Local Media na tukio la Gongo la Mboto

Chief Isike

JF-Expert Member
Jan 17, 2010
445
462
Sijaelewa kwa nini inakuwa hivi, tangu jana, baada ya milipuko ya Gongolamboto, hatujapata a good report from the scene, hususan katika televisheni zetu. Jan ITV walikuwa wanaendelea tu na kipindi maalum cha mkutano wa viongozi wa dini, TBC wakiendelea na kipindi maalum cha Maulidi, Star TV nayo mambo sijui ya tamthilia.

Sasa hivi pia, no one is there, ukiachailia mbali ripoti za asubuhi katika taarifa za habari na kidogo ile ya TBC walioweza kufika kule, na taarifa ya Pinda bungeni, nothing is going on...wanaweka katuni, picha za Ki-Nigeria, wengine habari za huko nje, basi.

So wanasubiri kuitwa na akina Shimbo na Mwinyi waambiwe so so so and so, kisha watuletee. PLZ TV guys do ur homework. Picture whether in print or televisheni, tell more, especially kwenye event kama hizi. PLz. Msisubiri press conferences na press releases.
 
Inawezekana kuna uwasi ndani ya kambi hiyo na habari imekuwa nyeti ,ndio ukaona kimya kikubwa ,mkuu wa polisi nilimsikia kwenye nyuzi akisema wananchi wasifikirie jambo jingine zaidi ya kuwa ni ajali imetokea ,hapo ndipo nilipotilia mashaka kuwa si ajali ,something is going on.
 
pia kwanini pasiwekwe sheria kwa wamiliki wa vyombo vya habari (hususan TV na radio) kuwa mstari wa mbele yanapotokea majanga km haya...inashangaza kukuta nyimbo na vipindi vya katuni wakati kuna mwenzetu wanapoteza maisha...kwanini wamiliki wasifikiri bila uhai hivyo vipindi vyao havina watazamaji/wasikilizaji?
 
Sijaelewa kwa nini inakuwa hivi, tangu jana, baada ya milipuko ya Gongolamboto, hatujapata a good report from the scene, hususan katika televisheni zetu. Jan ITV walikuwa wanaendelea tu na kipindi maalum cha mkutano wa viongozi wa dini, TBC wakiendelea na kipindi maalum cha Maulidi, Star TV nayo mambo sijui ya tamthilia.

Sasa hivi pia, no one is there, ukiachailia mbali ripoti za asubuhi katika taarifa za habari na kidogo ile ya TBC walioweza kufika kule, na taarifa ya Pinda bungeni, nothing is going on...wanaweka katuni, picha za Ki-Nigeria, wengine habari za huko nje, basi.

So wanasubiri kuitwa na akina Shimbo na Mwinyi waambiwe so so so and so, kisha watuletee. PLZ TV guys do ur homework. Picture whether in print or televisheni, tell more, especially kwenye event kama hizi. PLz. Msisubiri press conferences na press releases.

ingekuwa Aljazeera, CNN au BBC World ungepewa full coverage live bila chenga. usiku kucha.

huku kwetu kuripoti habari mpaka upate kibali cha polisi. vinginevyo utakuta wameweka pingu kwenye OB-van na kusingiziwa ulitishia kuuwa mtu ukitaka rushwa ya milioni 10.
 
wanaangalia maslahi yao kwanza na yale ya taifa baadaye............tbc kazi yao ni kuisaidia ccm tu basi lakini sio watz
 
Hawataki watu wajue kilichojiri! Mi napigania uchapaji kazi ktk eneo husika watu wa tv mmeshindwa nini kukesha eneo la tukio? Au siyo kazi yenu au mna habari kubwa zaidi ya iliyotokea? Au hampewi overtime? Au tajiri zenu hawataki mambo haya yaanikwe sana ili kila mtu ajue kilichotokea. Toeni ujinga wenu wa kuweka tamthilia wakati kuna disaster
 
Sijaelewa kwa nini inakuwa hivi, tangu jana, baada ya milipuko ya Gongolamboto, hatujapata a good report from the scene, hususan katika televisheni zetu. Jan ITV walikuwa wanaendelea tu na kipindi maalum cha mkutano wa viongozi wa dini, TBC wakiendelea na kipindi maalum cha Maulidi, Star TV nayo mambo sijui ya tamthilia.

Sasa hivi pia, no one is there, ukiachailia mbali ripoti za asubuhi katika taarifa za habari na kidogo ile ya TBC walioweza kufika kule, na taarifa ya Pinda bungeni, nothing is going on...wanaweka katuni, picha za Ki-Nigeria, wengine habari za huko nje, basi.

So wanasubiri kuitwa na akina Shimbo na Mwinyi waambiwe so so so and so, kisha watuletee. PLZ TV guys do ur homework. Picture whether in print or televisheni, tell more, especially kwenye event kama hizi. PLz. Msisubiri press conferences na press releases.

wanataka hadi waitwe sehemu kama maelezo ili walipwe posho
 
ingekuwa Aljazeera, CNN au BBC World ungepewa full coverage live bila chenga. usiku kucha.

huku kwetu kuripoti habari mpaka upate kibali cha polisi. vinginevyo utakuta wameweka pingu kwenye OB-van na kusingiziwa ulitishia kuuwa mtu ukitaka rushwa ya milioni 10.

...na matangazo mengine yote yangesitishwa, kungekuwa na breaking news ya kulipuka kwa mabomu. Si unakumbuka septemba eleven??!!, usiku kucha habari ilikuwa ni hiyo tu. Lakini hapa kwetu kila chombo cha habari kivyake.
 
Binafsi nimeshangazwa sana how scanty the report from our major electronic media houses was/have been....Ukisikiliza redio one sasa utasikia wanazungumzia umuhimu wa kuvaa soksi safi na umbea mwingine, clouds nako mipasho na vituko tu, EA radio muziki kwa kwenda mbele nk.watu wengi wangependa kujua je is it safe sasa kwenda maeneo ya huko pugu, Jet, Airport nk kwasababu wengine huko ndiko wanapopata mkate wa kila siku. Traffic ikoje kwa wanaotumia barabara hiyo....hali za mahospitalini ,kuwa na frequent taarifa juu ya watu/watoto waliopotea. Pia kuna amabao tungesafiri leo, je mamlaka ya viwanja vy ndege inasemaje nk....
 
Kwa kweli inashangaza zaidi ya mno!!!! Redio zote hakuna hata moja inayotoa taarifa za maafa hayo! Nimejitahidi kutafuta redio hadi redio bila mafanikio!!! Wote wanapiga miziki ya mapenzi tu!!!! Yaaani..... I fail to comprehend about this media of ours!!!!! Outrageous!!!
 
Watakuja na kisingizio kimoja kuwa Masuala ya jeshi hawapaswi kuingia ndani, lakini hata kutoa picha za nyumba zilivyobomoka na watu wanavyohangaika kusaka watu wao na je ya kule uwanja wa uhuru ambako wananchi wamekusanyika, pia ni masuala ya jeshi?
 
Ndiyo maana hii taaluma ya uana-habari inapoteza mvuto kila kukicha...wadau wamelala na hawaonekani kufanya jitihada kuhamasisha vijana wanaochipukia kupenda kazi hii...na wanapoibuka wachache wanaothubutu kujaribu wanaonekana WACHOCHEZI...heko wanahabari,hebu tumieni kalamu na kamera zenu kutufahamisha tulipo,tulipotoka na tunakoelekea
 
Inasikitisha sana kuona vyombo vyetu vya habari vinakosa vipaumbele
ambavyo ni muhimu kwa masilahi ya uma
 
Labda wameogopa kufika eneo la tukio.
Si ajabu hata baadhi ya wanajeshi kusikia wamekimbia. Lol!
 
Waandishi wa habari wa Bongo waoga ndugu yangu....mabomu yalipuke umwone paparazi wa kibongo kwenye tukio?..... Hayo waachie akina Anderson Coopers wa CNN na wenzake wanaoona vifaru mitaani Egypt wanatoka Atlanta na kutia timu eneo la tukio...

Bwana asante lakini kwa hili sijui kama watona thread yako labda wataamka
 
Tatizo ni kuwa vyombo vya habari Tz sio professional kwa utoaji habari. Vyote vipo kwa ajili ya kujenga maslahi binafsi ya watu au vikundi fulani. Wameajiri watangazaji ovyo, watawala ovyo, na wameweka mitambo ovyo pia...
 
Kwa kweli inashangaza zaidi ya mno!!!! Redio zote hakuna hata moja inayotoa taarifa za maafa hayo! Nimejitahidi kutafuta redio hadi redio bila mafanikio!!! Wote wanapiga miziki ya mapenzi tu!!!! Yaaani..... I fail to comprehend about this media of ours!!!!! Outrageous!!!

ilikuwa taabu kweli kweli unatafuta taarifa nini kinatokea unakutana na miziki ya mapenzi, as if they are broadcasting from outside dar
 
Back
Top Bottom