Lowassa ana dhambi nyingine zaidi ya Richmond?

kunani kati ya EL na CDM?
Hao CHADEMA unaowataka ni akina nani?....na huyo Lowassa ni nani CCM..Hivi kweli watu mbona mnataka sana kuzungumzia WATU..Hii akili finyu mlokuwa nayo nyie wenyewe mnataka hata vyama vianze kuzungumzia watu badala ya ideas za kuondokana na Umaskini, Ujinga na Maradhi?..
Chadema waseme mara ngapi ikiwa sikio la kufa halisikii dawa...Chadema wamezungumzia Ufisadi toka wakiwa chama na CUF, wamemzungumzia Lowassa toka sakata la Richmond kuanza halikutoka hewani. Leo mnawataka Chadema waseme nini zaidi ikiwa kama sii wao msingejua lolote kuhusu Richmond..
 
Lowassa ni Gamba originated from CCM, unataka CDM waingilie kufanyaje?
Au CCM wameshindwa kulivua ndio wanaomba msaada kwa CDM??
Mangapi wamesema mkaishia kuwabeza??
Mnalo hilo, shauri lenu na Gamba lenu!!!
 
Hivi zile siri za ufisadi ni kambi ya EL ama EL mwenyewe walikuwa wanwapa CDM?

Mhn! Lets wait and c...
 
Wakati uleee, iliwahi kusemwa humu ndani kwamba magwanda wanajipanga kimkakati kumsafisha Lowassa!!!! wakabisha, na wengine kama kawaida yao wakatoa maneno ya kejeli na matusi!!! CDM gani iliyoacha ku-discuss watu na kujikita zaidi na issues?! Humu JF, ni mara ngapi kumekuwa na post kuhusu Nape?! hivi kuna upuuzi kama ku-discuss personal life?! Mbona humu jamvini kuna post kibao tu kuhusu sijui mwichemba mwigulu sijui nani sijui (manake yule jamaa sina hakika kama nalifahamu jina lake sawasawa) kwamba katembea na mtu!!! Mara oh, JK kashindwa kuilea familia yake.....!!!! Linapokuja suala la Lowassa, ham-discuss watu bali issues, na kwa wengine......!!
 
mmesahau baada ya uchaguzi mkuu uliopita na chadema kudai hawayatambui matokeo ya urais katika watu wote chadema (mboe)alikubali kuzungimza na nani katika mazungmzo yaliyofanikishwa na zitto kabwe ambae ndie aliwakutanisha na baadae chadema "kulainika"?
 
Do not trust politicians 100%... I dont!

Ila one thing for sure. I HATE UFISADI NA ELEMENTS ZOTE ZINAZOHUSISHWA NAO.
 
Mhe. Lowassa ametangaza rasmi ushindi wa kisiasa katika kanisa la KKT Singida dhidi ya wabaya wake kisiasa na kusema wameshindwa.

Mi kwa kweli Lowassa bado najaribu kutafuta wa kumpambanisha naye uraisi 2015, zaidi ya Mhe Dr slaa nakosa!
 
Ngoja muda ufike
Inashangaza kuona kajipa ushindi mwenyewe hakutaka hata kusubiri wachunguzi wa mambo ya kisiasa wampe ushindi huo, dah!

Kweli kwenye kinyang'anyiro cha 2015 ndani ya magamba kutawaka moto wa kufa mtu.
 
Jamaa amedai Mungu kamficha dhidi ya maadui wake wote... Amechangia 10mil out of 138mil zilizopatikana...

Nahisi huyu jamaa anachanganyikiwa na kutapatapa, baya zaidi udhaifu ulionyeshwa na NEC na CC kushindwa kumchukulia hatua kwake yeye ni ushindi mkubwa sana.....na ndio maana ameanza kutoa kauli za kejeli kwa wanachama na wananchi kwa ujumla....
 
Kasema yamesemwa meeengi nchi nzima lakini hatimaye tumeshinda.Kasi yake kwa sasa ni kubwa na baada ya haya atasema mengi subirini!!
 
Yeye aendelee kutangaza ushindi na kweli ameshinda vita ndani ya chama kisicho na maadili,chama kinachofuga mafisadi,chama cha wafanya biashara sio cha wakulima na wafanya kazi.ni kweli kawashinda kina Nape na kina Sitta,ni kweli kashinda katika chama cha kinafiki,lakini ushidi huo hamhalalishi kuwa raisi ajae,hata achangie makanisa sana bado inaweza ikala kwake.wote mnaoshawishika nae kugombea na hata kuwa raisi wenu lazima ni wa uzao wa kifisadi,lazima ni wa uzao wa kinafiki na kwenu ninyi ni sehemu ya matatizo ya watanzania.Mshindwe na Mlegee kwa damu ya Yesu
 
Back
Top Bottom