Loliondo Saga: Wakili akamatwa kwa tuhuma za ujasusi, Mawakili Arusha waandamana kupinga

Chachu Ombara

JF-Expert Member
Dec 11, 2012
5,897
10,358
Mawakili wasomi mkoa wa Arusha wameandamana leo kupinga wakili Shilinde kushikiliwa na Jeshi la polisi huko Loliondo na kupinga taaluma ya uwakili kudhalilishwa.

Polisi mkoani Arusha wanamshikilia wakili huyo wa kituo cha sheria na haki za binadamu (LHRC) kwa kosa la ujasusi. Wakili huyo ameambiwa kufanya ujasusi wakati si kweli, yeye alikuwa akifanya kazi yake ya uwakili.
Mawakili arusha.jpg


Alichokisema Wakili Msomi Shilinde kuhusu kukamatwa na kuhojiwa

Dear colleague, clarification kwa wale ambao hajawaelewa post yangu. Kwa wale ambao haifahamu Loliondo ni takribani km 400 kutoka Arusha.

Huku kunawawezaji kwenye sekta ya utalii na kunakampuni mbili maarufu zinazolindwa na serikali kwa nguvu kubwa.

OBC ni kampuni ya mfaulme Mwarabu na TCL ni kampuni ya tajiri wa kimarekani anaitwa Rick.Kampuni hizi zina migogoro ya Ardhi ya muda mrefu na wanavijiji.

Zipo Kesi za madai ya ardhi High court Arusha zinaendelea na Mimi ni mmoja wa prosecuting adv. kwenye kesi hizo.Serikali na makampuni hayo wanaona Kesi hizo ni kikwazo kwa maslahi yao hivyo Mawakili wamekuwa associated na migogoro hiyo.

Katika hali ya kuwatisha viongozi wa vijiji na wanakijiji kuendelea kudai haki zao mahakamani serikali imekuja na task force inawakamata na kuwatia ndani viongozi wa vijiji na wanakijiji na viongozi wa NGOs walio mbele kuwasaidi vijiji kupata haki zao.

Kamatakamta ya polisi ikawaweka ndani wanakijiji,na viongozi wao pamoja na director wa NGo moja hapa loliondo kwa takribani siku 8 sasa bila kufikishwa mahakamani.

As a human rights lawyer I volunteers to come here in Loliondo kuja kutia Msukumo watuhumiwa hao wafikishwe mahakamani ili pia tuwawakilishe mahakamani.

Harakati hizo ndizo zilizopelekea wakili kutuhumiwa pamoja na wateja wake na kisha kuzuiliwa ili ahojiwe ktk tuhuma zinazodaiwa kuwa za ujasusi.

Polisi walinidhamini niondoke kituoni Jana usiku kwa sharti la kuriport leo kutoa maelezo.

Leo nimekwenda kituoni time ikawa extended hadi Jumatatu kwa dhamana ya OCD.Kwa hiyo nipo Loliondo bado.

Kauli za wakili mtetezi kuwa sehemu ya kosa ya mteja wake na Jaji Au hakimu kumuachia mharifu akijua kuwa mharifu na yeye ni mharifu alisema mkuu wa kikosi kazi hicho Afande Commissiner Chilya wakati wa kunihoji na timu yake.

Swala hili ni tofauti kabisa nala wakili Mwale.Mimi nimeona mkakati huu wa kipolisi ni tishio kwa kazi ya uwakili na ndio maana nimeraise alarm hii.

Lakini pia suala zima pia la mawakili kuonekana wanaganga njaa.Hata hivyo ninawashukru sana mawakili wote kuonyesha solidality kupinga udhalilishaji wa taaluma yetu unaofanywa na polisi .

I will keep you up dated.
 
Hii imetokea katika mkoa Wa arusha baada ya wakili mmoja kuunganishwa na Wateja wake na kuswekwa ndani kwamba nae ni mhalifu kwasababu anatetea wahalifu huko longodo mkoani arusha
1469530383461.jpg
1469530416679.jpg
 
Back
Top Bottom