Mpaka naondoka kituoni hali ilikuwa kama hivi:
Nilipiga Kura yangu saa 1.30 asubuhi nikiwa mtu wa 5.
Uhakiki wa wapiga kura unachua muda:
Ofisa wa Kwanza wa NEC anapokea kadi ya mpiga kura na kuangalia kama jina lako lipo.
Ofisa wa pili anaangalia kama uko katika daftari ya wapiga kura. Akiona jina anaoanisha na picha na kisha mawakala wa vyama nao wanashuhudia. Baada ya hapo anasoma namba yako na niliona mawakala wa CUF, CCM na CHADEMA wananakili namba ya mpiga kura.
Baada ya hapo unaenda kwa msimamizi wa kituo, anakagua kadi yako na kisha anaisoma kwa sauti na mawakala wanahakiki. Kisha anakupa karatasi tatu. Ya blue nyuma - Urais, Nyeusi nyuma - Ubunge na nyeupe nyuma - Madiwani. Anazikunja na kisha kugonga mihuri miwili kwa nyuma katika kila karatasi. Kisha anakupatia.
Kisha unaenda katika sehemu iliyoandaliwa kupiga kura kuna pen hapo, unakunjua karatasi zako na kuweka vema kwa mgombea unayemtaka na kisha unazikunja.
Ukimaliza: Blue-Urais unatumbukukiza katika sanduku la kura za Rais, Black-sanduku la Ubunge na Nyeupe sanduku la mwadiwani.
Ukimaliza hapo kuna mdau wa NEC anakupaka wino katika kidole kidogo kisha unaondoka.
wakuu TBC is already biased... stinky television
mimi katika kituo nilichoenda huku Tegeta bahari beach utaratibu ulikuwa hivi:
- ukifika kituoni unapanga mstari mita kama 20 toka maafisa wanaoendesha upigishaji kura walipo.. wanaume mstari wao, wanawake mstari wao
- Afisa wa Polisi anaigiza wanawake 7 na wanaume 7..
- kwa kuwa kituo changu kilikuwa na sehemu 7 za kupigia, ukiingia either unaenda direct kwenye sehemu yako (kama ulifika kabla ya leo na kunakiri namba ya sehemu ya wewe kupigia --- naamanisha namba 1 mpaka 7) kama hujui unatakiwa uende sehemu majina yalipobandikwa na kutafuta jina lako na namba ya kituo.. KUMBUKA MAJINA YAMEPANGWA ALPHABETICALLY
- ukishajua NAMBA YA sehemu unayotakiwa kupigia kura, karani mwongozoji atakuelelekeza wapi pa kwenda
- ukifika sehemu ya kupiga mstari.. utapanga mstari.. kama utakuta kuna wengine mbele yako
- zamu yako ikifika unaenda kwa karani wa kwanza ambaye unampa kadi yako, anahakiki jina lako kwenye rejister, na kisha anataja kwa sauti ambapo mawakala wa vyama nimeona wanaandika kumbukumbu kwenye writing pad zao (ila mmoja nimeona kama anasinzia)..
- ukitoka hapo unaenda kwenye karani mwingine ambaye anaandika namba yako kwenye karatasi ya rejester (kipande kinachobaki kitabuni) na kisha kukuchania katarasi za kupigia kura
- then, unaenda kwenye kibanda cha kupigia kura
- ukishamaliza kupiga unatumbukiza kwenye box kwa kuzingatia rangi-- bluu ya raisi, nyeusi mbunge na nyeupe diwani
- ukishatumbukiza, karani mwingine anakuwekea wino mweusi
- baada ya hapo unaondoka kituoni
huo ndo utaratibu nilipitia... ila kasheshe moja nimeona kwa wasio jua kusoma.. nimeona kuna uwezekano mkubwa kudanganywa... kwa sababu wanaambiwa chagua mtu yeyote (minogoni mwa wapiga kura kama utakuwa hujaenda na mtu wa kukusaidia)
habari ndio hiyo!!
Baada ya briefing ya hapo juu, sasa naamia katika TV's kuwapa updates: ITV wako Live wanaohoji waandishi sehemu mbalimbali, , TBC pia wanarusha matangazo; , Channel 10 nao wako hewani na Star TV pia.