Lowassa afananisha dhana ya gamba na kitunguu

kimboka one

JF-Expert Member
Jan 23, 2010
734
85
kumbu mhe lowasa alisema mengi nec na kufananisha dhana ya ccm kujivua gamba na kitunguu eti kila hatua ina gamba ukiamua kuvua patabaki patupu kadhalika ccm wakiamua kuvuana gamba habaki mtu
 
Kweli swala zima la Gamba la UFISADI huko CCM haina tofauti na Kitunguu na MAGAMBA yake yalioumana tangu nje ha mle kati kati kabisa ambapo wengi wengi wangetarajia kusiwepo na biashara yoyote ya aina hiyo hata kidogo.

Na ni kwa sababu hii ndio maana narudia hapa kwamba Umma wa Tanzania kwa hasira kali juu ya ufisadi na hivi sasa utekwaji wa madaraka yetu kujitungia Katiba Tuitakayo, tunakusudia kufyeka idadi kubwa ya wabunge wa CCM tangu sasa hadi huko 2015 toka kwenye 250 hadi viti 78 tu!!!!!!!!!!!

Na hilo liko njiani, shauri yao wale wanaoamini tu mambo kwa kuona kwa macho bila kujichukulia tahadhari mapema!!!!!!!!
 
Kama ni kweli EL alisema hivyo, basi ujue CCM imeoza na ndo maana gamba "limekakamaa". Shime watanzania, kitunguu kilichooza hakifai hata kutolewa gamba lake moja, ni shurti kitupwe mbali.
 
EL ni balaaa mfano wa kitunguu umemaliza kila kitu,ukizingatia CCM wote wanamagamba je wote wataweza kujivua?
 
CCM hawawezi kujivua gamba wao wenyewe kwani CCM ndo gamba hivo Watanzania tuinyime kura ili tupate watu makini
 
kama kweli haya maneno uliyasema nakupenda mh. EL, ila sipendi uwe rais wangu, kwani hata ukiwa rais utapata wapi watu wa kuunda serikali yako kwani wote ni magamba.....teh teh teh.
 
Kama tunakubali kwamba Edo si msafi,basi lazima tukubali pia MTANDAO wote si msafi.Hatuwezi kumtoa kafara Edo peke yake.Wako wengi.Kama na wao hawawezi kujivua basi ni vema wamwache Edo aendelee na harakati zake then Watanzania wenyewe wataamua.
 
EL Kiboko akihojiwa na Tbc amesema eti vingozi wanakabiliwa na skendo wamuige yeye kwa kuwajibika kujiuzulu du! Sijui mafisadi wanatuonaje sisi wanananchi?
 
au wanafanana na kabeji

Si kutoa magamba tu kuwa ukiondoa la juu linaki la ndani nalo gamba shart liondoke
... Pia magamba haya yanaoza
 
ninachojua mimi ni kuwa ccm hawawezi kumuvua EL gamba wamwache aendelee na harakati zake za urais hili gamba lake hata kama ni gumu sisi wananchi ikifika kwenye kura tutaliondoa hata bila ya yeye kulia wala kulalamika
 
Back
Top Bottom