Mlalahoi
JF-Expert Member
- Aug 31, 2006
- 2,182
- 883
Hata sielewi implication yake...backlash, backfire, hatua madhubuti zaidi; au itaishia kuwa soga tu.
Nadhani reactions za hao waliotajwa zitakuwa za pupa na za haraka mno.Slaa atatuhumiwa kuwadhalilisha viongozi wa kitaifa "kwa kutoa tuhuma za uongo zenye lengo la kuvuruga amani na utulivu.
"Nakubaliana na idea ya Dr Slaa kwamba for the time wao kwenda mahakamani ni sawa na kuwapa muda hao wala rushwa kwa vile kesi zinazohusu vigogo huwa zinachukua muda mrefu sana,na wakati huohuo vigogo hao watakuwa wanafanya kila wawezalo kufuta ushahidi.
Tusisahau pia kuwa majaji wetu ni wateuliwa wa Rais....Backfiring?Well,watajwa watafanya usanii kumgeuzia kibao Dr Slaa ili ionekane hiyo ishu imemgeukia yeye.Backlash?That's expected.
Hawa wala rushwa huwa hawapendi kubughudhiwa wakati wanakula keki ya taifa.Hatua madhubuti?Well,that's up to the public to work on what's been revealed to them.
Soga tu?Again,hili jeshi dogo la akina Slaa linaweza kumprove Bob Marley right aliposema shoka dogo linaweza kuangusha mti mkubwa,lakini for that to happen,inabidi kuwe na support ya kutosha kutoka kwa wananchi wenye uchungu na nchi yao.