wanamfurahisha Rais? Nimekasirishwa na issue ya Masoud Kipanya! Kweli wanahabari wa Tanzania bado sana!
Hata kwa washindani masoud Kipanya hayupo? Hivi wana akili hawa? Ndio maana nashinda humu JF sitaki habari zao!mbona hata nathan anachora kama masoud au kisa hana jina..
mbona hata nathan anachora kama masoud au kisa hana jina..
Hizi tuzo batili haiwezekani gazeti la uhuru na mzalendo hayamo!nitawapatia live update kutoka hapa Diamond Jubilee ambako muda mfupi ujao waandishi kadhaa nchini watatuzwa kwa kutambua mchango wao katika kuhabarisha jamii kwa mwaka 2011.
pia atakuwepo mwandishi bora wa jumla ,huyu atalamba takribani sh milioni 7
wageni wanaingia kwa wingi
nadokezwa kuwa TBC1 watakuwa live
Updates
Najulishwa hapa kuwa pia Rais atatumia muda huo kutoa hotuba.
Mwandishi bora wa jumla ni kati ya hawa-David Azaria (Habari Leo, Mwanza); Neville Meena (Mwananchi ,Dar ) Joseph Bura(TBC Taifa ,Dar) na Polycarp Machira(The Citizen ,Dar).
1.mpiga picha bora
ni Khamis Said kutoka uhuru
2.mchoraji bora wa kibonzo
ni Nathan Mpangala
alichora katuni iliyoonesha wabunge wakijongeza posho huku wanananchi wakisota
3.Utawala bora gazeti
Nevile meena-Mwananchi
4.utawala bora tv
emmanuel buohera-itv
5.utawala bora radio
Noel Thomson
6.Habari za Malaria-Gazeti
Audax Mutiganzi-Rai
7.Habari Malaria-Radio
Gelvas Hubile-TBC
8.Mwandishi bora Michezo-gazeti
Iman man
9.Habari za michezo -radio
Abdala Majura
10.Habari michezo Tv
Anuary Mkama
11.Habari za Watu wenye ulemavu-gazeti
David Azaria
12.Watu wenye ulemavu -tv
Lekoko-Channel ten
13.Mwandishi wenye ulemavu-radio
Tuma Dandi
14.Jinsia -Gazeti
Nasra Abdalah-Tanzania daima
15.Habari za Ukimwi-Gazeti
Elias Msuya
16.Habari za UKIMWI-Radio
Beatrice Nangawe
17.Habari za Afya
Sharifa Karokola
Wamemkomoa Masoud Kipanya!! Wameniudhi kweli! Masoud huwa anagusa pasipo gusika alafu wanamtema kirahisi hivi wanadhani tutakaa kimya!! Kwanini wanahabari wanaolilia uhuru wa habari wanakosa weledi? Kweli wamenichefua! Hata kwa washindani?Mimi namfahamu Nathan kwa siku nyingi kidogo, na kwa mtamzamo wangu nilitaraji kuona wote wawili wakichuana hapo (Masoud na Nathan) lakini tumesikia majina mageni kabisaaaaa!!
vipi kuhusu habari za mtandaoni?
Malaria sugu na faiza foxy hawapo?lol
Idea ya wa kuwa na hizi awards ni nzuri sana lakini naomba nitoe mapungufu;
1. Uendeshaji wa shughuli uko hovyo (sina maneno mazuri ya kutumia) ni hovyo kabisa. 3 or 2 nominees wanatajwa, wote wanatakiwa waende mbele then ndio mshindi anatangazwa? Kwa nini wasisome hao nominees then mshindi tu ndio anaenda mbele/jukwaani kupokea zawadi?
2. Clips za hao nominees hazioneshwi hivyo watazamaji hawawezi kuelewa ni habari gani hasa ilishinda.
3. Stage arrangement iko miguu chini sijui nianze wapi! Utaratibu mbovu sana. Hivi nyingi wanahabari hamuoni sehemu nyingine wanafanyaje kwenye awards ceremenies kama hizi?
4. Mshindi hapewi muda wa kutoa shukrani! hili nalo ni kituko. yuko mwanamama anaongea kama kafungiwa kengele. Mhehereshaji mwenziwe kabaki bubu!
5. Kwa kuangalia inaonekana kama hii ni 'formal event' Sielewi ni madharau au kutojua, lakini kuna watu wamevaa kama alikuwa anaenda kununua mboga mboga, hasa wanaume. Wanawake wamejitahidi lakini wanaume kwa kweli kazi ipo.[/QUOT
Frankly nakubaliana na wewe, ndio maana hapo juu nimesema wako dis-organised sana!!
Nilitarajia kwa habari za biashara tena kwa TBC no body could beat Stanley Ganzel.... lakini amekuja mtu hata sikumbuki kama nimewahi kumuona..... sijui nikalale tu!!
sasa kafunikwa nini?
Nayeye alikuwa anashindania.
Hebu tulia uandike ulichotaka kuandika kwa ufasaha ili tupate point za kuchangia.
Umekurupa mno.