Live Updates: Misa ya Maziko ya Kardinali Rugambwa kanisa la Kashozi - Bukoba

Misa ya Maziko ya Kardinali Rugambwa inaendelea katika kanisa la Kashozi nje ya mji wa Bukoba, baada ya misa yatafuata maandamano kuelekea kanisa Kuu la Bukoba yatakapofanyika maziko rasmi.

Misa imeongozwa na Askofu Thadeus Ruwaich kutoka jimbo la Mwanza na imeisha muda mfupi uliopita, Watu ni wengi, mvua ya wastani inapiga.

attachment.php

Kanisa atakamozikwa mjini Bukoba.

Nshomila bana, kwenye wasifa wa Marehemu Mwadhamu Kardinali Rugambwa wameanza na 'alizaliwa kwenye aristocratic family!

Mbele ya kanisa kama sikosei hilo ni bango la Vodacom. Linafanya nini hapo mbele ya jengo zuri namna hiyo? mbona wanaharibu mandhari bana?? waweke bango sehemu nyingine lakini siyo mbele ya jengo la kanisa. Inashusha hadhi.
 
Nshomila bana, kwenye wasifa wa Marehemu Mwadhamu Kardinali Rugambwa wameanza na 'alizaliwa kwenye aristocratic family!

Mbele ya kanisa kama sikosei hilo ni bango la Vodacom. Linafanya nini hapo mbele ya jengo zuri namna hiyo? mbona wanaharibu mandhari bana?? waweke bango sehemu nyingine lakini siyo mbele ya jengo la kanisa. Inashusha hadhi.
sasa kama ndio ukweli wenyewe waandike vp? maana wakati huo kanisa ilibidi lifanye urafiki na watu hao ili waweze kufikia waumini. Ilikuwa vigumu kuwapuuza Machifu halafu utegemee kupata waumini kirahisi!
 
RIp. Rugambwa.Nakumbuka nilimuona pale kwake oysterbay, st peters ,1984, tulikuwa wadogo.Akatuoffer dreva wake atupeleke mpaka nyumbani.Ni mtakatifu.
Onyamege.
 
Kama kuna anayefahamu, naomba afafanue swala lifuatalo: Iweje Waziri Mkuu aende kuiwakilisha serikali kwenye mazishi na asihudhurie maziko yenyewe? Maana maziko ni pale mwili unawekwa mavumbini ulikotoka.

Let us thank the Lord for the gift of the life of this holy man.
 
Asante mkuu KAUDO kwa kutujuza. Nasi walio mbali tuneshiriki kwa kuona, asante sana na Mungu akubariki.

Apumzike kwa amani, Mhadhama Laurian Kardinali Rugambwa.
 
RIP Kardinali, bado sijaelewa ni kwa nini hukupenda kuzikwa katika kanisa lililokustahili; Kanisa kuu la Mt. Joseph - Dar es salaam.

Utuombee kwa Mungu kwani ile amani kidogo uliyotuacha nayo sasa inapotea!
uLAURENT! au ukabila!
 
Askofu Kilaini yupo hajapewa nafasi ya kungea,pamoja na Maaskofu wengine kutoka ndani na nje ya nchi,Maandamano ndo yanaanza

Hiyo ni kauli ya kumfanyia diagnosis presidaa kam ilivyo ya "kuwa hana shida ila ni watendaji wake tuu".Na si unajua kuwa ndio anaanguaka na CCM ,bila kuwa na rais wa hivyo tungemwaga damu nyingi zaidi kuiondoa CCM.
 
Back
Top Bottom