Listi ya wabunge MATAJIRI Tanzania

Game Theory

Platinum Member
Sep 5, 2006
8,545
835
Naaminsha wote wa Chama Tawala na Upinzani.

WHATS YOUR TOP 20?

1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
 
Kwa mishahara na marupurupu ya wabunge sidhani kama kuna mbunge maskini. Mafao ya ubunge yana tosha kumfanya mtu yoyote awe tajiri kwa standards za nyumbani bila hata kuiba. SO with that said, kila mbunge ni tajiri. The important question is, nani mwenye mali zisizo halali?
 
Last edited:
Hivi mnajua Ndesamburo ana nyumba zaidi ya 13 pale MayFair na South Kensington, London?
 
Mnamsahau vipi Aloyce Kimaro ambaye shamba lake lilivamiwa na wanakijiji wa sing'isi? mbona hamumsemi cigwiyemisi aka tingatinga?
 
Game Theory,
Anavyofoji hizo risiti za matibabu ndivyo mahitaji yanayoongezeka. Nothing will stop him. It's simply like the world of the dead, there is always enough room for more! Huoni kila kukicha mara mishahara, mara tununue mitambo ya DOWANS, na kama hiyo haitoshi, sasa hata shujaa wetu Slaa naye anasema njia bora ya kugawana keki ya taifa ni kupitia hiyo mifuko ya maendeleo ya jimbo. Kuna mtu wa kuaminiwa humo?
 
1. NIMROD MKONO ( Pesa za BoT)
2. EDWARD LOWASSA ( Ufisadi)
3. ROSTAM AZIZ (Dili za kifisadi)
 
Hivi mnajua Ndesamburo ana nyumba zaidi ya 13 pale MayFair na South Kensington, London?
kaaanza long time ago huyo ndesa, kwanza kawa maskini alipoingia ubunge, the guy ni entrepreneur wa long, hata hela za bunge huwa ametoa msaada ikiwa ni pamoja na gari yake ya ubunge
 
Tunarudi palepale katika kujadili watu ,kwenye private zao.Huku ni kupindishwa kwa mawazo na badala ya kujadili nini kimefanywa na CCM na je inahitajika au haihitajiki tunaenda kuvamia watu ,hivi si watatuacha hapahapa tukibishana ?
 
Ni kweli wabunge wote ni matajiri lakini jamaa anataka list ya wanaoongoza kwa wingi wa mali hasa zilizipatikana kiujanjaujanja.
 
Ndesa tunamfahamu kama mtu aliehenya sana kufika hapo alipo. Kuna Chama kimoja wanaomba kila siku awe kwao ili wafaidi mapesa yake.
 
Tunarudi palepale katika kujadili watu ,kwenye private zao.Huku ni kupindishwa kwa mawazo na badala ya kujadili nini kimefanywa na CCM na je inahitajika au haihitajiki tunaenda kuvamia watu ,hivi si watatuacha hapahapa tukibishana ?


As kiongozi nadhani wananchi wana right ya kujua mali zao na wamezipataje so ukisema ulifumbie macho hilo ndiyo tunabakia kuwa masikini.Tatizo letu sisi waTz tunapenda sana kulalamika pembeni kufanya matendo ni waoga sana.

Nadhani kuna shetani ameingia maana ukiangalia utawala wa Nyerere,hakuna kiongozi aliyekuwa na mali kama walizokuwazo sasa hivi.
 
Sasa kama uongozi wa Nyerere kulikuwa hakuna kiongozi tajiri au mwenye mali basi hata raia nao walikuwa wamekondeana.

Hivi sasa raia wengi wanamiliki nyumba nyingi tu na pia tunakaribia kila nyumba kuwepo na gari ,na uwezo wa wananchi pia unaoenekana kuongezeka ,karibu kila mtu hivi sasa anamiliki simu ya mkononi na karibu wanafunzi na watoto walio chini ya miaka kumi na nne nao watamiliki simu za mukononi ,hivyo kuwajadili wabunge ambao mishahara yao ni minono na inajulikana itakuwa hamuwatendei haki ,maana japo wana mishahara minono inategemea akili ya mtu inavyofanya kazi na uwezo wa kutumia na kupanga matumizi ya hela anayoipata. Au kwa msemo wa kibiashara vipi ataekeza hela anayopata ili izalishe hela zaidi ,ni uwekezaji tu ndio unaoweza kumuinua mtu yeyote yule ,hebu fuatilia story za mabilionea uone ,walivyoanza na mtaji ambao ukipewa wewe haumalizi mwezi hela yote umetafuna. Watu wanajua kufunga mkaja ,msione vinaelea jamani ,huu ni msemo wetu katika lugha.
 
1. Rostam aziz
2. Lowasa
3. Mramba
4. Ndesamburo
5. Mkono
6. Chenge
7. Diallo
8. Mzindakaya
9. Rwakatare
10. Dewji
 
1. mo dewji - mkwepa kodi ($25m tax fraud ya edible oil). akitoa $3m kwenye kampeni ya ccm anabakiwa na $22m na kuhakikishiwa ulinzi na kuendelea kukwepa kodi...
hayo ndiyo mambo ya banananananan republic......
 
Back
Top Bottom