Hivi nyie viwavi wa cdm mbona mambo ya ndani ya ccm yanawakuna
Majumuisho (yanaendelea...)
2. Prof Issa G. Shivji: Mwalimu alikuwa ni kiongozi mzuri mwenye maadili. Alijaribu kusimamia mfumo japokuwa hakufanikiwa kujenga UJAMAA. Zamani kulikuwa na mabeberu ambao sasa wanaitwa "wawekezaji." Kwa sasa tunaenda kutafuta uongozi toka kwao. Tumeanza kumsaliti Mwalimu tulipoanza mfumo wa Kiliberali mamboleo, tukaleta uwekezaji. Tatizo la sasa ni mfumo. Someni Mwongozo wa CCM wa mwaka 1981 kwamba limejitokeza tabaka jipya dhidi ya Ujamaa, tabaka hilo litashinda. Hakuna Mwongozo mzuri kama huo, utafuteni muusome. Sasa tumeanza kutambua baada ya kuanza Uliberali Mamboleo, miaka 20 sasa, kwamba wakombozi wetu sio wawekezaji. Kilimo Kwanza: PM alienda Brazili, vijana wetu tumewafanya kuwa wavivu. Je, wakulima wetu tunapouza ardhi tunawapeleka wapi? Sisi tunazungumzia juu ya UTAWALA BORA, mimi sipendi UTAWALA BORA bali Azimio la Arusha lilizungumzia juu ya UONGOZI BORA. UTAWALA BORA ni wazo la World Bank. Je, utakuwa na Ubepari wa Kitaifa chini ya Ubeberu? Kuna mabadiliko makubwa ya Sheria ya Ardhi yanakuja ambayo yataleta uwekezaji...
majumuisho yanaendelea:
3. Mzee kingunge ngombale mwiru: Nafurahi kwamba kwa sasa watu wanazungumzia ujamaa kwa sasa......................... Naona uvivu hata kuandika anayozungumza huyu mzee, naona amepitwa na wakati!