LIVE UPADTES: M4C DAR - Lengo ni Kukusanya Bilioni 5 CHANGIA MABADILIKO

Aiseeee baba yangu huku nyumbani rombo kuna baridi sana ila cha kushangaza watu ni wengi sana hapa kwa mwenyekiti wa kijiji watu ni wengi sana wanashangilia mboe akisema pipo wananchi wanaitikai pawa
 
Chadema wanatakiwa watoe ahadi kuwa mambo yote ambayo wamewahi kuyasema,watayashughulikia endapo watapewa ridhaa na wananchi ya kuongoza Taifa.Ni wakati wa kutoa ahadi kama hizo...Tunataka kuona accountability,tunataka kujuwa kama chadema watawachukulia hatua wote waliolifisadi taifa na wasiotaka mabadiliko na kutumia mbinu chafu kama torture na mauwaji,chadema ni lazima wawapromise wananchi justice,na si kuishia tu kusema tu "hatuwaogopi"
 
Hakika Mbowe Maneno aliyoyatoa leo ni mwiba kwa yule anaendelea kuziba masikio.
 
Sasa Kwa walio nje ya nchi na wanataka kuchangia watafanyaje.
View attachment 61499

Kampeni ya Kuchangia harakati za Mabadiliko M4C Nchini zitaonyeshwa Live kupitia Kituo cha Luninga cha Star TV kuanzia saa 2 na Nusu Usiku na lengo ni kukusanya shilingi Bilioni Tano.


Mratibu wa Fund rising hiyo Mh. Kamanda Godbless Lema amesema fedha hizo zitatumika kununulia magari yatakayowezesha kufika kila maeneo nchini na kuhamasisha mabadiliko pamoja na kugharamia kampeni zote za ukombozi kamili wa Mtanzania.


Kila mpenda mabadiliko anatakiwa kuweka kiasi cha fedha katika simu yake kuanzia shilingi 1000 - 1000000 na kuendelea na zitatangazwa namba za MPESA ambazo zitatumika kufanikisha azma hiyo kwa malengo ya Muda Mrefu.

JINSI YA KUCHANGIA: Updated

Kwa watumiaji wa VODACOM: Watumiaji wa Mitandao mingine vuteni subira kidogo kama nilivyobainisha hapo chini:


Bonyeza *150# baada ya hapo bonyeza 4, kisha weka nambari ya kampuni ni 111333. Halafu unaweka namba ya kumbukumbu ya malipo ambayo ni namba yako mtuma fedha, halafu unaweka kiasi unachochangia , kisha nambari yako ya siri na unathibitisha mualamala kwa kubonyeza 1.

MITANDAO MINGINE
Tuma neno CHADEMA kwenda namba 15710 kila ujumbe ni shilingi 500 tuma ujumbe nyingi uwezavyo kwa kadiri ya kiasi cha fedha ulichokusidia kuchangia M4C


CHANGIA MOVEMENT FOR CHANGE

KUTOKA ENEO LA TUKIO:


Timu ya Star TV ishafika na vifaa vyao, wanafunga Dish la kurusha matangazo na kutandaza Nyaya hapa SERENA HOTEL


Keep hooked for more UPDATES

UPDATES:
Namba za Kuchangia zitatangazwa moja kwa moja wakati wa kurushwa Matangazo hayo. Watanzania wapenda mabadiliko mtaarifiwa namna ya kufanya ili kuhakikisha mnaeza kuchangia kwa kiasi chochote kuanzia shilingi mia tano hadi ukomo wa nafasi yako katika kuunga mkono kampeni hizi.

Namba za kutuma Pesa Kupitia Simu ya Kiganjani
Taratibu zinawekwa sawa kuhakikisha hakuna hujuma yoyote na zitatolewa kunako majira ya saa moja jioni ya leo. Vuteni subira na msikose kutazama Star TV na pia thread hii kwa UPDATES

Tahadhari:
VODACOM msifanye yale yaliyojitokeza Arusha kwa kuzifanya namba hizi kuwa busy na huduma ya MPESA kushindikana kwa wakati huo.

ADIOS
 
Jamani watanzania wenzetu hata kama mmebahatika kuwa wabunge lakini chungeni mnayoyasema mnatudharirisha
 
Kawaida unapotaja wahusika kadhaa wewe unayejitaja unakuwa mwisho lakini Mhe. Mbowe Kajitaja Kabila lake la kwanza!!!!????
 
inabidi waandike neno CHADEMA kwa capital letters tupu kwani kwa small leta haitafika hyo sms,let them inform those at startv
 
jamani umeme ni kwetu mbagala tu au hata kwenu!! duh, kweli nchi hii safari ni ndefu
 
Back
Top Bottom