Lizzy

Lukansola

JF-Expert Member
Sep 5, 2010
5,435
1,597
Sasa nakuja kivingine, nakuja kwa staili ya mistali, I dedicate this to Lizzy nilimuahidi mistali. (Hivi ni mistali au mistari?)

ni wapi utapokaa, uhuru ukiwa nao
vitufe ukivibofya, ukiona na video
maovu yajulikana, hakuna upendeleo
Lizzy naye akasema jukwaa ndilo kioo

mchango tunautaka, wa hayo yako mawazo
hasira acha kwa sasa, ni kitu cha kitulizo
ukweli utakuuma, maria rosa liwazo
Lizzy naye akasema, jukwaa ndilo kioo

airtel twawapenda, kulonga mwatuwezesha
loliondo mmefika, kwa babu mwawakilisha
mbele mmeonekana, kurembesha ukurasa
Lizzy naye akasema, jukwaa ndilo kioo.

waziri twakushukuru, bajaj kutuonesha
tandale kawe na bunju, kote huko kufikishwa
moto haufui dafu, bajaj kusuluhisha
Lizzy naye akasema jukwaa ndilo kioo.

machoni pangu haupo, moyoni nimekutia
ndiwe wewe invizibo, napenda ukitokea
kwanini wabaki huko, msaada ukitoa
Lizzy naye akasema jukwaa ndilo kioo

Akili kichwani vipi, Lizzy kumchonganisha
Ugomvi yeye hawezi, ni mzuri kwenye hoja
kufwata yako hiari, ushauri ushapewa
Lizzy naye akasema jukwaa ndilo kioo

kupendana mpendane, lakini kwa taratibu
sio ki baba na mama, huko sasa kwa wakubwa
walimu msiwaguse, msiharibu majibu
Lizzy naye akasema, jukwaa ndilo kioo

Jinsia yako nyingine , Lizzy hapendi kwa hivyo
jaribu tena badae, kwa sasa sio richabo
manyanja katamkiwa, alipotuka ndoano
Lizzy naye akasema jukwaa ndilo kioo

kwa mengi nisiwachoshe, kurasa kuwajazia
Lakini niwakumbushe, jukwaa kulichangia
jamii ijiendeshe, hata kwa vocha ungisha
Lizzy naye akasema jukwaa ndilo kioo
 
wewe mshairi halafu unauliza ni msatali au mstari? Ni "mstari", ukiwa mmoja na "mistari" ikiwa zaidi ya mmoja.
 
Aiseee!Asante kwa shairi Luka.,nimeamka na tabasamu hapo hapo!Mistari imetulia sema mimi leo mashairi yangu yako mapumzikoni!
 
Aiseee!Asante kwa shairi Luka.,nimeamka na tabasamu hapo hapo!Mistari imetulia sema mimi leo mashairi yangu yako mapumzikoni!

You are welcome Lizzy, msalimie manyanza, uko naye hapo?

Ngoja nikatafute sehemu ya kuibia....nakuja!

Wala huna haja ya kuiba we unafunguka tu mradi maneno kwenye verse yaishie na herufi za kufanana pia yelete maana, its's just about playing with words mimi mwenyewe, hilo ndo shairi la kwanza toka nizaliwe.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom