Lowassa aendelea kunyanyasa CCM

mgomba101

JF-Expert Member
Oct 21, 2011
1,817
706
KAMBI ya Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa imeendelea kuyanyanyasa makundi mengine ndani ya CCM, ambayo yamekuwa yakijipanga kwa ajili ya Uchaguzi Mkuu wa 2015.Kambi ya kiongozi huyo ni kama imehamia Dodoma ili kuhakikisha watu wake wanashinda katika chaguzi za viongozi wa juu wa jumuiya za CCM baada ya kufanikisha kile inachodai kuwa ushindi mkubwa katika ngazi za wilaya na mkoa kutokana na watu wake wengi kushinda.

Wapambe wa Lowassa wakiongozwa na Mbunge wa Kigoma Mjini, Peter Serukamba na Mjumbe wa Baraza Kuu la Umoja wa Vijana (UVCCM), Hussein Bashe wapo Dodoma kabla ya kuanza kwa Mkutano Mkuu wa uchaguzi wa Jumuiya ya Wanawake (UWT) na wataendelea kuwapo mpaka jumuiya zote zitakapokuwa zimefanya uchaguzi huo.

“Hapa kazi ni moja tu, hakuna kulala maana tukilala tutajikuta tumewekwa pabaya. Tumefanikiwa UWT na sasa tunaelekeza majeshi yetu UVCCM... lazima tuhakikishe tunakomesha uonevu wa kuitana magamba mwaka huu,” alisema mmoja wa wapambe wa Lowassa juzi usiku.

Matokeo ya uongozi wa juu wa UWT yameongeza matumaini kwa kambi hiyo ambayo imezoa zaidi ya asilimia 80 ya viongozi katika jumuiya hiyo yenye ushawishi mkubwa katika uamuzi mbalimbali wa chama hicho.

Mwenyekiti wa UWT Taifa, Sophia Simba ambaye alitetea vizuri nafasi yake na Makamu wake, Asha Bakari Makame wanatajwa kuwa katika kambi hiyo huku wajumbe saba kati ya tisa waliochaguliwa kuiwakilisha jumuiya hiyo katika Halmashauri Kuu ya Taifa (Nec) ya chama hicho, wakiwa waumini wa kambo hiyo.

Walioshinda nafasi za ujumbe wa NEC ambao wanatajwa kuwa wafuasi wa Lowassa ni pamoja na Mbunge wa Ukonga, Eugen Mwaiposa, Waziri wa zamani wa Maliasili na Utalii, Shamsa Mwangunga na Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Katiba, Sheria na Utawala, Pindi Chana.

Wengine ni wabunge wa Viti Maalumu, Diana Chilolo, Zainabu Kawawa, Mary Mwanjelwa na Subira Mgalu.
Wajumbe wawili ambao ni pamoja na Naibu Waziri wa Fedha, Janeth Mbene yeye anatajwa kuwa hana kundi lolote wakati Mbunge wa Viti Maalumu, Betty Machangu ambaye anatajwa kwamba alikuwa akimuunga mkono Mbunge wa Same Mashariki, Anna Kilango Malecela.

Kilango ambaye alikuwa akiungwa mkono na makundi ya watu waliojipambanua kuwa wapambanaji na ufisadi, aliangushwa vibaya na Simba kwa zaidi ya kura 400 katika kinyang’anyiro cha nafasi ya Mwenyekiti wa UWT.
Vigogo wengine wanaotajwa kuwa na kambi katika kinyang’anyiro hicho cha urais wa 2015 ni Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Benard Membe na Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta ambao katika uchaguzi wa jumuiya za CCM nguvu zao zinaonekana kuwa si kubwa kama ilivyotarajiwa.

JK awapasha viongozi UWT
Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete juzi usiku aliwatolea uvivu viongozi wa UWT, akiwataka kuchukua hatua za kumaliza nyufa zilizosababishwa na uchaguzi uliomalizika Jumamosi iliyopita.

Rais Kikwete alisema viongozi waliochaguliwa wakiongozwa na Simba ambaye pia Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto wachukue hatua kuondoa makundi ambayo yanatokana na uchaguzi.

“Hii jumuiya siyo yenu, ni ya wanachama kwa hiyo baada ya uchaguzi lazima muwe tayari kufanya kazi na kila mmoja, isije ikawa ni wale marafiki zako tu maana ikiwa hivyo utamteua hata kama uwezo hana,” alisema Kikwete alipokuwa akifunga mkutano huo wa uchaguzi mjini Dodoma.

Alikemea tabia ya chuki inayojengwa na uchaguzi akisema inatokana na viongozi walioko katika nafasi mbalimbali za uongozi kudhani kwamba wanazimiliki binafsi.

“Hupaswi kumchukia mtu eti kwa sababu amegombea nafasi fulani, hakuna nafasi ya mtu, nafasi zote ni za chama, kwa hiyo kama ulikuwa mwenyekiti, uongozi wako unakoma pale tunapotangaza upya uchaguzi,” alisema Rais Kikwete na kuongeza:

“Tukishatangaza kila mwanachama mwenye sifa anakuwa na haki ya kugombea nafasi hizo, sasa wewe usimchukie na kumuuliza eti kwa nini unagombea nafasi yangu, siyo nafasi yako, hii ni nafasi ya chama.”
Alikemea tabia ya baadhi ya viongozi au wagombea kuwajengea chuki wale ambao hawakuwaunga mkono, na kwamba anayefanya hivyo hapaswi kuwa kiongozi.

Alisema kiongozi wa aina hiyo daima ataongoza kwa makundi, akiwapenda wale waliomuunga mkono na kuwatenga wale ambao walikuwa na mtazamo tofauti jambo ambalo ni hatari kwa ustawi wa jumuiya na chama kwa jumla.

“Kila mwanachama ana uhuru wa kumuunga mkono mtu anayempenda, sasa wewe unapomkasirikia na kumjengea chuki unamaanisha nini? Demokrasia maana yake ni kila mmoja wetu kumchagua mtu anayeona anafaa,” alisema.

Alitoa mfano kwamba baada ya yeye kuteuliwa kuwa mgombea wa urais kupitia CCM mwaka 2005 na baada ya uchaguzi uliompa ushindi, aliwateua wale waliokuwa washindani wake katika Baraza la Mawaziri, akiwamo Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Kazi Maalumu), Profesa Mark Mwandosya.

“Mwandosya tuko naye hadi leo, hata wale waliokuwa wakinipinga na wengine walinifanyia mambo ya ajabu kwelikweli, lakini hayo yote inafika mahali unaweka kando maana huwezi kuongoza nchi kwa kuwateua marafiki zako tu,” alisema Kikwete.

Uchaguzi UVCCM leo
Rais Kikwete leo anatarajia kufungua Mkutano wa Nane wa UVCCM utakaofanyika katika Chuo cha Mipango, Dodoma huku vita kubwa ikitarajiwa katika uchaguzi kwa misingi ya kambi za urais kuelekea 2015.
Vita kubwa katika uchaguzi huo ni katika nafasi ya Makamu Mwenyekiti ambayo inawaniwa na Paul Makonda, Mboni Mhina na Ally Salum Hapi, wakati nafasi ya Mwenyekiti inawaniwa na Sadifa Juma Khamis, Rashid Simai Msaraka na Lulu Msham Abdallah.

Katika nafasi ya umakamu, Makonda anaungwa mkono na kambi ya Membe, wakati kambi ya Lowassa imeamua kuelekeza nguvu zake kwa mwanadada, Mboni. Kambi hiyo pia inamuunga mkono Sadifa anayegombea nafasi ya Uenyekiti.

Katibu Mkuu wa UVCCM, Martin Shigela alisema jumuiya yake inafuatilia mienendo ya wagombea wote na wapambe wao na kwamba watakaobainika kukiuka taratibu za uchaguzi watachukuliwa hatua.
Akizungumzia suala la rushwa ambalo linaonekana kuiandama CCM pamoja na jumuiya zake, Shigela alisema: “Katika hilo tumejipanga vizuri kukabiliana nalo.”

“Mfano mzuri ni kule Zanzibar, katika Mkoa wa Mjini Magharibi tumetengua nafasi za wajumbe wawili wa Baraza, hii ni kuonyesha kuwa hatutanii lazima watu wawe waadilifu,” alisema.

Kwa mujibu wa Kanuni ya Umoja wa Vijana, mkutano huo utakuwa chini ya Uenyekiti wa Benno Malisa kwani kanuni inasema kama mwenyekiti si mgombea, basi ndiye atakayeongoza mkutano huo.
Mkutano huo pamoja na kuchagua viongozi wa UVCCM, pia utapitisha katiba mpya ya jumuiya hiyo.
 
Money! Power! Respect! Fedha fedheha mengine tunamezea! uongozi unanunuliwa kwa ajiri ya urais 2015!! eeeeh mwenyezi mungu tuepushe na balaa hili.
 
Uchaguzi UVCCM leo
Rais Kikwete leo anatarajia kufungua Mkutano wa Nane wa UVCCM utakaofanyika katika Chuo cha Mipango, Dodoma huku vita kubwa ikitarajiwa katika uchaguzi kwa misingi ya kambi za urais kuelekea 2015.
Vita kubwa katika uchaguzi huo ni katika nafasi ya Makamu Mwenyekiti ambayo inawaniwa na Paul Makonda, Mboni Mhina na Ally Salum Hapi, wakati nafasi ya Mwenyekiti inawaniwa na Sadifa Juma Khamis, Rashid Simai Msaraka na Lulu Msham Abdallah.
MMH KAAZI KWELI KWELI MAGAMBA LEO...... UVCCM NDIO JESHI LAO....KAMBI ZINASHINDANA KUTEKA MAWAZO YA VIJANA 2015. NIMETOKEA KUFAHAMU HISTORIA MBONI SINA PINGAMIZI YA KUWA MEMBER WA KAMBI YA EL ILA NAOMBA KWA ANAEMFAHAMU PAUL MAKONDA ANIJUZE..
 
Lowasa, lowasa, lowasa!!!!!!!!! Eee MUNGU tuepushie hili balaa!

Ikulu ni mahali patakatifu... kwa mtu mwaminifu, ikulu ni mzigo... mkimuona mtu anagombania kuingia ikulu muulizeni anakwenda kufanya biashara gani?-Late Mwl. Nyerere
 
Mwacheni Lowassa aingie Ikulu tupate mvua za mfululizo kwakua sisi wakulima tumeshakata tamaa na kilimo!
 
Ni ukweli kwamba wagombea wa kambi za Membe na Sitta hawakufanikiwa kupata nafasi katika uchaguzi huo ambao hao waliochaguliwa hawakuvutiwa na sera za kambi ya Lowassa bali ni mvuto wa mabilioni yaliyotolewa kiuendawazimu na huku wenyewe wakijisifu kwamba kambi yao inapeta. No body in their right thinking minds can ever dish out stupid monies to buy leadership. At least not Membe and Sitta.
 
Kazi lazima ionekane 2015,naona EL anajitahidi kutumia kila aina ya sabuni kujitakasa. Nadhani CDM wana kila namna ya kujiandaa kushika hatamu za uongozi wa nchi hii maana njia inaonekana nyeupeeeeeeeeeeeee!
 
Lowasa, lowasa, lowasa!!!!!!!!! Eee MUNGU tuepushie hili balaa!

Ikulu ni mahali patakatifu... kwa mtu mwaminifu, ikulu ni mzigo... mkimuona mtu anagombania kuingia ikulu muulizeni anakwenda kufanya biashara gani?-Late Mwl. Nyerere


Na NDIO HIVYO ANAKUWA RAIS... namkubali...

Anayo kura yangu... Ana UAMUZI, mchapakazi, hana longolongo....
I will vote for him....
 
Mboni na lowassa ni majirani mtaa moja masaki nyumba ya tatu toka lowassa. Tatizo huyu binti ni kilazza mno. Kasha disco vyuo zaidi ya vinne.
 
Na NDIO HIVYO ANAKUWA RAIS... namkubali...

Anayo kura yangu... Ana UAMUZI, mchapakazi, hana longolongo....
I will vote for him....

Unaweza ushangae hili li tanzania gani lina mawazo ya ajabu hivi kumbe ni toto la EL au fisadi mwenzake... haya bwana ngoja tuone kama kweli waTZ ni wapumbavu tutathibitisha 2015
 
asa kama lowassa anainyanyasa ccm, itakuwaje akishika nchi, si ndo tutanyanyasika kabisa..uuuuuuuuuuuuuuwik!!!
 
Unaweza ushangae hili li tanzania gani lina mawazo ya ajabu hivi kumbe ni toto la EL au fisadi mwenzake... haya bwana ngoja tuone kama kweli waTZ ni wapumbavu tutathibitisha 2015

TAKE THIS AS UR HOMEWORK...

1: Muulize Sitta kwann alikimbia mbio Dodoma na kusahau uspika

2: Muulize Sumaye alikuwa analia lia wiki mbili mfululizo bila kusema nani kampiga.... Anazunguka zunguka NA WANAHABARI.... ni nini ...??

3: juzi Anna Kilango ALILIA MACHOZI WAZI WAZI KAMA KAFIWA...... muulize ni nini...???


Ndio ukipata majibu U WILL KNOW WHAT I AM TALKING....

LAIGWANAN is NOT AN ORDINARY FIGHTER...
 
Huyo ndo EL, nguvu ya pesa inachangia haya na product ni makundi na minyukano ndani ya ccm,hadi 2015 tutayaona mengi.
 

Lowasa ni janga na angamizo kwa taifa letu, mtu mwema hawezi kutumia mabilioni yote hayo kuutaka urais kwa nia njema, watanzania tuungane kumkataa kuyu fisadi.
 
TAKE THIS AS UR HOMEWORK...

1: Muulize Sitta kwann alikimbia mbio Dodoma na kusahau uspika

2: Muulize Sumaye alikuwa analia lia wiki mbili mfululizo bila kusema nani kampiga.... Anazunguka zunguka NA WANAHABARI.... ni nini ...??

3: juzi Anna Kilango ALILIA MACHOZI WAZI WAZI KAMA KAFIWA...... muulize ni nini...???


Ndio ukipata majibu U WILL KNOW WHAT I AM TALKING....

LAIGWANAN is NOT AN ORDINARY FIGHTER...

Nimekupata mzee, ila tumwambie EL pesa zake atanunua SEX but not LOVE!
 
Mie nafurahi wanaposhindwa hao unaowaita wenye maamuzi makubwa wa ccm. Kushinda kwao ni kete ya turufu kwa upinzani kushinda 2015. Kwa sababu uozo wao tunaujua, ni kazi ndogo kuwaambia wapiga kura hatari ya uozo huo kuendelea mbele. Kina Kilango wangeshinda ingekuwa kazi ya ziada kuhitajika 2015 sababu tayari wanajulikana kuwa wapambanaji wazuri ambao tungependa idadi yao iongezeke tupate Tanzania mpya hata kama kupitia magamba. Sasa CCM wanajiua wenyewe, wanajikaanga kwa mafuta yao wenyewe kwenye nundu za ufisadi wao. Wewe subiri utaona.
 
Back
Top Bottom