Dodoma: Hotuba ya Rais Jakaya Kikwete kuzindua Bunge la 10, Nov 2010

Basi Maalimu Sief ameruhusiwa kuingia ndani ya ukumbi wa bunge akiambatana na JK
 
kuna kichekesho hapa!
hoja ya kutengua sheria ili Seif aingie imepita ha hakuna aliyesema sio,
wabunge wote wamecheka maana walijua CHADEMa wangesema siyo...ha!ha!ha!ha!ha!
 
Kuna hoja kama wabunge wanaafiki eti makamu wa kwanza wa Rais apewe kibali cha kuingia kwa tamko na wengi wanasema ndiyo hivyo Mheshimiwa Seif Shariff Hamad amepewe ruhusa ya kuingia bungeni ifikapo 1630, kwa hiyo kikao cha mwanzo kimeahirishwa hadi muda huo ambapo kutakuwa na kikao cha pili cha JK kulihutubia bunge
 
Naibu spika ndo anatoka nje ya Ukumbi. Tutaungana hapo baadaye tena ifikapo kumi na nusu.
 
kuna kichekesho hapa!
hoja ya kutengua sheria ili Seif aingie imepita ha hakuna aliyesema sio,
wabunge wote wamecheka maana walijua CHADEMa wangesema siyo...ha!ha!ha!ha!ha!

Kwa nini chadema isipinge? au ndo 'muungano wa ccm na cuf' weshaukatia tamaa kuushinda?
 
Werema anatoa hoja ya bunge kutengua sheria ili makamu wa kwanza bara. Maalim seif aruhusiwe kuingia.
hapa ndi utibitisho kuwa CUF ni sehemu ya serikali ya muungano kwa hiyo si wapinzani
Naam, lete habari zaidi.
 
Hii yote ni tokana na kuwa Zhu hailewi anachokisema. You are short minded and myopic kama wewe mko wengi hapa JF
 
kinachoendelea hapa ni baadhi ya wabunge kuwapongeza hawav wageni waloapa leo
 
Wanabodi,
leo ndio namalizia ile live ya ufunguzi rasmi wa Bunge la 10 unaofanywa na Rais wa JMT, Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete.

Kama ni kufurika, leo ndio Dodoma imefurika. Wakuu wote wa vyombo vyote vya Umma wako Dodoma, hapa bungeni ndio hapafai kabisa maana hata makundi ya malobbyst wote wako usawa huu.

Leo ni hadi magari ya wanabalozi, baada tuu yakuwashusha, wamefukuziwa mbali wakajitafutie maeneo ya kuegesha kule nje ya ukumbi wa Bunge, ng'ambo ya barabara, eti ndani hapatoshi!.

Poa mkuu. Pia habari bungeni zinapatikana kupitia DONDOO ZA DOM, katika radio clouds fm, zikiletwa live na dada regina mwalekwa. Kama simu yako ina redio basi fungua clouds fm.



Huelewi na hutaelewa sijui unafanya nini humu. Kweli ni rais wa NEC hakuna anebisha lakini si rais wa Watanzania kwa maana wengi hawakumchagua.

Ushindi wa uchaguzi wa urais nchini tanzania ni wa SIMPLE MAJORITY, mshindi hahitaji kushinda kwa zaidi ya asilimia 80. Ushindi rahisi (SIMPLE MAJORITY) wa hata asilimia chini ya 50 unaweza kumpa mgombea ushindi. Hivyo huyo Jakaya Mrisho Kikwete ndiye rais kwa kutumia taratibu hizo za SIMPLE MAJORITY, kwa hiyo yee ni rais wa jamhuri ya muungano wa tanzania, na wewe ukiwemo.
Kwa bahati mbaya katika fomu mbalimbali tunazozijaza huwa hakuna nafasi ya kujaza rais wako, kama ingekuwepo wee ungejaza rais unaemtaka wewe alafu uone kama hilo ombi lako mfano la kuomba viza kama lingekubaliwa
 
seifu mzee wa sawa sawa?

huyu kazi yake itakuwa ni kufungua ofisi mpya na kuhudhuria hafla kama mgen rasm
hana makali kule zenji
 
Naona Six anamnong'oneza kitu Mbowe.
mbowe ni kama anasema "all is right" nimeconsider body langage
 
msafara wa Seif ndo unaingia ukumbini, pamoja na makamu wa pili balozi seif Iddi
 
Back
Top Bottom