho.
Kusimama kwa Lowassa kama mgombea Urais ni pigo kubwa kwa vyama vya siasa hasa Chadema, CUF na NCCR Mageuzi. Kutokana na rekodi ya Lowassa, ni mtu wa kufuatilia kila jambo analoamini katika dhamira yake kwamba linafaa kwa ajili ya maendeleo ya wananchi ni mwenye hulka ya kusaidia na kuchangia shughuli za kijamii bila kujali itikadi za kisiasa wala dini, tofauti na viongozi wengine wa kisiasa amekuwa mtu tegemeo katika shughuli za kijamii iwe za kanisani au msikitini.
Ukitaka kumjua Lowassa ni kiongozi wa namna gani, tembelea jimboni kwake Monduli ukaone namna alivyowezesha makundi ya vijana na wazee kiuchumi.
Kinachonifurahisha mimi licha ya kelele zote na propaganda za udini na ukabila wa CCM, lakini Rais ajaye ni lazima atoke kaskazini na ni lazima awe Mkristo, hapa mmejikaanga kwa mafuta yenu wenyewe.
Nadhani Pasco anafanya kazi nzuri sana kama ameweza kumsajili na Ritz kwenye kikosi kazi cha kuelekea 2015, narubungo uko wapi?
Keshaingizwa kwenye payroll,pesa haina dini wala kabila mkuu!Mkuu Ritz sikujua na wewe unasapoti kambi ya lowassa,hivi na madudu yote ya Richmond na mvua za kutengeneza unafikiri anaweza kupenya??