LIVE ON Star TV: Kwanini Uwajibikaji kwa Viongozi si suala hiyari?

Yahya, tumefikia hapa sababu ya kuingiza sana uswahiba katika serikali.Waziri anafanay madudu na utamsikia anajigamba tena bila wasi wasi kwamba SIWEZI KUJIHUZURU kwa vile nilikuwa appointed na president!Maana yake ni nini hapa, rais amepewa madaraka makubwa sana kikatiba.

Inatakiwa mawaziri wasiwe wateule wa raisi mfumo ubadirike na kuwa wateule wa bunge,ili iwe rahisi kwa wabunge kuwawajibika.Leo hii kwa vile kaka yetu na raisi wetu amekalia uswahiba kila sehemu na kukimbilia kwa wazee wa Dar, sitegemei mabadiriko katika baraza lijalo tutarajie kuona sura zile zile katika kona tofauti na kuongezea rafiki zake kina Stephen Maselle. Na uwajibikaji usiishie kutoka madarakani bali sheria pia ipewe nafasi kwa waliotuhumiwa kufisadi pesa ya umma.

Na kwa nini Dr Mrema asikabidhiwe kitengo kipya cha kudeal na maadili ya mawaziri?
 
Ndg Yahya habari za kazi?

Mie nadhani tatizo kubwa lililopo kwenye serikali yetu haina kiongozi wa juu kwa maana wote wanafika mahali na kujiona wako sawa. Ninashaka pia mkuu wa kaya nae anaweza kuwa na mgawo wake katika madudu haya ya wizi unaofanyikan kwanini apate kigugumizi kuchukua hatua? Hadi sasa ameeleza CC ya chama chake nia ya "kulisuka" upya baraza lake la mawaziri, kuna haja gani kueleza CC na kusuburi wiki nzima kuchukua hatua leo mawaziri wote wako likizo maana hawajui fate yao. Hakuna uwajibikaji na kuna kumalizia deals zilizokuwa zina hang. Jambo la msingi ni kuwachukulia hatua za kisheria maana taarifa za CAG zinathibitisha kuwa na kughushi na hili ni kosa la jinai.

Kura ya kutokuwa na Imani kwa Pinda ni kutokuwa na Imani kwa serikali ya JK mwenyewe.
 
'CCM ina wenyewe, na wenyewe ndio sisi na tuna wanachama kibao' Wenye CCM yao hawasomi St kayumba, hawaishi maeneo machafu, hawauzi nyanya sokoni, wanakaa kwenye majumba ya kifahari, wake zao wakiugua Chunusi wanapandishwa ndege kutiwa nje.

Kutekeleza haya watanzania ambao ni wanachama kibao lazima waibiwe ndio maana nchi hii inaliwa pande zote kwa kujifanya wateja wa vyama.
 
rais kateua mawaziri rafik zake kwahiyo sifikirii kama ataweza kuwasimamia, kisha andaeni mada ya rais apunguze safari za nje zinatumia pesa nyingi.
 
Mh rais ndo anazidi kutuchanganya wananchi, kama hamna mtu mwingne wa kuwawajibisha mawaziri na makatibu wakuu,ya nini tuwalaumu wengne wakati rais ndo tatizo? Tunazunguka zunguka wakati rais wetu ndo kikwazo?

Vote of no confidence kwa waziri mkuu kwa miwani yangu naona inamstahili impate rais, hapa naona watu wanakwepa kesi ya kuitwa wahaini kwa kumwajibisha rais.

Nani amfunge paka kengele???
 
Taarifa ya CAG ni ushahidi tosha kabisa kuwafikisha mahakamani wale wote waliotafuna mabilioni ya pesa za walipa kodi. DPP na DCI wako kimya kabisa kana kwamba hakuna lolote lililotokea.

Kuna kila dalili kwamba kuna mtandao mkubwa wa watumishi wanaotafuna fedha hizi. Nadhani hata matatizo ya nyongeza za mishahara kwa watumishi hasa wa kada za kati na chini yanasababishwa na upotevu mkubwa wa fedha unaohusisha mtandao mpana.

ULAJI HUU NI SAWA NA MKULIMA ANAYETAFUNA/KULA HATA MBEGU ZA MSIMU UNAOFUATA. Ndiyo maana maisha ya kawaida ya kila siku yanazidi kuwa ovyo kwa gharama kupanda kila siku.
 
serikali iliyoingia madarakani kwa hila itaongoza nchi kwa hila, leo mawaziri watajiuzuru lakini mi sioni mabadiliko yeyote makubwa haijalishi nani atateuliwa badala yao, kwani hii ni report ya kwanza? mbona hali ni ile ile?

Tukitegemea wabunge walete mabadiliko tunakosea, tukisubiri serikali ilete mabadiliko tunakosea, mabadiliko lazima yaanzishwe na yasimamiwe na sisi wananchi.
 
Hivi mawaziri vivuli walikuwa wapi? na wao wanapaswa kuwa "watch dogs" wa hizi wizara? Kama anavyosema Mrema, wanangoja mpaka CAG anafanya "postmortem". Walikuwa wamelala? Au na wao wanakatiwa kitu kidogo wakae kimya kivulini?
 
yahya! Nchi inahitaji overhaul ya system nzima, hakuna mtu mmoja ambae tunaweza kumhold responsible kwasababu pesa inapita kwenye mikono mingi sana "sign nyingi sana mpaka pesa kufika kwenye kazi husika"
 
naomba watanzania tujue tunakufa kwaajili ya watu wachache tuchukue hatua yakuwajibisha kwakuiondoa madarakani serekali nahao wezi wafunguliwe mashtaka bada yakufukurwa kazi.
 
Mi ninachoona uwajibikaji umekuwa unawashinda viongozi wetu kwakuwa wameweka maslai yao mbele na wengi wamekuwa wakilindana kwa mitandao walioianzisha ndani ya vyama vyao, pengine ifikie wakati rais apunguziwe mamlaka,
 
Viongozi wetu hawako tayari kuchukua jukumu la kujiuzulu linapotokea tatizo la kiutendaji katika idara ama wizara kwa sababu ya kushindwa kuelewa dhana nzima ya uwajibikaji.

Kila mmoja anadhani kwamba akichukua jukumu la kujiuzulu kama ishara ya kuwajibika ni sawa na kukubali kwamba yeye ndiye aliyetenda makosa hata kama kweli hakufanya makosa lakini watu walioko chini yake ndio wametenda makosa na yeye hakuchukua hatua za kuwawajibisha.

Hadi hapo tutakapoweka kipengele cha uwajibikaji katika katiba mpya kwa sasa sioni dalili za uwajibikaji chini ya viongozi/uongozi wa sasa.
 
DEUS KIBAMBA: Mheshimiwa rais ana madaraka makubwa, sisi wengine tumekua tunasema asitumie madaraka yake yote lakini yeye hatumii kabisa

Mytake: Kibamba kasema exactly kitu nilichokua nafikiri, well said kibamba.
 
Habari star tv? Tatizo la uwajibikaji katika nchi yetu ni kansa mbaya sana.

Najiuliza, hivi KIKWETE tumempe madaraka, nguvu na uwezo wa kusimamia mali ya nchi na ustawi wa watu wake, inakuwaje leo anashindwa kufanya mambo yaliyo bora kwa kuwajibisha wezi na mafisadi kwa kutumia mamlaka yake bila kutafuta mbeleko ya chama chake???

Uwajibikaji ni utamaduni katika jamii, tendo la uwajibikaji hufanywa na viongozi wanaofanya kazi kwa ajili ya wananchi, lakini kinyume na dhana hii viongozi wa Tanzania hawafanyi kazi kwaajili ya watanzania.

I believe, Rais ni mdhaifu pasipo shaka na asiyetaka kuamini aendelee kuamini hivyo.
 
Wananchi tunafika hatua tunafikiria kuwa tanzania labda si nchi,ni genge la wahuni wenye mamlaka! Tuna TAKUKURU,tuna DCI tuna polisi na usalama wa taifa wote wanakula kwa kamba zao...taasisi zote tajwa apa hazisubiri rais atoe kibali cha kuwakamata mawaziri majambazi ila zimeamua tu kuliua taifa letu kwa kushirikiana na mh rais. Ni hatari kwa taifa lisilojitambua na wote kwa kuangamiza taifa ili mna la kujibu mbele za Mungu!
 
nachokiona ni kubadili mfumo mzima wa upatikanaji wa viongozi wetu na hasa hawa presidential appointees. ifike pahala wengine wawe wanaajiriwa na kuwajibika directly kwa wananchi kwa kuwa na assesment sheets ambazo ndani ya muda wake wa ajira wana-assesiwa then wanapewa mkataba mwingine.

Lakini pia ifike Pahala tuangalie tatizo la mfumo wa upatikanaji linatokana na "tabia binafsi za rais anayewateua" kuwa mpole na mzembe mnooo...TUMWONDOE KOCHA tuone kama wachezaji wetu ni wabovu kwelii???..sio kila wakati timu ikifanya vibaya tatizo linakuwa ni WACHEZAJI...maranyingi sana tatizo limekuwa ni KOCHA na sio wachezaji...TUMNGOE KOCHA/RAIS TUONE TIMU ITAVYOGAWA DOZI.
 
Sijui kama nchi hii ina mipango mizuri ya kuwapata viongozi, maana naona kuna viongozi wengine hawana uzalendo kabisa, Waziri ananunua nyumba $410 huku mwananyamala hakuna vitanda na madaktari wanagoma kwa sababu ya 20,000/= ya posho. Mh Rais fukuza wote hawa maana kama TWIGA amepanda ndege bila mtu kumuona basi hii wizara ina watu vipofu.
 
Atulikula vyao wakati wa uchaguzi,,ndo maana haya yote yanatupata....aliyekupa kitu huwezi kumwajibisha..baba akiwa hajali nyumba yote watu wanakuwa hawajali
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom