Logo
JF-Expert Member
- Jan 26, 2011
- 588
- 48
- Thread starter
- #41
Popote duniani hakuna dawa ya kuzuia au kutibu kifo
Wagonjwa wanakufa hata kwenye hospitali kubwa kabisa zenye wataalam wa hali ya juu kabisa
Dawa ya babu ni dawa na imani (neno la Mungu)
Hata wakati wa Yesu watu walikuwa wanakufa; Lazaro anatajwa kwa vile alifufuliwa.
Yesu alianza peke yake lakini alipotaka watu wengi wahubiriwe, aliwatuma wanafunzi wake; Babu ameanza peke yake, kadri watu wanavyoongezeka, tuombe Mungu amfunulie ili awatumie hao wanaomsaidia kugawa dawa (nao wawe na uwezo wa kutoa dawa kama babu)
Malaria ina dawa tena ambayo kisayansi inaaminika kutibu, lakini wapo watu wanaokunywa dawa hiyo na wanakufa hadi inafikia mahali pa kutafuta kinga (net).
Kwa kuwa watu wengi bado wanapona kwa kunywa kikombe cha babu, serikali inatakiwa kuimarisha huduma za dharura ili wale walio mahututi waendelee na dawa zao za kawaida kabla ya kufika kwa babu. Wakati niko kwenye msitari wa kufika kwa babu niliona gari la ambulance la Halmashauri likizunguka kwenye foleni likiwa na mganga tayari kuhudumia wale walio mahututi - wa pumu, kifafa nk. Hii ni step nzuri. Ile kodi ya Tshs 2000 kwa kila gari, halmashauri iitumie kuimarisha hali ya usafi pale. Chimba vyoo vya muda along the road up to say 10 km. Chimba mashimo ya kutupa takataka along the road, na watu waelekezwe kutupa takataka humo. Siku hizi watu ni wastaarabu, ukiwaelekeza usafi wanafuata. Kwa kuwa kikombe cha babu kinakubalika na wengi, tumuwezesha kuchemsha dawa kwa wingi zaidi na kuimarisha namna ya kusafisha vikombe. Kwa mfano akiwezeshwa kuchemsha kwa kutumia gesi, hii inaweza kuchemsha dawa nyingi na hata maji ya kuoshea vikombe yakawa ya moto pia; Hii pia itazuia uharibifu wa mazingira utakaosababishwa na ukataji kiti kwa ajili ya kuni nk.
Pamoja na tahadhari na wasiwasi juu ya kikombe cha babu, as long as wengi wanakikubali, ebu tuboreshe mazingira yake; tukubali kwamba kwa hivi sasa ni vigumu kuwazuia watu wasiende!
Si rahisi sana kama sio mtu wa rohoni kuyatambua mambo kama haya! Babu haui, dawa yake haiui, serikali haiui, wagonjwa hawajiui ila Hii ni mbinu kubwa ya shetani kuua watu!