Lowassa afuata upako kwa 'Nabii' wa Nigeria

Ngao One

Member
Jan 26, 2011
35
29
Waziri Mkuu wa zamani aliyejiuzulu mwaka 2008 kwa kashfa kubwa ya ufisadi ya Richmond, Edward Lowassa, ametuma ujumbe wa watu wawili waende Nijeria kukutana na Pastor TemitopeBalogun Joshua a.k.a. Prophet T.B. Joshua ambaye 'alimtabiria' Mbunge Beatrice Shellukindo kuwa Lowassa atakuwa Rais wa Tanzania baada ya uchaguzi wa mwaka 2015.

Wajumbe hao wa Lowassa ni mtoto wake Frederick Lowassa na mshauri wake mkuu wa masuala ya vyombo vya habari, Absalom Kibanda, ambaye ni mhariri wa gazeti la Tanzania Daima linalomilikiwa na Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe.

Frederick na Kibanda wako safarini Nijeria kwenda kuchukua 'upako' ili wamletee Lowassa asafishe nyota na kuepuka na dhoruba kubwa ya kisiasa katika kipindi hiki kigumu ambacho wajumbe wa NEC ya CCM wamedhamiria kuwafukuza mafisadi kwenye chama, akiwemo Lowassa, Andrew Chenge na Rostam Aziz.

Wajumbe hawa wa Lowassa wanatarajiwa kukutana na TB Joshua siku ya Jumapili Juni 12, 2011, ambayo mchungaji huyo atakuwa anasherehekea birthday yake na atawapa "dawa" wamletee Lowassa Tanzania ili asafishe nyota yake.

Ikumbukwe kuwa 'nabii' huyu wa Nijeria aliwahi kumwambia Mbunge wa CCM, Beatrice Shellukindo, kuwa anatabiri Lowassa atakuwa Rais ajaye wa Tanzania.

Beatrice, ambaye mume wake William Shellukindo, aling'olewa ubunge kwenye jimbo la Bumbuli na kina Lowassa-Rostam-Chenge na kisha wakamuweka January Makamba, sasa amehamia kwenye kambi ya kumpigia debe Lowassa awe Rais pamoja tuhuma kubwa za ufisadi dhidi yake, ikiwemo kujilimbikizia sana mali, ufisadi wa Richmond, kununua hekaru la sh bilioni 1 London na mengine mengi.

Siri ya Edward Lowassa nje | Gazeti la MwanaHalisi

Eti huyu fisadi kweli anadhani atakuwa Rais wa Tanzania?
 
hao wameenda kuchukua waganga wa kienyeji wanajifanya wanaenda kwa tb joshua kama geresha tu. wamefuata waganga wa kenyeji huko.

Hilo nalo neno, maana Lowassa anatafuta Urais by any means necessary
 
Wewe unapakatwa kweli na Lowassa. Kila mara ujitokeza kumtetea bwana wako kwa pesa chache unazopewa. Kazi unayo kijana


huyo tb joshua anahusiana vipi na mambo ya lowassa?kwani huyo joshu ni mganga wa kienyeji au ni nini?
 
Hivi kweli hata kama angefuata upako wapi Mungu si mnafiki hata kidogo kama wapiga ramuli.
hHi nchi ikiongozwa na mtu kama huyu tumekwisha na wala Watanzania hatujasahau bado tunauguza
vidonda.
 
hivi kweli hata kama angefuata upako wapi Mungu si mnafiki hata kidogo kama wapiga ramuli;
hii nchi ikiongozwa na mtu kama huyu tumekwisha na wala watanzania hatujasahau bado tunauguza
vidonda



nimecheka sana uliposema "ramuli"
 
Hivi kweli mimi na msimamo wangu itokee eti namkubali Lowassa kwa sababu tu kaenda kwa nabii au mpiga ramli! Atishikaye huyo mwendawazimu na pia lazima mfuasi wa hizo imani. Lowassa lazima ajibu hii hoja lasivo akubali kuwa bado anazipokea na kushabikia kashfa.
 
yaani fisadi katili namna hii ndo awe rais? basi nchi kwishney kabisa
 
Maswali na majibu ya humu yananifanya nicheke tu! bwahahahah hahaaaa haaaa!:behindsofa:
 
Sisi wateule tunatazama mchezo huu kwa umakini mkubwa! Lengo letu ni kupata kiongozi bora kwa wananchi wake, hayo makundi yatakufa kifo cha kadhia.
 
Back
Top Bottom