Lo kumbe ubaguzi wa ccm hata kwa wapinzani wanaojiunga nayo!

Ngekewa

JF-Expert Member
Jul 8, 2008
7,705
1,288
Mbunge amcharukia Mwenyekiti UV-CCM




Na Thobias Mwanakatwe



3rd January 2010


email.png

B-pepe



printer.png

Chapa



comment_bubble.png

Maoni








Mpesya(1).jpg

Mbunge wa Mbeya Mjini, Benson Mpesya



Mbunge wa Mbeya Mjini, Benson Mpesya, amemshukia Mwenyekiti wa Jumuiya ya Vijana wa Chama cha Mapinduzi mkoa wa Mbeya (UV-CCM), Regnald Msomba kwa kumtaka aache kuropoka kwa kuwashambulia wabunge wa mkoa huu kwamba hawatembelei wananchi majimboni mwao bila hata ya kufanya utafiti wa kubaini ukweli wa jambo analolizungumzia.
Akizungumza katika mkutano wa Baraza Kuu la Vijana wa Mbeya Mjini jana, alisema inashangaza kuona Mwenyekiti huyo wa Umoja wa Vijana Mkoa wa Mbeya amekuwa na tabia ya kujisemea tu mambo ovyo kuwashambulia wabunge wakati mambo yanakuwa hayajaamuliwa na Baraza la utekelezaji la Jumuiya hiyo ambalo ndilo lenye maamuzi ya kusema.
Mpesya alisema inashangaza Mwenyekiti huyo wa UVCCM mkoa wa Mbeya kupenda kuwashambulia wabunge na kwamba haieleweki kama ni nani aliyempa mamlaka ya kikatiba ya kuwasimamia wabunge wakati wanaopaswa kuwasimamia wabunge ni wananchi wenyewe waliowachagua.
"Mbunge kama amefanya jambo fulani kikawaida anaitwa kwenye kikao na huo ndio utaratibu wa CCM, lakini wengine wakisema kitu tunawasamehe tu kwani tunaangalia historia yao wametokea wapi maana unakuta kwamba alikuwa chama cha upinzani akahamia CCM yanakuwa ni matatizo, CCM tuna utaratibu wetu, siyo kwamba wabunge hatuwezi kusema unasamehe tu sisi sote ni watoto wa mjini,"alisema Mpesya.
Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa CCM mkoa wa Mbeya, Regnald Msomba Novemba 11 akiwa mgeni rasmi katika maandamano yaliyofanywa na wanafunzi wa Vyuo Vikuu mkoani hapa aliwashambulia wabunge wa mkoa wa Mbeya kwamba hawaonekani majimboni mwao hali ambayo imepelekea kuwepo na kero mbalimbali zinazolalamikiwa na wananchi.
Msomba katika mkutano huo wa wanafunzi wa Vyuo Vikuu ambao alikuwa mgeni rasmi, bila kuwataja majina alisema baadhi ya wabunge wamekuwa wakikomalia suala la EPA na ufisadi ambapo hawatumii muda wao kwenda majimboni kuzungumza na wapiga kura wao kero zinazowakabili.
Mwezi Oktoba mwaka huu UVCCM mkoa wa Mbeya uliingia kwenye malumbano mengine makali na wabunge kufuatia kumtumia Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM, Kingunge Ngombare Mwiru kuwasimika makamanda ambao baadhi yao walishaonyesha nia ya kugombea ubunge uchaguzi mkuu wa mwakani kwenye majimbo ya mkoani hapa.
Makamanda waliosimikwa na kuzua malalamiko kadhaa kutoka kwa wabunge walikuwa ni Laulenti Mwakajumulo ambaye ni Kamanda wa Vijana Mkoa anayetaka kugombea ubunge jimbo la Rungwe Magharibi kupambana na Profesa Mark Mwandosya.
Wengine ni Phelemon Msomba Kamanda wa Vijana Wilaya ya Chunya ambaye ni kaka yake na Mwenyekiti wa UVVCCM mkoa wa Mbeya, Regnard Msomba aliyeonyesha nia ya kugombea ubunge jimbo la Songwe kupambana na mbunge wa sasa Guido Sigonda.
Nafasi ya Kamanda wa vijana Wilaya ya Mbarali alipewa Burton Kihaka anayetaka kupambana na Esteria Kilasi mbunge wa sasa wa jimbo hilo wakati Kamanda wa Vijana wa Kyela alikuwa ni Elias Mwakalinga.




CHANZO: NIPASHE JUMAPILI

Jamani huko CCM kuna watu wenye trade mark? Na kwa nini hufanya sherehe mnapowapata hao Wapinzani?
 
Pichani kwa mbaali wanaonekana wachovu mno wananchi na nadhani kwa hofu mbunge kasimama mbali sana na wao maana anaweza kunaswa kibao
 
Mti hutambuliwa kwa matunda yake.
CCM inatafunwa na ugonjwa wa ubaguzi kutoka kila kona. Usitegemee muujiza wa CCM kuacha ubaguzi.
 
Back
Top Bottom