Loan Board [Heslb] waja kivingine.......Wataalam tusaidiena sababu bado hawasomeki.

Sep 2, 2012
48
7
Ndug wanajukwaa poleni sana kwa shughuli na kukosa mikopo kwa baadhi ya wanachuo watarajiwa.Leo majira ya saa 12.06 jioni website ya bodi ya mikopo imeanza kufunguka na wameomba radhi kwa matatizo yaliyojitokeza na kuonesha njia mpya ya kuona Mkopo uliopata na mchanganuo wake.Maajabu na kitu cha kushangaza ni kwamba wanakuelekeza jinsi ya kuona huo mkopo,
1.Click view results,kisha itakuletea yafuatayo
a].Ingiza key word [Ni moja kati ya uafuatayo;Index number,First name,middle name or surname]
b].Ingiza security code kama walivyokuwekea kwa mbele.

Kitu cha ajabu ni kwamba hawajaka maelekezo ni index number ipi inayotakiwa kutumika kati ya ile ya kidato cha nne na cha sita?Majina yanafanana je,watayatofautisha namna gani?Lakini cha ajabu zaidi ukifuata maelezo hayo bado account zetu za loan board hazifunguki.

Wataalam tunaomba mtusaidie kwa hili kama sisi ndo tuna uelewa mdogo wa au ni tatizo linalotusumbua wote?
 
Jaribu kutumia moja kati ya majina yako pia inafunguka. Mi nimejaribu kwa majina kadhaa na imekubali vyema.
 
weka jina lako moja either la baba or la kwako itakuja list ya majina ya wale wote wenye jina kama hilo walio pata mkopo na maelezo ya ziada.
inaonesha haukujaribu umekimbilia jf kuuliza kwanza, jaribu na utajionea mwenyewe
 
Jaribu kutumia moja kati ya majina yako pia inafunguka. Mi nimejaribu kwa majina kadhaa na imekubali vyema.

Thenks kaka nimefanikiwa kuyafungua lkn nimekosa kumbe ilikuwa inakataa 7bu jina langu halimo.Nitahitaji msaada na ushauri zaid wa kimawazo toka kwa wanajukwaa wenzangu katika kipindi hiki kigumu cha huzuni na simanzi kwani nahisi km nimetupwa katika giza nene kiasi kwamba sioni popota.Ndoto zangu zimezimika ghafla.

ALL THE BEST.
 
inakubali mbona kama index ni ya olevel na jina ni vyema ukatumia ubini ili uwah kuona kwasababu majina ya mwanzo meng yebo yebo
 
daa pole sana aisee try 2find financial assistance kwa watu wenye uwezo kama wazaz au walez hawana uwezo maana no way out ishatokea
 
Nitajaribu kukata rufaa,ikishindikana nitajaribu next year,cz wazazi wenye uwezo wa kugharamia elimu ya juu ni wachache sana na waziazi wangu hawamo kati ya hao.
 
Back
Top Bottom