Live Bungeni: Mbowe kwa niaba ya kambi ya upinzani wamekubali yaishe

Hilo la kurudishwa tena bungeni kwa marekebisho ya katiba hiyo, inaonesha moja kwa moja kuwa CDM ni chama imara ambacho wabunge wanajali maslahi ya taifa!! Viva CHADEMA
 
wachambuzi wa mambo ya siasa hebu nijuzeni "CCM ina marupurupu gani kungangania kuwatumia Ma DC kwenye kura za maoni?" wakati wote tunajua Ma DC ndiyo makada numberi one wa chama cha Mapinduzi wilayani na hoa hao ndiyo huwa wanakula dili kuvuruga kampeni za vyama vya upinzani. Mama Kilango hebu tufafanulie utakosa maslahi gani kama tutawatumia wakurungezi wa wilaya badala ya hawa ma DC wako? , Je wakurungezi hawana Elimu na Uzoefu wa kutosha wa kushughulikia zoezi zima la upokeaji maoni ya wananchi? maana jana uliongea hadi unatoa machozi kwamba LAZIMA ma DC ndio wasimamie hili.

naomba ufafanuzi tafadhali labda mimi sijaipata mantiki ya CCM kwa ujumla.
 
saivi ni kujipanga tu na kuhakikisha hawa ma DC wanasimamia maslai ya taifa na sio chama chao cha kijani, wabunge wa CCM ndo tatizo kwani wingi wao na udhaifu wao wa kudadavua mambo ya msingi ndio yanatupeleka huku kwenye kipengele kama hiki ambacho kinaweza kutia dosari mchakato wa katiba
 
Mbowe amezungumza kwa busara sana sana. Na amekubali wakuu wa wilaya waingie ndani ya marekebisho. Tunashukuru sana Mbowe kwa uzalendo wako na kukubali compromise sio kubisha kila kitu

Nani aliyekuwa anabisha?
Mapendekezo ya Serikali - ambayo ki-mantiki ni mapendekezo ya CHADEMA yanasema DEAD aingie, CCM wakabisha, wakakataa mapendekezo hayo........

Sasa wewe unaona hapo nani amepinga?
Au wakisema akina Kilango ndo inakuwa sheria, na yeyote anyesema tofauti anakuwa mpingaji?

busara zako zipo kwenye kisigino wewe!!!
 
Kwa nini tunaingiza siasa katika suala hili la katiba? tuelewe kwamba hawa watu ma DC na ma DED ni watumishi wa serikali.

MDC ni makada wa magasmba tena wengine walikataliwa na magamba wenzao kwenye kura za maoni. Mfano kiherehere Nape.Achilia mbali waliokataliwa na wananchi kwenye uchaguzi mkuu.:amen:
 
Kwa nini tunaingiza siasa katika suala hili la katiba? tuelewe kwamba hawa watu ma DC na ma DED ni watumishi wa serikali.

DC ni kada wa chama hilo liko wazi.. wala huitaji elimu ya chekechea kuona lengo la Anne kilango malecela
 
Politicaly, cdm wc mr. Mbowe wame2mia zaid ya busara ndg zng!Cha mcing 2subir mchakato utakwendaje na je uta2letea katiba bora au bora katiba!Hapo 2tafanya tathmin mwisho kama DCS au DEDS wameathir +vely/-vely pgm nzma!vngnevo ITAWACOST at end!
 
Nimemkumbuka Wenje jana na story Wabunge wa CCM kuwa watermellon. Ndani nyekundu, nje green!!!!
 
hivi ni kweli mbowe amewasahau wakuu wa wilaya au anafanyeje sasa maana hawa watu ni wavurugaji wakubwa sana kwanza katiba mpya ilikuwa isiwatambue sasa utawatoaje maana huwezi pendekeza wasitambuliwe huku wakiwapale

Mkuu muda wa kuwa mwoga umekwisha hao tutawachana live hata kama watakuwepo,hao ni makada wa CCM tu hilo wala lisikupe hofu tutakula nao sahani moja,maadamu kiongozi mkuu wa upinzani bungeni amkubali yaishe na akatoa angalizo,basi wacha hao Ma DC-CCM wawemo kama watu pia wanaoweza kufikiwa na tume ili waandae watu kwa ajili ya kutoa maoni,hivyo tusijiogopeshe kabla,tutawachana live wajue kabisa hatuwataki tena
 
Kwa nini tunaingiza siasa katika suala hili la katiba? tuelewe kwamba hawa watu ma DC na ma DED ni watumishi wa serikali.

VGL, Katiba ndio siasa yenyewe. Tunaongozwa na katiba; tutachagua viongozi kwa Katiba; tutatawaliwa kwa Katiba; tutatumia/tutasimamia raslimali zetu kwa Katiba; nk. Hivyo hakuna namna yoyote utakapoitoa siasa katika suala na KATIBA na mchakato wake.
 
Mh hebu weka wazi amekubali nini sasa, kwamba katiba ibakwe na CCM au?

Mimi nafikiri chadema imepigana kwa nafasi yake kama chama, kazi ni kwenu watanzania kusimamia kile mnachokitaka bila woga: nikweli MaDC hawa ni wabakaji wakubwa wa Demokrasia na ndo wanaoogoza kwa kuwatisha wananchi huko wilayani, wanan nguvu kuliko mbunge kwenye jimbo! Ila Chadema hawawezi kutufanyia kila kitu, pale wanapopungua sisi wananchi tuatakiwa ku-cover! Sisi tuwasubiri hao MaDC mtaani wakileta mambo yao tunawaanzishia hukohuko! Kitendo cha CDM kuwaamini wakurugenzi thidi ya MaDC tayari ni devide and rule strategy!
 
CDM kama chama kimemaliza kazi yake imebaki kazi yetu sisi wananchi kuelimishana wenyewe mapungufu yaliyopo ndani ya katiba iliyopo na ynatuathiri vipi. Tukishindwa kutekeleza wajibu huo tutakuwa hakuna tena mwingine wa kumlilia.
 
wachambuzi wa mambo ya siasa hebu nijuzeni "CCM ina marupurupu gani kungangania kuwatumia Ma DC kwenye kura za maoni?" wakati wote tunajua Ma DC ndiyo makada numberi one wa chama cha Mapinduzi wilayani na hoa hao ndiyo huwa wanakula dili kuvuruga kampeni za vyama vya upinzani. Mama Kilango hebu tufafanulie utakosa maslahi gani kama tutawatumia wakurungezi wa wilaya badala ya hawa ma DC wako? , Je wakurungezi hawana Elimu na Uzoefu wa kutosha wa kushughulikia zoezi zima la upokeaji maoni ya wananchi? maana jana uliongea hadi unatoa machozi kwamba LAZIMA ma DC ndio wasimamie hili.

naomba ufafanuzi tafadhali labda mimi sijaipata mantiki ya CCM kwa ujumla.

Wew kwa akili yako unafikiri CCM watakubali kung'oka kirahisi mdarakani, watakufa wakipiga mateke, hivyo sisi wachinjaji wao ni lazima tuhakikishe kuwa tunafanya kazi ya ziadq bila kuchoka.
 
Nani aliyekuwa anabisha?
Mapendekezo ya Serikali - ambayo ki-mantiki ni mapendekezo ya CHADEMA yanasema DEAD aingie, CCM wakabisha, wakakataa mapendekezo hayo........

Sasa wewe unaona hapo nani amepinga?
Au wakisema akina Kilango ndo inakuwa sheria, na yeyote anyesema tofauti anakuwa mpingaji?

busara zako zipo kwenye kisigino wewe!!!

huyu ni nani tena ??
 
Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom