Wakuu, Malecela anazungumza kama makamu mwenyekiti wa CCM, ni muhimu sisi tuifahamu lugha yake kwanza...Huyu sii kiongozi wa serikali na hana nguvu huko..
Pili, alichosema ni ukweli mtupu.. kwani kama kweli hawa jamaa wanaotaka kumeguka CCM watoke! hizi habari za kutuzuga hata sisai wananchi hatufahamu wanachosimamia ni kutuzidishia hasira tu.. Waondoke CCM, wananchi tujue moja kama ni hao Mafisadi wanatishia kuondoka waondoke.. na kama kuna wale wanaojiona wasafi na CCM sio mahala pao - waondoke...
Jamani ndilo sisi wananchi tunachotaka kuona na tunatarajia mtu yeyote mwenye kujali maslahi ya Taifa atakuwa amechukua maamuzi ya maana isipokuwa wale wanaotaka kutubeza..sio kuitisha vikao kila siku kujitangaza wajkati bado wamo ndani ya chungu wakipikwa..
Kuhani, kwa hili Mzee Malecela yuko sahihi. Mwalimu aling'atuka mara mbili, katika nafasi mbili tofauti. Mwaka 1985 aling'atuka na kuachia u-rais wa nchi, lakini aliendelea kubaki na kofia ya Mwenyekiti wa Chama. Mwaka 1992 aling'atuka Uenyekiti wa Chama (CCM). Hayo maneno aliyasema wakati anang'atuka Uenyekiti.
Ambacho nashindwa kumuelewa yeye na viongozi wenye hulka kama yake, ni kwa nini wanadhani kuwa CCM hii ya sasa ni "madhubuti"? Kwa kuwa tu wanashinda chaguzi haina maana kuwa ni madhubuti! CCM baada ya kuwa kwenye siasa/utawala kwa miaka takribani 55 (1954 - 2009), bado kina wanachama milioni 4 tu na kinasumbuliwa na vyama vilivyo na uhai usiozidi miaka 15! Huu ni mpambano wa mtu mwenye malaria vs mwenye kipindupindu, hakuna madhubuti hapo.
Mkuu Kiungani,
Mambo kama haya ndivyo yanavyotakiwa. Unaona mwenzako amekosea, unamweka sawa kwa facts ulizonazo. Na sisi wengine tusiojua tunaelimika.
Amandla............
Kuhani, kwa hili Mzee Malecela yuko sahihi. Mwalimu aling'atuka mara mbili, katika nafasi mbili tofauti. Mwaka 1985 aling'atuka na kuachia u-rais wa nchi, lakini aliendelea kubaki na kofia ya Mwenyekiti wa Chama. Mwaka 1992 aling'atuka Uenyekiti wa Chama (CCM). Hayo maneno aliyasema wakati anang'atuka Uenyekiti.
Nakuunga mkono FM. Lakini sahihisho dogo kutokana na kumbukumbu zangu Nyerere aling'atuka CCM mwaka 1990. Wakati wanapitisha vyama vingi mwaka 1992 Mwalimu Nyerere alialikwa tu. Tena katika ushauri wake kwa CCM ilikuwa lazima wakubali mfumo wa vyama vingi. Ni Malecela huyo huyo aliyesema kwamba wale watakaohama CCM 'they be left out in cold'
Sasa nani yuko sahihi? Kuhani au Kiungani?
Sijaona mahali ambapo Kuhani anasema maneno ya "mimi nang'atuka" yalitolewa lini?!