jmushi1
Platinum Member
- Nov 2, 2007
- 24,989
- 22,521
Unapokuwa kwenye mahojiano, facts kama za miaka na mahali zinaweza kukutoka. Na hicho ni kitu kinachokubalika iwapo tu miaka na mahali sio agenda za mahojiano yenyewe bali ni kichapizo tu.
Mnategemea Mzee Malecela akiwa kwenye mahojiano, akumbuke mahali na mwaka kwa usahii kabisa kama vile anakwenda kwenye mtihani wa historia wa darasa la nne.
Nyie watu wazima mnashindwa kujadili theme ya kile alichosema na mnabaki kubishana kwenye miaka. Angesema mwaka 1990, mantiki ingebaki hilehile.
Mkuu hapa JF watu wanauliza kila kitu,every little thing,si kwamba nasapoti hilo,lakini kwani viongozi nao hawajianadai? Ama wanafanya mazoea wakidhani Tanzania hii ni ile ile ya zamani? Mkuu kiongozi kama Dk Malecela ni lazima ajiandae na facts kutokana na heshma yake,watu wanafuatilia kwa makini maneno yao na si siasa kama za zamani...Historia inaandikwa kutokana na maneno yao,sasa wasipotukumbusha wao waliokuwa karibu na matukio muhimu nani mwingine atafanya hivyo...Ni Mh Mzee mwenye wasaidizi na ni vyema akacheck facts,inawezekana pia kuna mifano ya hapa na pale nk,ambayo anaitumia kama mifano rahisi,lakini ni muhimu kuwa makini...Amezungukwa na watu wenye uwezo wa kumsaidia,binafsi naona amnsaidie Mama Kilango maana yeye huja na facts za nguvu na huwa ana uhakika na anachosema,at least mara nyingi nimeshuhudia hilo.