Live: Nusu fainali ya challenge cup

Wamefungwa SIMBA si watanzania , wewe na akili yako kweli unamuweka Kaseja golini? ha ha ha ha hapa ndo mtajua kwa nini Maximo alikuwa hamtaki KASEJA
 
Wamefungwa SIMBA si watanzania , wewe na akili yako kweli unamuweka Kaseja golini? ha ha ha ha hapa ndo mtajua kwa nini Maximo alikuwa hamtaki KASEJA
Haya mambo ya Usimba na uyanga ndio yanaiharibu timu ya taifa..
 
cecafa haiwezi kukubali tutolewwe......... watakula wapi?

nilikuwa natizama SS9 mechi za leo, mtangazaji alisema coordinator wa marefa wa FIFA kwa ukanda huu alikuwapo leo uwanjani, labda ndio sababu CECAFA wameshindwa kuichakachua mechi ya leo.
 

Timu ya Uganda leo imeiadhibu timu ya Kilimanjaro Stars kwa mabao 3-1 katika hatua ya Nusu Fainali katika mchezo uliomalizika hivi punde kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.


Katika mchezo huo Kilimanjaro Stars ndiyo ilikuwa ya kwanza kupata bao la kuongoza kupitia mshambuliaji wake machachari, Mrisho Ngasa katika kipindi cha kwanza bao lililodumu hadi timu hizo zilipokwenda mapumziko.


Kipindi cha pili Uganda ilikuja juu na kuandika bao la kusawazisha kupitia Beki wake Mwesigwa aliyepanda na kufunga mpira wa kichwa kufuatia mpira wa kona na kufanya timu hizo kumaliza dakika 90 zikiwa sare ya 1-1 na kwenda katika dakika 30 za nyongeza kabla ya mchezaji,Emmanuel Okwi,kuongeza maumivu kwa kufunga bao safi kwa kichwa na baadaye kusababisha penati iliyoipatia Uganda bao la tatu na la ushindi katika mchezo huo.


Kwa matokeo hayo sasa Uganda itavaana na Rwanda katika Fainali za michuano hiyo siku ya Jumamosi, huku Kilimanjaro Stars ikimenyana na Sudan iliyochapwa na Rwanda mabao 2-1 katika kuwania nafasi ya tatu ya michuano hiyo.mia
 
Haya mambo ya Usimba na uyanga ndio yanaiharibu timu ya taifa..

KATAVI

Hakuna cha U Simba na U Yanga, tuwe wakweli na tujiulize ni kwa nini tangu arudishwe timu ya Taifa baada ya Maximo kuondoka ni matokeo gani tunayo?

Ukiangalia uchaguzi wa timu hii, kila mtu alijiuliza hivi kweli tumedhamiria?

Tumevuna tulichopanda
 
Kumbe ndiyo maana Fuso ni muhimu sana Taifa stars.
Wachezaji wanashindia Chips mayai, halafu jioni utawakuta Baa na bangi juu.
 
wewe figganigga sija kimbia. mimi ni mzalendo...hahaaha

Wachezaji wetu wanatunyima raha na kutufanya kujawa na machungu sisi mashabiki. kila tukicheza.sasa kaseja, boban, juma nyoso, juma lidondo, chuji na nurdin sasa washaliwasha. na hii hali ya hewa. Bora hata tegete yeye huwa anakesha sehemu band ya taraab ya mzee yusuph inapopiga.hahaaaa...!!.mia
 
Haya mambo ya Usimba na uyanga ndio yanaiharibu timu ya taifa..

Kwani hujui makocha wote wale ni simba damu? Mi nimefrahi sana tulivyo tolewa na fraha yangu itaendelea tukishika nafasi ya nne julio na mwenzie watakuwa wamefungwa midomo walitamka wazi eti hakuna mchezaji wa kumchukua yanga eti simba inaongoza ligi ndo inawachezaji wazuri kuliko timu zingine wamevuna walicho chagua.
 
Hapana, waliokimbia ni Mkwasa, Tenga na Bala ..
Bala is always here....

Pole zangu nyingi ziwafikie 'wazee wa best luza'...Kwa kweli tumeytaka wenyewe na tumestahili kuvuna tulichokipanda na tena tushukuru Mungu kwa kufikia hata hapo tulipofika maana kwa jinsi nilivyoyaona mashindano haya bingwa alitakiwa awe kati ya Uganda,Rwanda,Burundi,Malawi na Zimbabwe...Hawa wamecheza soka la kuvutia hasa ukilinganisha na 'wazee wa best luza'....

Fikiria timu inatangazwa wiki moja kabla ya mashindano pasipo michezo ya kirafiki wala eti wanategemea mazoezi ya Coco Beach ndo yatawapatia ushindi.....Halafu,kulikuwa na umuhimu gani kwa kocha(Julio) kutangaza majina ya wachezaji 28(na baadae yakawa 30) badala ya kuteua moja kwa moja majina ya wcezaji 20 wanaohitajika?,kitendo cha kuctangaza majina ya wachezaji 30 na kuwachuja siku 2 kabla ya mashindano kilichangia kwa kiasi kikubwa kudhoofisha maandalizi ya timu,ni heri angetangaza tu majina ya wachezaji 20 kisha wakaanza mazoezi ya moja kwa moja kujiandaa kwa mashindano....Pia nilishangazwa sana na kitendo cha kumteua Charles Boniface kuwa kocha mkuu ilhali yupo nje ya nchi(RSA),kocha naye amerudi toka RSA siku 2 kabla ya mashindano kuanza,hiki ni kichekesho na kinaonesha ni jinsi gani hatupo makini katika mambo muhimu(tunapenda sana mambo ya zimamoto)....

Maoni yangu:-
Kuna haja sasa ya TFF kujiondoa katika mashindano makubwa(yanayoandaliwa na CAF na FIFA) kwa miaka mitano ijayo ili kuweza kujipanga na kutengeneza timu ambayo itakuwa ni ya kiushindani zaidi badala ya kuwategemea wachezaji aina ya Kaseja,SMG,Nyoso na wengine ambao kimsingi wameonesha kushindwa kuliwakilisha Taifa kama sisi tunavyotaka......Ikishindikana katika hili basi tuiendeleze timu ya Ngorongoro Heroes ambayo imejaa vijana wenye vipaji(tuige mfano wa Zimbabwe ambao katika mashindano haya ya CECAFA wameleta timu ya U23) timu hii ya Ngorongoro Heroes ambayo imeonesha soka safi katika mashindano ya COSAFA Metropolitan(U23) iongezwe nguvu kwa kuwajumuisha Mbwana Samatta,Thomas Ulimwengu na Shomari Kapombe....Hapa tutangeneza timu ambayo itakuwa ni imara na tishio katika Afrika...

Wasalaam.

Bala
 
Kwani hujui makocha wote wale ni simba damu? Mi nimefrahi sana tulivyo tolewa na fraha yangu itaendelea tukishika nafasi ya nne julio na mwenzie watakuwa wamefungwa midomo walitamka wazi eti hakuna mchezaji wa kumchukua yanga eti simba inaongoza ligi ndo inawachezaji wazuri kuliko timu zingine wamevuna walicho chagua.

Hata Mkwasa nae ni simba damu?
 
mi nilikuwa napenda sana itoke kwa uganda walikuwa washapaniki wanafikiri wanabebwa na jambo kubwa kuliko yote mgosi hajui anachofanya ni gharasha mbaya..

ngoja tusubirie mshindi wa nne..
 
Back
Top Bottom