MzalendoHalisi
JF-Expert Member
- Jun 24, 2007
- 4,520
- 1,368
Ni ile ndege Inayopaa sasa imetua? Ina maana sasa tu/amefika?
Mkandara .Nina habari za huu mkakati mzito.Na kila nikiangalai naona kila aina ya dalili baada ya rais kuanza kujikanyaga kwenye majukwaa.Lowasa huenda akaenda Ubalozini ama akapata nafasi moja kubwa na ya ulaji lakini anapigania kurudi kwenye siasa ndani ya CCM.
Lowassa ana ndege siku hizi?
............................. Richmond ilikuwa kati ya makampuni yaliyo fail vibaya sana, lakini bado kutokana na shinikizo toka ofisi yake walipewa tender hiyo.
Uhalifu ilianza kabla hata contract haijawa signed na nadhani kama alikuwa hana mkono wake angeanza kuwaambia watu kushiriki kwake kabla/toka siku ya uchaguzi wa kampuni hiyo na sio baada uya kuwa signed................................Swali lilikuwa:- Kwa nini Richmond walipewa Tender hiyo?...Jibu la kamati lilikuwa ni nguvu toka ofisi ya Waziri mkuu. Hadi wakati huu hajajibu kabisa nafasi yake wakati tender ikitolewa..isipokuwa anazungumzia baada ya contract kuwa signed.
Unajua, ingekuwa mimi ni EL na nina nia ya kurudi kwa nguvu, ningekubali kuwajibika na kutotota hata sababu moja kujitetea kuwa sihusiki.
Ningesema " Kwa nafasi yangu kama Waziri Mkuu, nilipaswa kuwa makini katika kufuata taratibu za sheria na utendaji katika kutafuta mzabuni wa umeme huu wa muda. Nakiri kufanya uamuzi kwa pupa ya kutaka kutatua tatizo bila kuwa makini. Kwa hili na mzigo wote ambao nimeupa Taifa kutokana na maamuzi yangu, naomba radhi kwa Taifa kwa kushindwa kulitumikia ipaswavyo na kulilinda kutokana na uhujumu, kwa mujibu wa katiba na kiapo changu kama Mbunge, Waziri Mkuu na Mwana CCM. Naomba Watanzania wanipe imani yao kuwa nitaliwakilisha jimbo langu la Monduli kwa umakini kwa kujifunza kutokana na makosa niliyofanya ambayo yamepita. Kidumu Chama cha Mapinduzi"
Kwa mtaji huo, watu tutasahau kuwa yeye ni "fisadi" tutasema kafanya uungwana na ikifika 2015 na matunda ya yeye kuwa Mbunge mahiri bungeni, anaukwaa Ugombea uraisi kupitia CCM.
Lakini, huyu ni Lowassa hivyo......
Baada ya kuyaona haya yanayojiri hivi sasa na michezo ya maigizo tunayochezewa na kina Lowassa, nazidi kuiamini nadharia niliyokuwa nayo mwanzo kuwa labda Kamati ya Mwakyembe ilikuwa na melekezo maalumu kutoka mahali fulani kuwa Lowassa asihojiwe, ili kumpa mwanya wa kuendelea na mpango wao fulani.
Na hata ushabiki watu wengi walioonesha kwa PM "mpya" naanza kuhisi ni yaleyale mambo ya "kipya kinyemi ingawa ........".
Kazi ipo!
Tumwamini nani? Tume , Lowasa au watetezi wake? Tafuta riport ya Mwakyembe.