Loan defaulters mlioajiriwa mmekwisha!!

Hahaha! Pole sana! Mie ndo hata sijajiangalia wananisimanga vipi!
Ila hawa jamaa nahisi hizi hela zitakuwa kama za EPA zilizorudishwa! Wezi mno! Afadhali za radar wazungu wamekomaa nazo! Kha!
kamanda

Jamaa wamenitenda kweli, i went there in person nikaambiwa sina deni, juzi nimekuta MTM ndani ya wadaiwa sugu, nimewaomba tena niwalipaje?? na nitahakikishaje kwamba jina limeondolewa? wameniambia wataniarifu sasa nimekua mpole
 
Mie ndo hata siwaelewi,maana kuna watu tumeanza nao darasa moja na tumemaliza nao lakini tuna maden tofauti, mie nalipa hela nyingi ya mwenzangu!mi naona ili kuondoa utata wangeandika majina na amount unayodaiwa kwenye magazeti au online!from there utaweza kujua kama unachokatwa ni sawa au sio! na sio kutuwekea li figure tu kwenye salary slip kumbe wanachakachua
 
Hiyo itakuwa mara ya pili kupelekewa majina hayo, lakini hawafuatilii malipo yao. Waache uzembe.
 
Inasikitisha sana Serikali imeshindwa kuajili wasomi ili waendeshe HESLB matokeo yake imeajili kwa kujuana kiasi kwamba hakuna utendaji wa uhakika. Mi ni mhasibu na ndiye ninaandaa mishahara ya kazini kwang, huwa ninaandaa cheki kwenda HESLB kwa ajili ya mikopo ya wafanyakazi waliofaidika na hiyo mikopo. La ajabu ni pale nilipo kuta majina yetu yako kwenye Loan defaulters!!!!!!
Hili ni tatizo la serikali yetu. Hivi wahasibu wa bodi ya mikopo ni wahasibu kweli? cheki zinazoandikwa kupokelewa huko, hawajui kuzifanyia kazi.?

Kweli nchi yetu imeajili ndugu badala ya competent staff, ndo maana na wizara ya afya yanawasibu hayo.
 
Swali la ufahamu, mwenye majibu anielimishe:
Kwanini wanaotakiwa kulipa ni kuanzia 1994? Kwanini kila mtu aliyefaidika na hizo pesa ni kuanzia 1994 na si kila beneficiaries? Au aliye andaa hilo dai yeye ni kabla ya hapo? Huo ni ubinafsi wa viongozi wa nchi yetu walio fanikiwa kupata nafasi na hivo kuona asiyeajiliwa na serikali kuwa hana stahili ya nchi
 
Nitalipa iwapo wote waliosomeshwa na serikali toka uhuru watalipa akiwemo JK!
 
kamanda

Jamaa wamenitenda kweli, i went there in person nikaambiwa sina deni, juzi nimekuta MTM ndani ya wadaiwa sugu, nimewaomba tena niwalipaje?? na nitahakikishaje kwamba jina limeondolewa? wameniambia wataniarifu sasa nimekua mpole

Mkuu, naomba msaada wa link ya majina ya wadaiwa..
 
Wale loan defaulters wa HESLB ambao walikula kiapo kwamba hawatalipa kwa kuwa pesa walizopewa ni ruzuku sasa wajiandae kulipa!HESLB imeteua mawakala ambao wanapita katika kila taasisi kuwapa maelekezo wakuu wa Idara namna ya Kuandaa taarifa za wahitimu wa vyuo vikuu waliosoma kwa mikopo ili waanze kulipa mara moja!Rafiki yangu mmoja ambaye alikuwa mkaidi kuhusu jambo hili,nilipomfahamisha alinywea!LIPENI PESA ZA WALIPA KODI BANA!MLIKUWA MNATANUA NA BOOK ALLOWANCE PALE MABIBO HOSTEL NA PALE MEEDA BAR!

Ulivyoongelea kishabiki hapo...wewe lazima utakuwa baadhi ya waliokosa mkopo HESLB wakati huo ukawa private, hela ya kwenda Meeda mpaka ukaombe kwa baba, pole!

Inayolipwa ni tuition fees tu, na sio allowances za vitabu, kujikimu, na/au mafunzo ya vitendo! Na tunalipa hayo madeni, acha wivu! Msiolipa jamani muanze kulipa wadogo zetu nao wasome!
 
watu walioko kwenye ajira rasmi ndo watapatikana kwa urahisi sana, tatizo sio kulipa tatizo ni matumizi ya hizi pesa hii board ina urasimu mkubwa sana nikikumbuka walivyokuwa wanachakachua ile means testing hata sina hamu ya kulipa deni nahisi hata haya madeni kuna uwezekano yakachakachuliwa tu, uzalendo unahitajika sana kwenye hili.
 
Ulivyoongelea kishabiki hapo...wewe lazima utakuwa baadhi ya waliokosa mkopo HESLB wakati huo ukawa private, hela ya kwenda Meeda mpaka ukaombe kwa baba, pole!

Inayolipwa ni tuition fees tu, na sio allowances za vitabu, kujikimu, na/au mafunzo ya vitendo! Na tunalipa hayo madeni, acha wivu! Msiolipa jamani muanze kulipa wadogo zetu nao wasome!

Are you sure kuwa tunadaiwa tuition fee peke yake? kama ni hivo basi loan board wamechemsha na zoezi litakuwa gumu mara dufu coz kuna watu walilipiwa na celtel au wahisani lakini majina yao yametoka as if na wao ni wadaiwa...hapa sielewi.
 
Nilikuwa nafuatilia muda mrefu kuhusu huu mgomo wa madaktari ila nimegundua kwamba selikali yetu haina kabisa mapenzi na sisi .

 
Kalipe Deni nimeona wewe ni mmoja kati ya Watu ambao hawajaanza hata kupeleka Malipo yao

...Haa ha ha...

....Mie nilishamalizana nao longtime, tuliopata fursa ile tunao wajibu wa kimsingi wa kulipa hii loan ili kuwawezesha vijana wengine nao waweze kupata fursa kama hizo, kufanya vinginevyo ni usaliti kwako binafsi na kwa taifa lako....
 
Tatizo bodi wenyewe hawana kumbukumbu, mimi nilikuwa private nimelikuta jina eti nadaiwa, wanaumwa kweli
 
Back
Top Bottom