Location ya satellite ya FTA channels za GTV receiver

Sinkala

JF-Expert Member
Dec 22, 2008
1,773
683
Jamani mtakumbuka mwaka 2009 jamaa wa GTV walipokumbwa na mtikisiko wa uchumi wa dunia na wakasepa kiaina. Hata hivyo watu tuliendelea kupata Free To Air channels katika receiver yao, nakumbuka zilikuwa channels za nchi za Afrika kama Angola, Togo, Senegal na nyingine nimesahau. Binafsi nilihama makazi yangu ya awali nilikofungiwa dish, na huko nilikohamia imebidi nitundike upya hilo dish. tatizo linalonikumba ni kutofahamu location ilipo satellite ya FTA channels za GTV (kama bado zinaexist) lengo ni kuweza kulielekeza dish langu dogo la GTV. Nimejitahidi kuelekeza West kama ilivyokuwa awali, lakini bado Quality ni 0% na hivyo siwezi kuscan channels kwa mafanikio. Kwa kuwa ni muda kidogo tangu nihame, huenda kuna mabadiliko fulani hapo. Sasa mnaotumia hii service naombeni mnielekeze walau nipate ladha tofauti. Sitaki kulipia channels kwa kuwa sishindi sana nyumbani, halafu mambo ya kulipia yamekuwa mengi sana, vyakula, usafiri, umeme, maji, gesi, mshahara wa house girl, michango ya masherehe, yaani hakuna balance bongo hii! Nimeimiss Setanta, ingawa wanapenda kuonyesha recorded!

Naombeni mnipe location ya sat
 
Kwa kweli hapo kwenye wekundu umesema ukweli hawa jamaa wanakula pesa za bure,badala ya kutoza kiwango flat kwa mwezi mimi naona wangetoza kama LUKU,yaani kama umeme au simu watoze kulingana na matumizi ,mbali na kutokushinda nyumbani ,pia kuna wakati hupati picha au kuna kuwa mikwaruzo mitupu,pia kuna mambo ya MEGAWATI,hawa jamaa waanze kutoza kama LUKU bana,ngoja nipeleke mapendekezo TCRA(ingawa wako bize na kuwapa wajumbe wa bodi simu za bei mbaya na posho ya kila mwezi)hili nalo ni jambo la muhimu ,watumiaji tunaibiwa sana na hawa wa VING'AMUZI VYAO
 
Asante kwa mawazo, lakini zaidi nataka nijue jina, azimuth na elevation ya hiyo satellite
 
Back
Top Bottom