Live On Star TV: Kipindi maalum na TRA kuhusu mauzo na utoaji risiti

Star TV

Member
Jan 1, 2008
21
26
Ndugu Wana JF,

Tunapenda kuwatangazia kwamba, usiku huu, kuanzia saa tatu na nusu mpaka saa nne na nusu (21:30 - 22:30 EAT) tutakuwa na kipindi cha moja kwa moja (LIVE) kwenye station yetu ya Star TV.

Wageni wetu watakuwa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA).

Tunapenda kuchukua fursa hii kuwaomba wale wote wenye maswali ambayo yanahusiana na kodi na utoaji stakabadhi za mauzo (risiti) wayaandike kwenye uzi huu ili mtangazaji wetu apate kutuwakilishia pale itakapofaa ndani ya kipindi hiki.

Aksanteni.
 
MASWALI KUHUSU STAKABADHI ZA VAT.

  1. Kuna tofauti gani kati ya VAT on invoice na VAT on Receipts?
  2. Kuna baadhi ya makampuni wanatoa Invoice zisizo na VAT codes wasema wanatoa VAT receipt baada ya kupokea malipo Je hii ni sahihi?
  3. Kwa mfanya biashara ambae hajafanya mauzo yoyote kwa Mwezi mzima kwa mfumo huu wa VAT machine bado anahitajika kupeleka NIL report?
 
Mimi mfanyabiashara niliesajiliwa VAT ninayetumia mita za umeme na Maji zilizosalijiliwa kwa jina la Mwenye Jengo la biashara ninawezaje kudai makato ya VAT nilizolipa kwa huduma hizi?
 
Swali kwanini gharama za ukokotoaji zilizo wekwa kwenye website yao zinakuwa tofauti na gharama ambazo unakuja kutozwa baada ya kuagiza gari toka nje ambapo unajikuta wakutoza zaidi tofauti na gharamaulizozipata kwenye website zao.

Swali la pili kila mtanzania anaponunua kitu chochote analipia na vat ya 18% ikiwa nusu tu ya wa tanzania wakifanya manunuzi ya shs 5000 kwa mwezi walipa vat ya sh 900 ambapo ni zaidi ya trilion moja kwa mwezi hizo hela zingine zinaensa wapi? au kunaudhaifu wa ukusanyaji wa kodi?
 
Umuhimu wa stakabadhi kwenye maduka yetu ya mitaani ambao hawamo kwenye VAT; ni bidhaa gani ambazo zinahitaji stakabadhi na zipi hazihitaji stakabadhi?
 
Ndugu Wana JF, tunashukuru kwa ushirikiano wenu. Tunapenda kuwaarifu kuwa kipindi hiki kitamalizika saa nne na dk 50 (22:50 EAT) badala ya 22:30 kama tulivyopanga awali kutokana na kipindi kuanza nje ya muda tuliokusudia awali.

Aksanteni.
 
TRA inafanya juhudi gani kukabiliana na wafanyabiashara wenye vitabu viwili viwili? Pia inakuwaje wafanyabiashara wanakuwa na uwezo wa kukuuzia risiti peke yake (mfano ukiwa unataka uprove ofisini kuwa ulinunua kitu fulani unaweza tu ukaenda kwa mfanyabiashara na akakuuzia risiti empty yenye tin number) ?
 
MASWALI KUHUSU STAKABADHI ZA VAT.

  1. Kuna tofauti gani kati ya VAT on invoice na VAT on Receipts?
  2. Kuna baadhi ya makampuni wanatoa Invoice zisizo na VAT codes wasema wanatoa VAT receipt baada ya kupokea malipo Je hii ni sahihi?
  3. Kwa mfanya biashara ambae hajafanya mauzo yoyote kwa Mwezi mzima kwa mfumo huu wa VAT machine bado anahitajika kupeleka NIL report?

Ngoja nikujibu:

Invoice vat na receipt vat tofauti inakuja ktk utengenezaji, invoice mara nyingi ni computer made ambayo inapita kwenye esd, Receipt vat yenyewe ni receipt inayo toka kwenye etr so invoice ina detail nyingi kuliko receipt.

- Kutoa invoice ambayo haijapita kwenye machine ni makosa, unapaswa ulipe then upewe fischalized invoice. sema tatizo lipo mfano upewe invoice ambayo imepita kwenye esd alafu usilipe wakati invoice ishaenda tra hilo tatizo ndio watu hawataki ndio maana wanafanya hayo makosa.

- mwisho kama hakuna mauzo yoyote itabidi utume report yenye zero wao wanataka report kila siku.
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom