Live..mdahalo shivji,kingunge...itv

Leteni Updates wakuu au mnataka mlimwe BAN?
updates Plz

Kingunge: Wawekezaji wengi hawawaaimini watanzania! Wameenda Nigeria, Ghana, nk. Nchi hii wanaotulisha ni wakulima wadogowadogo na kama tungekuwa na mpango endelevu tangu tulivyoanza kwa ile mikoa 4 (Ruvuma, Iringa, Mbeya na Rukwa) tungekuwa mbali sana kwa sasa!
 
Asante mkuu
 
Sasa ni maswali:
1. Kwa Kingunge: (a) Mipango mikakati mliyoiweka wakati wa Uhuru, nani mliowaweka madarakani waliiua? (b) Ardhi ni ya nani? Watz hawajafundishwa thamani ya ardhi yetu, eg Mlima Kilimanjaro unaingiza TSh ngapi kwa siku, mimi nikiulizwa ardhi ya mlima Kilimanjaro ina thamani gani siwezi kujibu.
2. Kwa Prof. Shivji: Je, tumeandaliwaje juu ya kupambana na mabepari wa urasimu maana mtu akitaka kupata kiwanja huchukua muda mrefu sana.
3. Kingunge ametupa History kuhusu kumiliki ardhi, kwa nini mpaka sasa hivi mkulima wa sasa hivi hajawa na maisha mazuri. Wewe Kingunge umekaa muda mrefu madarakani na umetoka aidha kwa kulazimishwa au kwa hiari, ni siri yako mwenyewe, kwa nini mkulima wa chini hajanyanyuka kimaendeleo?
4. Wakulima wakubwa na wadogo, tuendelee kupambana na hawa mapoka wa ardhi wanaowaumiza mama zetu huko vijijini.

Maswali yanaendelea:
5. Kwa Kingunge: Kwa nini mpaka sasa hakuna viongozi wanaojitoa kama Mwalimu Nyerere?
6. Sera ya Kilimo Kwanza imefaulu kwa kiasi fulani kwa kuwapa wakulima pembejeo lakini soko la mazao ni tatizo. Serikali ihakikishe kwamba soko lipo ndipo tutakapohakisha kuwa wakulima wanafaidika. Hakuna Kilimo kama hakuna Soko.
7. Swali toka kwa Mtembe, Mhadhiri Mwandamizi wa Lugha: Wakulima wengi hawapati habari na kama zinafika zinakuwa na lugha ambayo ni ngumu kuielewa (karibu 90% ya wakulima hawapati taarifa kulingana na utafiti uliofanyika).
 
Maswali yanaendelea...............!
8. Rashidi Selemani toka Makongo High School, Kidato cha Tatu: Kuhusu viongozi kukosa kujituma ni ukosefu wa National Interests na sasa viongozi wana Self Interests ni kwa sababu ya kukosa National Patriotism hasa wakati wa Rais Mwinyi. Tujiulize kuwa hivi tunapigania nini? Je, ni manufaa binafsi au manufaa ya jamii nzima? (Huyu dogo amepigiwa magofi sana maana anaongea kwa kujiamini mno na inaonekana kuwa ana uelewa mkubwa sana).
 
Kuna Bwana Mdogo toka Makonga Sekondari ni SPEAKER OF THE DAY.Dogo huyu kafunguka watu wazima wote kimya.
 
Maswali yanaendelea.................
9. Elizabeti Mashawa, Loyola High School, Form V: Enzi za zamani ilikuwa ni rare kwa watu kufa njaa, Je, kama Nyerere alifanya watu wakajitegemea, viongozi wetu wanatumiaje mikakati ya Nyerere ili kujitegemea kuliko kutegemea nchi za nje?
10. Mwalimu aliondoka lakini hakuondoka na mambo yake, wapo watu ambao alifanya kazi nao wapo mpaka sasa. Katika Azimio Arusha kuna mambo yaliyotiliwa mkazo, km kujitegemea. Wale ambao walikuwa wanafanya kazi na Mwalimu inawezekana kwamba waliomzika waliweka jiwe kubwa ili kama angefufuka basi afufukie baharini na sio Tanzania. Sasa hivi kuna migogoro ya ardhi mahali mbalimbali lakini wazee hawafanyi chochote. Wasomi ndio wanaoiangamiza Tanzania ijayo maana ukimuuliza msomi sasa hivi ukimaliza masomo ataenda kufanya nini atakwambia kwamba ataenda kujikusanyia maana kila mtu anachukua chake mapema. Tuache ngonjera kupambana na rushwa.
11. Christopher Ole Sendeka, Mfugaji, Mwakilishi wa Wananchi Jimbo la Simanjiro: Katika Ilani za Uchaguzi tumekuwa tunaweka mambo mbalimbali ya kuyatekeleza. Tukichukua suala la Ardhi, maelfu ya ekari kupitia mambo ya madini na kilimo, kupitia wageni. Hoja iliyopo ni kuangalia yaliyo mbele yetu. Mwalimu hakuwa vuguvugu, kama kuna jambo lililohitaji kuwa na ujasiri alisimama imara. Naomba kupata mawazo kutoka kwa Prof Shivji na Kingunge mnachukua hatua gani...
12. Joseph Emanuel: Tukae kimya kwa dk moja kumkumbuka Mwalimu (wote wakakaa kimya). Katika nchi ya Tanzania tulitakiwa tuishi kijamaa, taifa lenye misingi ya kupendana, lakini viongozi wa Serikali wanaongea bila kuangalia tufuate misingi ipi. Mwalimu alisema kwamba ili tuendelee tunahitaji WATU, ARDHI, SIASA SAFI na UONGOZI BORA. Sasa hivi hakuna uongozi bora. Tunaposema KILIMO KWANZA, An Agriculture Revolution is not an overnight event, tukae na wananchi tuwaulize kwamba wanahitaji nini...
 
Mbunge Ole sendeka ameichana CCM namna inavyotekeleza dhana ya kujivua gamba kwa kupeana siku za kuondoka chamani badala ya kuwachukulia hatua.Hii inatokana na dhana ya NEC na CC ya CCM kuwapa siku 90 watuhumiwa wa ufisadi kujiondoa chamani.Anaitaka CCM ichukue maamuzi badala ya kupeana maneno yanayoonekana kuwa ni kuogopana.Watu wamempigia makofi sana kwa hoja hii nzito ambayo imewakuna wanaharakati wengi na wapenda mageuzi.
 
Maswali yanaendelea...............!
8. Rashidi Selemani toka Makongo High School, Kidato cha Tatu: Kuhusu viongozi kukosa kujituma ni ukosefu wa National Interests na sasa viongozi wana Self Interests ni kwa sababu ya kukosa National Patriotism hasa wakati wa Rais Mwinyi. Tujiulize kuwa hivi tunapigania nini? Je, ni manufaa binafsi au manufaa ya jamii nzima? (Huyu dogo amepigiwa magofi sana maana anaongea kwa kujiamini mno na inaonekana kuwa ana uelewa mkubwa sana).

Huyu dogo kwa kweli anaonekana yuko well informed! Nimependa alivoongelea uzalendo!
 
Ole sendeka kamchana live J..... kasema hakuna haja ya kuwaambia mafisadi watafakar afu waamue kama watatoka kwenye chama au la!alichotakiwa ni kuwatimua tu!nimeipenda hiyo.
 
Mbunge Ole sendeka ameichana CCM namna inavyotekeleza dhana ya kujivua gamba kwa kupeana siku za kuondoka chamani badala ya kuwachukulia hatua.Hii inatokana na dhana ya NEC na CC ya CCM kuwapa siku 90 watuhumiwa wa ufisadi kujiondoa chamani.Anaitaka CCM ichukue maamuzi badala ya kupeana maneno yanayoonekana kuwa ni kuogopana.Watu wamempigia makofi sana kwa hoja hii nzito ambayo imewakuna wanaharakati wengi na wapenda mageuzi.

Hivi nyie viwavi wa cdm mbona mambo ya ndani ya ccm yanawakuna
 
Sasa Majumuisho:

1. Dr. Ng'wanza Kamata: Suala la kwa nini hali ya wakulima toka uhuru mpaka leo imekuwa ni ile ile. Mchango wa madini kwenye pato la taifa ni mdogo sana. Kwa hiyo misingi ya mapato yetu ipo kwenye Kilimo. Pia kuna hali ya kujidanganya kwamba hatuna uwezo. Je, mtaji unapatikana wapi. Tunaweza kupata mtaji kutoka ndani, Je, wakulima wanaozalisha kwa ziada, hiyo ziada inaenda wapi. Kwa hiyo uwezo wa kupata mitaji bado upo ikiwa tu tutabadilisha mitazamo na mifumo yetu. Sheria za Ardhi zimetengenezwa wakati nchi yetu imeingia kwenye Soko Holela (Huria), Chachage alikuwa anatumia neno "Tunajiandaa ili kuwekezwa!" Kuna wanaowapora kwa mujibu wa Sheria, Makuwadi wa Soko Huria. Je, mabadiliko yanakujaje na nani anayaongoza. Je, tunapambanaje na mfumo uliopo maana mfumo huu ndio unaowafanya wakulima wawe kama walivyo. Nani atakuwa AGENT wa mabadiliko: Wakulima, umoja wa wakulima, maskini wavuja jasho wa mjini, nk?
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom