Live in TBC topic what happened ktk uchaguzi wa Arumeru East

Huyu Mkumbo vp?
There is no court of law bana, kuna court of justice!!
 
Tendwa anasema maamuzi ya kutengua ubunge wa Lema ni legally process that y kuna kukata rufaa Baregu anasema kuna mkanganyiko.
 
BAREGU kichwa sana namkubali sana hoja zake anachallenge sana hapa.
Na Lwaitama namuona kama mshabik zaid
Maneno ya Nape yatumika kuwa eti CCM imekomaa kisiasa.
 
Lwaitama kwel mtata. Anashangaa inakuwaje Lema anavuliwa ubunge kwa madai ya kashfa wakati hiyo ndio sifa ya chama tawala huko Arumeru?
 
Hivi Tendwa alipataje u-judge, was it from Mwinyi, or Ben..coz he seemed to be
mwanachama/shabiki mzuri wa chama tawala.

Asilimia kubwa ya Majaji ni wanasiasa.

Unamuona Werema anavyopeleka miswada ya kishabiki Bungeni?

Unakumbuka mara baada ya uchaguzi wa 2010, alihojiwa kuhusu Katiba, akasema Tanzania haina haja ya Katiba Mpya. Kwa Jaji mwenye akili timamu hawezi kutoa kauli kama hiyo wakati Majaji Kibao kuanzia Nyalali, Kisanga na wengineo wengi wameishaikandia Katiba iliyopo kwa kuwa haina tofauti na Katiba ya mfumo wa Chama Kimoja.

Mzee Liundi (aliyekuwa Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi) mara baada ya kuondoka kwenye Tume, aliomba kugombea Ubunge kupitia CCM. Sasa watu kama hao wanakupa ushahidi kwamba alikuwa mshabiki wa CCM tangu akiwa Mwenyekiti wa Tume na si ajabu alicheza michezo michafu kuisaidia CCM ishinde. Ndio maana walipomfanyizia aliropoka kwamba angemwaga umafia uliofanywa na CCM nyakati za uchaguzi wakati akiwa Mwenyekiti wa Tume.

Tendwa akiondoka hapo alipo, sioni ajabu nikisikia anagombea Ubunge kupitia CCM. Maana yeye mapenzi yake kwa CCM sio siri tena bali yako wazi na siku zote CCM iko right ila wapinzani ndo wako wrong.

Lakini pia wapo Majaji ambao hawana vyama na wengine wanaunga mkono vyama vya upinzani.

Jaji Samatta aliwahi kuwa-challenge vyama vya upinzani, wasiishie kulalamikia ubovu wa Katiba, Mahakama haiwezi kufanya lolote bila kupelekewa shauri na wao Mahakama hawawezi kufungua shauri halafu walisikilize wao wenyewe na then watoe hukumu. Lengo ilikuwa ni kusaidia kuondoa sheria gandamivu ambazo zinapingana na katiba na haki za binadam. Bahati mbaya zama za utawala wake hakuna kesi ilienda, Mtikila akaja kupeleka rufaa yake zama za Jaji Augustino Ramadhani ambaye ni "mserikali" na hukumu yake sote tunajua.

Inasikitisha lakini ndo majaji wetu. Sikatai wasiwe mashabiki wa CCM, lakini uwe ni ushabiki wa kutenda haki unaoongozwa na kuangalia sheria zinasema nini. Mara nyingi watu huamini kwamba Jaji siku zote huwa yuko neutral na hana makengeza. Lakini majaji wetu wengi wana makengeza sana na hasa linapokuja swala la ushabiki wa vyama vya siasa na hasa kukipendelea chama tawala au kujipendekeza kwa chama tawala.
 
Najua wengi mshaacha kucheki TBCCM but just but that's what is happening Tatizo wanaongea english me siwapati coz nimetoka zile za kata na kingereza changu cha kichina aka feki.

Niambie japo kwa English yako usiyoiamini, wanasemaje?
 
Niambie japo kwa English yako usiyoiamini, wanasemaje?
Nimepata Haya
1. Tendwa kapewa ukweli kuwa alitumika kuisaidia ccm lakn akamkweza Lema kuwa Shujaa bila kutarajia kwa kauli yake ya wazee wakishiri na kumuua:
2. Tendwa alitaka kuvunja katiba kwa makusudi ya freedom of mvment Kwa kumzuia Lema kukanyaga arumeru
3. Wananchi wameamka hawataki poroji bali solution kwa problems zinazowasumbua,
4. Mkapa alipaniki alipoona cdma inatisha akashindwa kutoa walichofanikiwa na kuahidi cha mhim kwa wananchi akadandia kauli za kidwanzi
Wanasema police walijitahidi kulinda uchaguzi Kwa kuruhusu watu kukaa m100 wamesahau km walipiga mabomu bila sabb, mwngn anasema wananchi wameanza kuwa na Iman naNEC
Kifupi wachangiaji watatu
Lwaitama, Baregu, Mkumbo wapo fair na wanaongelea real what is moyoni wangu wamenikosha japo wanaminywa kwa kumaliza au kuingiliwa wasiongee na mwendesha kipindi ambaye ni mtetezi wa CCm na Tenndwa anatetea CCM na kujitegemea yy anababaika cjui Tatizo ni lugha au kiti cha motor Maana anajikanyaga sana,
Mwisho issue ya Lema
Ukiondoa TENDWA ALIYEKUBALI KUWA ILIKUWA FAIR
Wengine wote wameiponda ila kila mmoja Kwa maneno tofauti.
Hiyo ndio nimepata
 
Hivi Tendwa alipataje u-judge, was it from Mwinyi, or Ben..coz he seemed to be
mwanachama/shabiki mzuri wa chama tawala.

huyu tendwa huwa namfananisha na refa.anayeshabikia timu moja wapo kati ya hzo 2.anazochezesha.ikifunga ya kwake anapuliza pyenga.afu anashangilia kiaina.au akiona timu siye penda imefunga lazima atatafuta penalt kwa timu yake.ndiyo hayo ya mzee tendwa!
 
This Week In Perspective
Tuangalie hivyohivyo mkuu tutakuwa tunaokota okota baadhi ya vijineno ukiunganisha lazima utapata picha nzima2 hi lugha bwana we acha tu! Asante kwa taarifa mkuu!

watu wanacheck movie za kihindi na wanakutafriria sembuse na hii mkuu? Hahahahahaaa! Hivyo hivyo.
 
Back
Top Bottom