LIVE bungeni: Waziri wa fedha anasoma bajeti ya serikali 2012/2013

thatha

JF-Expert Member
Apr 29, 2011
15,340
1,566
Ni mh. Dr Mgimwa.

Anaendelea kushusha nondo kuhusu tulikotoka,tulipo na wapi tunaelekea kama nchi katika maendeleo ya kiuchumi.ameainisha ukuaji wa uchumi,mafanikio na changamoto mbalimbali zinazoikabili Tanzania ikiwa ni pamoja na deni la Taifa.

Tuendelee kufuatilia.
 
malengo ya bajeti 2013

kukuza kipato
kuimarisha miundombinu

kuthibiti mfumko wa bei
kukuza mikopo kwa sekta binafsi
kuimarisha ubia kati ya sekta binafsi

mikopo
utawala bora
 
kupunguza misamaha ya kodi,kupitia upya mfumo wa ukusanyaji kodi ili kuongeza mapato
 
Hamna chochote hapo bora niendelee kusukuma tursker nisije nikapata stress nisumbiri ya kambi ya upinzani niisikilize kwa umakini
 
Hapa nafuatilia hii bajeti kwa makini sana, lakini naona ni yale yale ya miaka iliyopita. Sioni kama kuna kitu kigeni hapo...!
 
juice kutoka nje zitatozwa kwa tsh85 kwa lita lakini kwa zinazozalishwa ni tsh8 kwa lita
 
Nimekurupuka kutoka kwenye kikao kuwahi updates humu naona blah blah tu! imekuwaje leo JF tumeshindwa kurusha live hiyo hotuba?
 
Haya majamaa yanakera sana kila mwaka yanatupandishia bei ya sigara lol!

Magari sasa tutaruhusiwa kuweka plate namba zetu miaka mitatu mil 5!
 
Sio kweli, hicho ni kiasi cha kuanzia kutozwa kodi ktk mishahara
 
Back
Top Bottom