LLB. vs B.A Law enforcement

EJay

JF-Expert Member
May 21, 2012
693
172
Wakuu,Salaam

Kuna hizi kozi mbili za sheria ya Bachelor of Laws LLB na Bachelor of Arts in Law enforcement,ni kozi ipi soko la ajira ni kubwa kwa sasa.

Ushauri wenu ni muhimu wadau na Mungu awabariki.
 
LL.B. ni shahada ya kwanza ya sheria.Hii humfanya mtu kuwa Mwanasheria na kazi zinazoendana na hizo kama Uwakili nk.B.A. Law Enforcement ni kozi mpya pale UDSM ambayo kimsingi haimfany mtu kuwa Mwanasheria.Hii inafundisha Sanaa na sheria kidogo kama wale wa Stashahada(Diploma) na Astashahada(Cheti) cha Sheria.Hii ilianzishwa ikiwalenga hasa wasimamizi wa sheria kama wanajeshi,maafisa usalama,TAKUKURU,magereza na polisi.BA Law Enforcement haimfanyi mtahiniwa kuwa na sifa za kuwa Wakili. Kwa maelezo hayo,ni vyema ukasoma LL.B...
 
vuta nkuvute kajibu vizuri sana...law enforcement hasa imeanzishwa kuwasaidia law enforcers kama polisi,kama uko interested kuwa mwanasheria soma LLB
 
kwa sasa tcu imeharibu kinoma mtu anatwo ya 10 anasoma LL.B UDSM SHIIT!
 
LL.B. ni shahada ya kwanza ya sheria.Hii humfanya mtu kuwa Mwanasheria na kazi zinazoendana na hizo kama Uwakili nk.B.A. Law Enforcement ni kozi mpya pale UDSM ambayo kimsingi haimfany mtu kuwa Mwanasheria.Hii inafundisha Sanaa na sheria kidogo kama wale wa Stashahada(Diploma) na Astashahada(Cheti) cha Sheria.Hii ilianzishwa ikiwalenga hasa wasimamizi wa sheria kama wanajeshi,maafisa usalama,TAKUKURU,magereza na polisi.BA Law Enforcement haimfanyi mtahiniwa kuwa na sifa za kuwa Wakili. Kwa maelezo hayo,ni vyema ukasoma LL.B...

Mkuu kuhusu ajira vp?
 
Asante kwa ufafanuzi, kwa kuongezea, hiyo Law Enforcement ni tailor made course kwa specific people wakati LL.B ni general. Ukisoma LL.B you can be anybody, lakini ukisoma hiyo enforcement, lazima ufanyie kazi areas za enforcement, polisi, magereza na uhamiaji!.

LL.B ni miaka 4 plus mwaka mmoja wa Law school, B.A Law enforcement ni miaka 3 na biashara imeishia hapo!.

Kwa maoni yangu, hakuna nafasi kujoin LL.B kama huna DIV 1 kali, wakat hiyo enforcement, principle 3 za A level zinatosha!.
 
Wakuu,Salaam

Kuna hizi kozi mbili za sheria ya Bachelor of Laws LLB na Bachelor of Arts in Law enforcement,ni kozi ipi soko la ajira ni kubwa kwa sasa.

Ushauri wenu ni muhimu wadau na Mungu awabariki.

Law enforcers ni Polisi, Magereza, Uhamiaji et al. Lawyers should go for LL.B first. Becoming a law enforcer is easier than becoming a lawyer. Choose the profession you want first. Ukitaka ajira za haraka somea ualimu na udaktari.
 
thumb up kwenye ualimu mkuu ila udaktari parefu hapo ni sawa na graduate wa sociology aliyepata kazi mwaka wa pili baada ya kukaa nyumbani!
 
Law Enforcement kwa kifupi BALE ni kozi iliyoanzishwa pale UDSM kwa wazo la IGP ,staafu MH. Mwema. Mwanzoni ilikuwa ikichukua Police tu lakini kwa sasa imeamuliwa kuwa hata ambao sio polisi wanaweza kuisoma. Ajira za BLE zipo nyingi tuu kwani unakuta darasani mpo 50 na kati ya watu hao 30 ni polisi 20 ni Freshers . Ajira zake ni kama TPDF, BoT, Migration, TAKUKURU, Magereza, Police, TRA, Usalama wa Taifa,Utumishi, Ikulu n.k
BALE ni nzuri kwani ina upana mkubwa wa ajira pia unaweza kujiajiri.. Unaweza ukafungua Foremsics Company pia Law Enforcement unaweza kuwa wakili kama ifuatavyo. LLB wanasoma miaka minne na wanapaswa kwenda Law School lakini Bale unaweza kusoma kwa miaka mitatu ukiona unataka kuwa advocate nenda kasomo Post Graduate ya Law ukimaliza unaruhusiwa kwenda Law School ukasomee uanasheria direct. Hii haina tofauti na mtu aloenda LLB miaka minne na akaenda Law School mwaka mmoja.. Tena unakuta unamzidi mtu wa LLB vitu vingi.
Cha msingi ni kwamba amini kuwa unachokisoma ni bora kuliko anachofanya mtu mwingine. Kwani hata hao wanaosoma LLB wangapi wapo mtaani wanahangaika na mabahasha? Wangapi wana mihuri ya uwakili na hawana wateja?
Ukisoma BALE unaweza fungua private Forensics Station kama LGC ya Uingereza, FAL ya Ufaransa n.k. Kitu ambacho hakipo Tanzania. Tatizo tumekariri ndo maana unaenda mji mdogo kama Bukoba unakuta Law Firms kama 10. Kuwa mbunifu. BALE inalipa na BALE naiona bora.
 
asante sana mkuu kwa kuwapa mawazo mapya vijana wapo watu hapa wamekuwa wakibeza lakini leo nadhani watafunguka macho kidogo
 
Back
Top Bottom