LIVE ON STAR TV: Mpango wa Utoaji wa anuani za makazi na simbo za Posta Nchini

Yahya Mohamed

JF-Expert Member
Oct 28, 2010
270
317
Habari za Jumanne ya leo wanaJF

Katika kipindi cha Tuongee Asubuhi Jumanne ya leo tutaangazia mabadiliko ya sera ya Posta Nchini ya Mwaka 2003 ambayo yalitoa uwepo wa uhitaji wa madailiko ya mfumo wa anuani za makazi na simbo za Posta nchini.

Mfumo huu unaoelezwa kuendana na hitajio la e-commerce, pia kukuza uchumi na kurahisisha mawasiliano kati ya serikali na wananchi wake unakabiliwa na changamoto nyingi.

Karibuni kufuatilia mjadala huo na kuuliza maswali yenu kwa viongozi wa TCRA watakaokuwepo STUDIO kufafanua na kujibu maswali yenu
 
Aksante sana ndugu Mtangazaji, mfumo huu ni muafaka na sahihi kwa mawasiliano katika karne ya hii. lakini kuna vikwazo vingi sana katika kutekeleza hili mojawapo ni mipango mobovu ya mipango miji. sehemu nyingi katika miji mikubwa hakuna mitaa wakati mwingine ni vigumu hata kutambua mipaka ya nyumba. Pia barabara za mitaa hazipitiki kabisa ni vigumu kutekeleza mpango huu. inatakiwa kuweka miundo mbinu kwanza.
 
Hii ni Aibu!! Ukiona mambo muhimu ya utendaji yanaanza Kujadiliwa kisiasa Ujue Kuna walakini Mkubwa Katika Taifa!!

Walitakiwa waanze Then on the way ndio wawe na Kipindi cha awareness campaign!! Hii inatia shaka sana siasa kila Mahali!! Dar es Salaam imekuwa Makazi Holela Kutokana na Uzembe Huu huu!! Sasa Hata Hizo anuwani zikiwepo Kule kwa Binti Kahenga na Manzese squatter watafanya nini ilihali Hakuna Hata Barabara ya Pikipiki?

Pia Ijulikane Katika Mipango Miji Kuna maeneo ambayo wamefanikiwa Kidogo Kuplan Kama Sinza na Mikocheni na kwingineko Kidogo, Ila wakazi wa maeneo Haya wamejenga na Kuzuia Mitaa kwa kufanya maeneo Hayo Kuwa mali yao!

Tunamuomba Waziri wa Ardhi asimamie Hizi kero Kwanza na sio just Kufanya planning za Mambo Makubwa wakati Madogo Yamemshinda!!
 
Mpango ni mnzuri sana kinadharia.Ila miundo mbinu katika majiji yetu ni tatizo kubwa je vijijini itakuwaje?Kwa sehemu za mijini nadhani mnaweza mkafanikiwa kwa kiasi kikubwa.
 
Zitaandaliwa post codes kwa kanda ili kurahisisha utambuzi wa Watumishi wa huduma kwa watanzania.
 
Nchi nzima inatakiwa kwanza ipimwe na kuwekwa katika blocks ambazo ndiyo zitakuwa ni kama references. Baada ya kuipima nchi nzima basi kuwapo na uhakiki wa kila nyumba na mitaa na kuingiza katika mifumo ya kisasa siyo hii ya kuchungulia mikaratasi ya siku nyingi ambapo pengine walioziandaa hizo documents hawapo.

Na hapa ndipo linapokuja suala la kuwapa mafunzo vijana wa kazi siyo nafasi zikitoka unakuta manager ndo anaenda badala ya watu wa kazi.
 
Wazo jema Mkuu licha hapo awali lilitukwaza kidogo kwa mada zetu kubebwa na vituo vingine na baadaye kuonekana tumecopy Kwai hasa wale wanapambazua alfajir
duuuh poleni sasa oke basi tupe mtiririko wa vipindi vyako ni lini na lini na muda gani
 
TUONGEE Asubuhi ipo kila siku kuanzia Saa Moja na Nusu Asubuhi hadi Saa Tatu kamili Asubuhi. Yahya M anafanya Kipindi JUMAPILI tu. Leo ni kwa dharura ya lini Sadam iliyomkumba muendeshaji wa Kipindi
Andante na don't miss this Sunday mada ni muendelezo wa wiki iliyopita so unaweza kuchangia mapema kwenye PM
 
Rushwa imeharibu Miundo mbinu ya Jiji Hili jiji lilishavurugwa Kitambo... Bora wajenge Jiji Jipya huko Kigamboni Space ni Kubwa kuliko Old Dsm City...

Hivi Vipindi Vimekaa Time Mbaya Sana Muda wa Kujiandaa kwenda Kazini na kinaendelea hadi time watu wakiwa kazini.
 
TUONGEE Asubuhi ipo kila siku kuanzia Saa Moja na Nusu Asubuhi hadi Saa Tatu kamili Asubuhi. Yahya M anafanya Kipindi JUMAPILI tu. Leo ni kwa dharura ya lini Sadam iliyomkumba muendeshaji wa Kipindi
Andante na don't miss this Sunday mada ni muendelezo wa wiki iliyopita so unaweza kuchangia mapema kwenye PM
Shukrani kaka,naakupongeza kwa wewe kufanya jitihada za kuwasiliana nasi kupitia jukwaa hili. Pia napendekeza ukiweka mada siku moja kabla uifafanue kwa uchache hata ambao tupo mbali -kwa maana ya kuwa hatuna access ya kuona kipindi chako moja kwa moja kwa naamna yoyote ile tuweze kuweka nondo zetu.

Ubarikiwe kuliko wanaume wote.
 
Huku kwetu iringa kuna namba zimeandikwa milangoni kwa kila nyumba,mtaa,kata na wilaya je hizi tofauti na hizi mpya?
Pili ni lazima uwe na sanduku la posta na simu ya posta ndipo upate anuani hizi?
Tatu vipi kuhusu wapangaji ambao mara nyingi ni watu wa kuhama hama?
 
Yahya M

Je zoezi hili la anuani za makazi litahusisha makazi ya aina zote (rasmi na yasiyo rasmi)? Makazi yasiyo rasmi, mara nyingi yanabadilika badilika, je wamejipanga vipi kukabiliana na changamoto hiyo hasa kushirikisha taasisi nyingine (ardhi, tamisemi etc). Tumeona mfano wa Madale DSM hivi karibuni ambapo makazi yasiyo rasmi kadhaa yamebomolewa.
 
Last edited by a moderator:
Shukrani kaka,naakupongeza kwa wewe kufanya jitihada za kuwasiliana nasi kupitia jukwaa hili. Pia napendekeza ukiweka mada siku moja kabla uifafanue kwa uchache hata ambao tupo mbali -kwa maana ya kuwa hatuna access ya kuona kipindi chako moja kwa moja kwa naamna yoyote ile tuweze kuweka nondo zetu.

Ubarikiwe kuliko wanaume wote.

Tupo katika mchakato na ndugu yangu Invisible tufanikishe hili. Tukipata njia nzuri itakayodhibiti kuvuja kwa mada zetu kwa wale copy n paste tutawajulisha Mkuu very soon.
 
TUONGEE Asubuhi ipo kila siku kuanzia Saa Moja na Nusu Asubuhi hadi Saa Tatu kamili Asubuhi. Yahya M anafanya Kipindi JUMAPILI tu. Leo ni kwa dharura ya lini Sadam iliyomkumba muendeshaji wa Kipindi
Andante na don't miss this Sunday mada ni muendelezo wa wiki iliyopita so unaweza kuchangia mapema kwenye PM
asante mkuu nitakupm ...pm mbili moja personal na ingine ya mada nitatupia swali kwa Nape
 
Naona huyo Mama Veronica amekomalia Kodi tu au ndio Dhamira yao tu Kodi na Si Vinginevyo?
 
Ahsante sana wakuu kwa michango yenu adhimu.
Tukutane JUMAPILI katika jukwaa la siasa

Asubuhi njema
 
Back
Top Bottom