Lissu kufunga ushahidi mchana huu-maendeleo ya kesi tangu jana.

Isango

R I P
Jul 23, 2008
295
450
Tangu jana mchana hatukutuma maelezo mengi katika JF kulikuwa na tatizo la mtandao. Naomba kutumia fursa hii kuwatumia maelezo ya tangu jana mchana, hadi sasa ambapo shahidi wa mwisho wa Tundu Lissu anafunga kwa kufanyiwa cross examination na wakili wa walalamikaji.

SHAHIDI WA TATU: SHABANI HAMISI LYIMU.
PINGAMIZI TOKA KWA WALALAMIKAJI: Shahidi huwa anahudhuria mahakamani kila siku, lakini pia sitegemei kama Tundu Lissu anaruhusiwa kumwongoza shahidi wake kama wakili.
LISSU ANAJIBU: kwa ufahamu wangu wa sheria sijawahi kuona kuwa shahidi wa utetezi haruhusiwi kuingia mahakamani wakati walalamikaji wanatoa ushahidi. Wanaokatazwa ni wale ambao katika kuwepo kwao hasa kwa upande wa walalamikaji.
Cha pili; kuhusu kama ninaweza kumwongoza shahidi wangu au la, hiyo ni haki ya pande zinazobishania jambo, sio haki ya mawakili tu. Wakili Wasonga hajajielekeza vizuri katika sheria, hivyo hajaielekeza vizuri mahakama yako kisheria. Kifungu 146(1) cha sheria ya ushahidi, ni upande uliomleta ndio unaweza kumhoji sio wakili wao. Hiyo ni haki ya msingi. Naomba pingamizi hizo mbili uzikatae na tuendelee.
JAJI: bwana Lyimu simama, je ni kweli ulihudhuria ndiyo, mara ya mwisho lini?
WP: Juzi, jana sikuwepo.
WAKILI WA WALALAMIKAJI: Ulipotoa kauli kuwa mashahidi wasiwepo hukusema kuwa ni wa walalamikaji tu.
JAJI: defence wasingeweza kujua nini kitasemwa na nyie ili kuestablish case yao, pingamizi nalikataa, mashahidi wa utetezi wasingejua ninyi mnasema nini. Ningekuwa na mawazo tofauti kama walikuwepo jana. Hata hoja ya pili ni haki ya kila mtu kumhoji shahidi hata kama yeye sio wakili. Pingamizi nimelitupitia mbali
T/L: Unaishi wapi na unafanya kazi gani?
WP: Nakaa kijiji cha Ntunduu, kata ya Kinyeto, Wilaya ya Singida vijijini, na ni Mkulima.
T/L: mwambie jaji kama una nafasi yeyote ya kisiasa.
WP:Nafasi niliyo nayo ni katibu wa CHADEMA Wilaya ya Singida vijijini.
T/L. Tangu Lini?
WP: August 2009.
T/L. Umewahi kushika Nyadhifa zipi katika Chama hicho?
WP: mwaka 1995, niliwahi kuwa katibu Mwenezi wa CHADEMA, (Singida vijijini), mwaka 2002, nilikuwa katibu wa Mkoa wa CHADEMA – Singida., nikiwa pia mjumbe wa baraza kuu la Chadema Taifa
T/L Ukatibu huu uliushika kwa miaka mingapi?
WP: Miaka 10
T/L: Shahidi tuna kesi ya uchaguzi, waweza kumweleza jaji uzoefu wako kuhusu mambo ya Uchaguzi?
WP: Nilianza mwaka 1995, uchaguzi wa Vyama vingi na wakati nikiwa kama katibu mwenezi., mwaka 2000 nilikuwa katibu nako nilishiriki, na 2005 vile vile nilishiriki, na uchaguzi mkuu wa mwaka 2010 nilikuwa katibu wa Wilaya
T/L: Umewahi kushiriki kama mgombea au mpiga kura.
WP: nilishiriki kama mpiga kura, lakini pia nimeshiriki kama mgombea wa Udiwani. Mwaka 1995, 2000, 2005, na 2010
T/L. Kwa kumbukumbu zako uchaguzi wa mwaka 2010 ulifanyika lini?
WP: tarehe 31/10/2010
T/L. Mwambie jaji, kwa nafasi yako kama katibu wa Wilaya wa CHADEMA ulikuwa na nafasi gani katika uchaguzi huo?
WP: Niliandaa wagombea wa Udiwani kupitia Chama changu, wabunge wanaotokana na Chama changu katika Majimbo matatu yaliyopo katika wilaya yangu.
T/L: kazi zingine?
WP:Kuratibu maelekezo mengine kutoka kwa msimamizi wa Uchaguzi, na maelekezo mengine toka ngazi ya Juu yanayohusiana na Chama.
T/L. Fafanua, unapotaja maelekezo yamsimamizi wa Uchaguzi una maana gani?
WP: Ni hatua zote za awali za uchaguzi, na maelekezo yote yanayohitajika, kuanzia kupata orodha ya wapiga kura waliojiandikisha katika Jimbo letu,
T/L. Mweleze jaji, utaratibu wa mawasiliano kati ya ofis yako na Msimamizi wa uchaguzi yalifanyikaje?
WP: Msimamizi wa Uchaguzi aliteua ofisa mmoja wa kusambaza barua, na kwa kuwa sisi hatukuwa na ofisi basi walikuwa wanapeleka wao kwa gari yao mpaka Nyumbani kwa Mwenyekiti.
T/L. Je nyie mkitaka kuandika barua kwa msimamizi mlikuwa mnafuata utaratibu gani?
WP: Tulipeleka wenyewe kwa njia ya Dispatch
T/L: naomba uangalie nyaraka hizi. Tuambie, hiyo unayoangalia ni barua ya nani?
WP. Barua hii inayohusu orodha ya mawakala ni yangu na nilipeleka kwa msimamizi wa uchaguzi.
T/L: Nini kilikufanya uandike barua hizi?
WP: Mheshimiwa jaji, nilitakiwa kufanya vile na msimamisi wa Uchaguzi siku saba, kabla ya uchaguzi.
T/L. Hebu mweleze jaji kiwango chako cha Elimu.
WP: Darasa la saba.
T/L. Umewahi kuhudhuria kozi yeyote ya mambo ya sheria?
WP: Hapana
T/L. Hiyo barua ya Chadema uliyosoma, imetaja vifungu vya sheria, mweleze jaji, hayo uliyatoa wapi?
WP: Nilipata toka kwa Mheshimiwa Tundu Lissu, aliyekuwa Mgombea wa Singida mashariki, aliniomba kuwa katika mawasiliano ya uchaguzi kwa kuwa mambo mengi ni ya kisheria, hivyo kila nilipopata barua niliwasiliana na Lissu kabla ya kuandika.
T/L. Kwenye orodha umetaja kuwa kuna wakala wa kituo na wakala mbadala, hayo uliyapata wapi?
WP: Tuliyapata toka kwa msimamizi wa Uchaguzi, kwani mawakala wote walipaswa kuapa.
T/L: Kwa vile umesema umeshiriki katika chaguzi nyingi je inaruhusiwa kuwa na wakala mbadala?
WP: Kwa ufahamu wangu, kuwa na wakala mbadala ni sahihi.
T/L, Hiyo barua imechapwa, wewe unayeda Singida mjini.
WP: Nilichapa katika stationary, na barua zangu zote huwa nachapa hapo
T/L. Mlikuwa na mawakala wangapi katika Jimbo la Singida mashariki?
WP. Tulikuwa na mawakala 124 wa vituo, na 124 mawakala mbadala.
T/L. Mweleze jaji, je unamfahamu aliyeandika barua hiyo ya CUF?
WP> Ni Seleman Ntandu – Katibu wa CUF singida vijijini.
T/L. Unafahamu huyu uliyemtaja?
WP: Ndio, tumewahi kuwa na ushirikiano wa kisiasa na vyama vyote kasoro CCM, kiwilaya na kimkoa, hivyo ninamfahamu
T/L. Umefanya kazi naye kwa muda gani?, na ni kazi gani maana jaji hakuwa pamoja na nyie?
WP:Kuhamasisha mikutano ya hadhara vijijini
T/ L. Ilikuwaje barua zenu zikafanana?
WP: Alipoona barua yetu, naye aliomba ili akaandike nayekwa Mkurugenzi, na nilimwelekeza pale nilipochapisha kaenda kuchapa ile. Na wengine waliomba ushauri wakaenda kuandika.
T/L. Nimeshtakiwa kuwa barua hizo zote ulizonazo niliziandika mimi, mweleze jaji unajua nini?
WP: Si kweli kwamba wewe umeaziandika
T/L. Wakati mnaziandika mimi nilikuwepo?
WP. Hapana, haukuwepo
T/L :Inadaiwa kuwa kwa sababu ya barua hizo, nilikuwa na mawakala 1240, 620 ndani ya vituo na 620 nje ya vituo je ni kweli?
WP: utaratibu tulioutumia, nilioorodhesha kwenye barua ndio uliotumika.
T/L. Mwambie jaji, je mawakal wa Chama chako walikuwa wa CHAMA chako tu? Au ulitumia utaratibu gani kuwapata?
WP: Vigezo tulivyotumia ni kuwaomba makatibu wetu wa kata watuletee majina ya wanachama, na wale wasio wanachama, ambao wanatuunga mkono na tuliothibitisha bila shaka kuwa ni waaminifu, wawe wanajua kusoma na kuandika.
T/L. Kuna ushahidi unasema kuwa mimi niliwafunza mawakala wote isipokuwa wa CCM wewe unajua utaratibu wa mafunzo ya mawakala wenu ulikuwaje?
WP: kuchukua wanaojua kusoma na kuandika, aliye muadilifu, ili awe wakla
T/L. Unafahamu kama wote waliohudhuria mafunzo kama wote walikuwa wanachama wa chama chako
WP: SIWEZI kuwafahamu.
T/L. Hivi wote waliohudhiria mafunzo hayo wote walipata nafasi ya Uwakala?
WP: Hapana sio wote.
T/L. Wale ambao ninyi hamkuwachukua nini walienda Chama gani?
WP; SIJUI.
T/L. Ninatuhumiwa kuwa niliwahonga mawakala wa vyama vingine isipokuwa CCM kwa kulipia Chakula chao, na usafiri wao. Je utaratibu ulikuwaje?
WP: Kwanza sio kweli. Nilipokea pesa toka makao makuu, kwa ajili ya kusaidia chakula cha mawakala siku ya uchaguzi.
T/L; Mweleze jaji ulizitumiaje?
WP: Nilizituma kwa viongozi wetu wa kata, siku tarehe 29/10/2010 walipokuwepo kwenye maeneo ya kula viapo, Ikungi na Mungaa, na kutoa maelekezo wanunue juice, maji na biskuti. Vyote vina gharama ya shilingi 800/= tukatumia 198,400/-
T/L. Unawafahamu waliogawiwa hivyo vitu?
WP: kwa ufahamu wangu najua waliogawia ni mawakala wa chama change.
T/L: Kuna ushahidi umetolewa kuwa hayo maji, juice na biskuti viligawiwa pia kwa mawakala wa Vyama vingine, wewe unazungumziaje?
WP: Bajeti yenyewe ni ndogo, ina upungufu mkubwa, hiyo haiwezekani. Zilibaki 1600/- tu.
T/L:niambie kama unakumbukumbu au unafahamu juu ya sherehe iliyofanyika makiungu?
WP:nafahaumu
T/L:nambiwa kuwa kwenye sherhe hiyo nilikiri kuwa niliwapa vinywaji na biskuti?
WP:Tuliwapa hivo vitu mawakala wa chadema tu
T/L:sema kama tuliwapa mawakala wa vyama vingine?
WP; tuliwapa ni uwingi wa mawakala wa chadema
T/L;Ni nani aliyefungua sherehe za makiungu
WP:aliyefungua ni mwenyekiti wa kijiji cha makiungu
T/L;niambie kama ulikuwa unamfahamu paskali halu na shabani selema
WP:Nimewafahamia mahakamani
T/L:je, unamfahamu bwana swai ambaye ni katibu tarafa ya mungaa na ambaye alipiga picha za video?
WP: ndiyo namfahamu
T/L:tangu lini?
WP: namfamu tangu mwaka 2008 alipokuwa katibu tarafa sepuka
T/L: je siku ya sherehe ulimwona?
WP:ndiyo nilimwona kwa muda mfupi na baadaye alitoweka
T/L:kulikuwa na chakula na vinywaji je, alikuwepo?
WP:La sikumwona wakwti wa chakula na vinywaji na hata wakati wa hotuba hakuwepo

MASWALI TOKA KWA WAKILI WA WALALAMIKAJI: cross examination:
WAKILI:Unakaa kijiji gani?
WP: Ntunduu, 14 km toka mjini Singida.
WAKILI: Ulisema kuwa mlikuwa na ushirikiano wa Vyama ya Upinzaji je ilikuwa ni ngazi ipi?
WP: WILAYA NA MKOA.
WAKILI: Mwambie jaji, Uliandika barua kwa maelekezo ya nani?
WP: Kwa maelekezo ya Tundu Lissu.
Wakili: barua ulizoshuhudia zikiandikwa ni zipi na zipi?
WP: Nilishuhudia ya CHADEMA NA CUF, Vyama vingine sijui.
WAKILI: Kawaida barua huwa zinaandikwa na nani?
WP: Na makatibu.
WAKILI: Fedha mlitoa kiasi gani toka makao makuu, zilitumwa na nani?
WP: Zilitumwa na Dady Igogo, kwa niaba ya Antony Komu
WAKILI: Je mnarisiti yeyote pale kwa jaji, kuonyesha kuwa mliwahi kupewa pesa?
WP: hakuna
WAKILI: Una nyaraka yeyote sasa kuonyesha kuwa mlitumiwa pesa?
WP: Sina.
WAKILI: Wewe ndo ulitoa maelekezo ili juice, maji na soda vinunuliwe, je vilinunuliwa wapi?
WP: Hapana
WAKILI: Ni wewe ndo ulivinunua?
WP: hapana,
RE: EXAMINATION
TUNDU LISSU; Umeulizwa kama una risiti ya pesa ulizotumiwa au benk statement, mwambie JAJI, Pesa ulitumiwa kwa njia gani?
Wp: NILITUMIWA KWA M-PESA

SHAHIDI WA NNE:
SELEMANI MOHAMED NTANDU;
T/L: Nitakuongoza kwenye ushahidi, uzungumze kwa makini,kwa sauti tena taratibu.
T/L: Mweleze Jaji, wewe una nafasi gani kisiasa katika wilaya,
WP: Mimi ni katibu wa wilaya
T/L: Tangu lini
WP: 2008, JULY.
T/L. Kabla ya hapo ulikuwa una kazi gani?
WP: Nilikuwa mtunza hazina wa wilaya, na nilikuwa mjumbe wa kamati tendaji CUF,
T/L. Mweleze jaji, kama unanifahamu mimi, na umenifahamu kwa muda gani?
WP: Nilimfahamu mwaka 2000 Dar, kwenye sherehe ya vijana Fulani walikuwa namaliza chuo kikuu, wakati huo Lissu alikuwa anatoka marekani na alikuwa mgeni mualikwa katika hiyo sherehe, pia namfahamu kwa kuwa tulifanya naye kazi ya siasa, Vyama vya CHADEMA, CUF, NCCR NA TLP Vilishirikiana kisiasa mwaka 2008, wilaya ya Singida vijijini.
T/L. Hebu tuzungumzie suala la Uchaguzi 2010.
Wp; Mimi nilishiriki kama mgombea wa Udiwani, kata ya Ikungi. Lakini pia kama katibu wa Wilaya nilikuwa mtendaji wa shughuli zote za chama
T/L: Mweleze jaji, kama Chama chako kilikuwa na wagombea wengine
WP. Tulikuwa na wagombea 6
T/L. Mwelezi jaji, wewe ulipokuwa mgombea wa Udiwani kata ya Ikungi, ulitembelea vituo?
WP: Ndio
T/L. Mwambie jaji, unamfahamu Husen Mwangia,
WP. Nafahamu kama mwislamu mwenzangu, tunasali pamoja, na tumefanya kazi ya siasa naye kwa miaka karibu miwili.
T/L. Ulimwona Husein mwangia, kituo namba 4?
NDIO
T/L Kwanini unasema ulimwona namba 4? ‘nini kilikuwa special’?
Wp: Kulikuwa na wakala wangu, ambaye ni mwalimu wa dini
T/L. Kura katika kata ya ikungi, zilipgiwa wapi?
WP: Kura zilipigwa majengo ya shule ya sekondari.
T/L:Naomba umweleze muheshimiwa jaji kama inavyonekana kweny kielelezo jina hayo kuanzia 14-18 vinasomekaje?
WP: Vinasomeka vyote ka pamoja vinasomeka shule ya msingi Ikungi
T/L: Naomba nimwonyeshe exbit p3 Je vituo vya Ikungi Vinaitwaje?
WP:Vinaita ofisi ya kijiji Ikungi 1-5
T/L: Naomba umweleze mheshimiwa jaji kama mkanganyiko huo uliathiri upigaji kura
WP: Hakuna aliyeathirika
T/P; Naomba umweleze mheshimiwa kama kuna akala aliyekanganyikiwa kwa
WP: hakuna
T/P: Je chama chako kiliweka mawakala kwenye vituo vya kupigia kura
WP:Tuliweka mawakala kwenye vituo vyote
T/L je mlitumia utaratibu gani kuwapata mawakala
WP: tulitumia viongozi a chama katika ngazi za kata na vijiji
T/L:Je hiyo barua na majina aliandaa nani
WP: Niliandaa mimi
T/P:Kwa juu kabisa kwenye barua kuna maandishi ya mkono mwambie jaji ni nani aliyeandika hayo maandishi
WP: Niliandika mwenyewe
T/L; Ilikuwaje ukaandika kwa mkono
WP:Nilisahau wakati wa kuchapa kwa nembo ya chama cha CUF
T/L:Je barua ulizonazo kwenye kielelezo kwa ufahamu wako zinafanana
WP: Zinafanana
T/L:Ilikuwaje hizo barua zikafananafanana
WP:Nilimpigia simu katibu wa chadema nikamwomba ushauri wa namna ya kuandika barua kwa vile nilijua mgombea wao ni mwanasheria
T/L:Shahidi mimi nimeshitakiwa kwenye mahakama hii kwa madai kwamba hizo barua na majina ya mawakala niliandika mimi je hiyo ni kweli?
WP: Si kweli ,kila chama kiliandaa jinsi wanavyojua
T/L:Je hiyo barua ya CUF iliandikwa na Tundu Lisu
WP: Hapana niliandika mwenyewe
T/L: Je wakati wa kuandika barua hiyo mimi nilikuepo?
WP: Haukuwepo na wala sikukuona
T/L:Naomba umweleze jaji jinsi mafunzo ya mawakala wa CUF walivyofundishwa.
WP: Mawkala wa CUF walifundishwa na makatibu wa chama wa kata
T/L:Je unaielezaje mahakama hii kuwa mie nilifundisha mawakala wa vyama vyote
WP: Si kweli kwamba mawakala wote walifundishwa na tundu lisu CUF wallifundisha wao wenyewe
CHAKULA NA MALIPO
T/L:CUF waliwalipaje mawakala wao
WP:Kila wakala alitakiwa kuonyesha fomu ya matokeo ndipo alipwe.
T/L:Chakula kwa mawakala kiligawiwaje?
WP: Kila wakala alitakiwa kutumia sio chini ya shs 2000 au wabebe chakula kutoka majumbani kwao
T/L:Naomba umweleze mheshimiwa jaji kama kuna wakala yeyote wa chama chako aliyehongwa na Tundu
WP:Hakuna
T/L: Mweleze jaji, kwa vile mlikuwa na mgombea ubunge, na wagombea udiwani 6, je mlishinda nafasi yeyote?
WP: hatukushinda nafasi yeyote.
T/L. Mweleze jaji, hizo kata 6, walishinda wagombea wa Chama gani?
WP: CCM walishinda katas 5, CHADEMA 1.
T/L. Kwenye Ubunge nani alishinda?
WP: Alishinda Tundu Lissu wa CHADEMA.
T/L. Jaji ameombwa atengue matokeo kwa kuwa uchaguzi haukuwa huru wala wa haki, wewe na Chama chako ambao hamkushinda nafasi hata moja unasemaje?
WP: Uchaguzi ulikuwa huru na wa haki, Sisi CUF tuliridhika na tukasaini matokeo.
CROSS EXAMINATION:
Wakili wa walalamikaji:Godfery Wasonga.
WAKILI: Naomba kujua elimu yako.
Wp: Mimi nina elimu ya darasa la saba.
WAKILI: Umesema mlikuwa na ushirikiano na vyama vingine vya Upinzani? Je wakati wa kuandika barua mlikuwa bado mnashirikiana?
WP: Tulikuwa tunashirikiana baadhi ya vitu si vyote.
WAKILI:Tusaidie barua hiyo ya CUF uliandika tarehe ngapi?
WP; 24/10/2010.
WAKILI: Kuna shahidi umemtaja hapa Husein Mwangia, alikuwa kituo gani/
WP: Shule ya Msingi, Ikungi namba 4.
Wakili: Ikungi kulikuwa na vituo vingapi?
WP: Kulikuwa na vituo vitano
WAKILI: je kwenye vituo vya Ikungi kulikuwa na kituo cha Ofisi ya VEO?
WP: hapana.
WAKILI: Shahidi namba 8, anasema alipewa juice, maji na biskuti, wewe unabisha?
WP: SIJUI.
WAKILI: Unajua kuwa Lissu alifundisha mawakala wa CUF?
WP: Sina kumbukumbu yeyote kama Lissu aliwahi kufundisha mawakala wa CUF.
WAKILI: kwenye vituo mawakala wenu mliwaambia wasitumie gharama ya 2000, je maandishi hayo yapo kwa jaji?
WP: CUF hawakuwa na kesi mahakamani kuna haja gani kuleta nyaraka za chama.
WAKILI: Umesema uchaguzi wote ulikuwa huru na wa haki, ulihudhuria vituo vyote?
WP: sikutembelea, ila mawakala walileta taarifa.

 
Good & detailed reporting. keep it up!:):):)

Tangu jana mchana hatukutuma maelezo mengi katika JF kulikuwa na tatizo la mtandao. Naomba kutumia fursa hii kuwatumia maelezo ya tangu jana mchana, hadi sasa ambapo shahidi wa mwisho wa Tundu Lissu anafunga kwa kufanyiwa cross examination na wakili wa walalamikaji. SHAHIDI WA TATU: SHABANI HAMISI LYIMU. PINGAMIZI TOKA KWA WALALAMIKAJI: Shahidi huwa anahudhuria mahakamani kila siku, lakini pia sitegemei kama Tundu Lissu anaruhusiwa kumwongoza shahidi wake kama wakili. LISSU ANAJIBU: kwa ufahamu wangu wa sheria sijawahi kuona kuwa shahidi wa utetezi haruhusiwi kuingia mahakamani wakati walalamikaji wanatoa ushahidi. Wanaokatazwa ni wale ambao katika kuwepo kwao hasa kwa upande wa walalamikaji. Cha pili; kuhusu kama ninaweza kumwongoza shahidi wangu au la, hiyo ni haki ya pande z
 
Huu mtiririko mzuri sana,ukiufuatilia vizuri,utapata insight nyingi sana za kisheria,kazi nzuri mkuu Isango
 
tangu jana mchana hatukutuma maelezo mengi katika jf kulikuwa na tatizo la mtandao. Naomba kutumia fursa hii kuwatumia maelezo ya tangu jana mchana, hadi sasa ambapo shahidi wa mwisho wa tundu lissu anafunga kwa kufanyiwa cross examination na wakili wa walalamikaji.

shahidi wa tatu: Shabani hamisi lyimu.
pingamizi toka kwa walalamikaji: Shahidi huwa anahudhuria mahakamani kila siku, lakini pia sitegemei kama tundu lissu anaruhusiwa kumwongoza shahidi wake kama wakili.
lissu anajibu: Kwa ufahamu wangu wa sheria sijawahi kuona kuwa shahidi wa utetezi haruhusiwi kuingia mahakamani wakati walalamikaji wanatoa ushahidi. Wanaokatazwa ni wale ambao katika kuwepo kwao hasa kwa upande wa walalamikaji.
cha pili; kuhusu kama ninaweza kumwongoza shahidi wangu au la, hiyo ni haki ya pande zinazobishania jambo, sio haki ya mawakili tu. Wakili wasonga hajajielekeza vizuri katika sheria, hivyo hajaielekeza vizuri mahakama yako kisheria. Kifungu 146(1) cha sheria ya ushahidi, ni upande uliomleta ndio unaweza kumhoji sio wakili wao. Hiyo ni haki ya msingi. Naomba pingamizi hizo mbili uzikatae na tuendelee.
jaji: Bwana lyimu simama, je ni kweli ulihudhuria ndiyo, mara ya mwisho lini?
wp: Juzi, jana sikuwepo.
wakili wa walalamikaji: Ulipotoa kauli kuwa mashahidi wasiwepo hukusema kuwa ni wa walalamikaji tu.
jaji: Defence wasingeweza kujua nini kitasemwa na nyie ili kuestablish case yao, pingamizi nalikataa, mashahidi wa utetezi wasingejua ninyi mnasema nini. Ningekuwa na mawazo tofauti kama walikuwepo jana. Hata hoja ya pili ni haki ya kila mtu kumhoji shahidi hata kama yeye sio wakili. Pingamizi nimelitupitia mbali
t/l: Unaishi wapi na unafanya kazi gani?
wp: Nakaa kijiji cha ntunduu, kata ya kinyeto, wilaya ya singida vijijini, na ni mkulima.
t/l: Mwambie jaji kama una nafasi yeyote ya kisiasa.
wp:nafasi niliyo nayo ni katibu wa chadema wilaya ya singida vijijini.
t/l. Tangu lini?
wp: August 2009.
t/l. Umewahi kushika nyadhifa zipi katika chama hicho?
wp: Mwaka 1995, niliwahi kuwa katibu mwenezi wa chadema, (singida vijijini), mwaka 2002, nilikuwa katibu wa mkoa wa chadema – singida., nikiwa pia mjumbe wa baraza kuu la chadema taifa
t/l ukatibu huu uliushika kwa miaka mingapi?
wp: Miaka 10
t/l: Shahidi tuna kesi ya uchaguzi, waweza kumweleza jaji uzoefu wako kuhusu mambo ya uchaguzi?
wp: Nilianza mwaka 1995, uchaguzi wa vyama vingi na wakati nikiwa kama katibu mwenezi., mwaka 2000 nilikuwa katibu nako nilishiriki, na 2005 vile vile nilishiriki, na uchaguzi mkuu wa mwaka 2010 nilikuwa katibu wa wilaya
t/l: Umewahi kushiriki kama mgombea au mpiga kura.
wp: Nilishiriki kama mpiga kura, lakini pia nimeshiriki kama mgombea wa udiwani. Mwaka 1995, 2000, 2005, na 2010
t/l. Kwa kumbukumbu zako uchaguzi wa mwaka 2010 ulifanyika lini?
wp: Tarehe 31/10/2010
t/l. Mwambie jaji, kwa nafasi yako kama katibu wa wilaya wa chadema ulikuwa na nafasi gani katika uchaguzi huo?
wp: Niliandaa wagombea wa udiwani kupitia chama changu, wabunge wanaotokana na chama changu katika majimbo matatu yaliyopo katika wilaya yangu.
t/l: Kazi zingine?
wp:kuratibu maelekezo mengine kutoka kwa msimamizi wa uchaguzi, na maelekezo mengine toka ngazi ya juu yanayohusiana na chama.
t/l. Fafanua, unapotaja maelekezo yamsimamizi wa uchaguzi una maana gani?
wp: Ni hatua zote za awali za uchaguzi, na maelekezo yote yanayohitajika, kuanzia kupata orodha ya wapiga kura waliojiandikisha katika jimbo letu,
t/l. Mweleze jaji, utaratibu wa mawasiliano kati ya ofis yako na msimamizi wa uchaguzi yalifanyikaje?
wp: Msimamizi wa uchaguzi aliteua ofisa mmoja wa kusambaza barua, na kwa kuwa sisi hatukuwa na ofisi basi walikuwa wanapeleka wao kwa gari yao mpaka nyumbani kwa mwenyekiti.
t/l. Je nyie mkitaka kuandika barua kwa msimamizi mlikuwa mnafuata utaratibu gani?
wp: Tulipeleka wenyewe kwa njia ya dispatch
t/l: Naomba uangalie nyaraka hizi. Tuambie, hiyo unayoangalia ni barua ya nani?
wp. Barua hii inayohusu orodha ya mawakala ni yangu na nilipeleka kwa msimamizi wa uchaguzi.
t/l: Nini kilikufanya uandike barua hizi?
wp: Mheshimiwa jaji, nilitakiwa kufanya vile na msimamisi wa uchaguzi siku saba, kabla ya uchaguzi.
t/l. Hebu mweleze jaji kiwango chako cha elimu.
wp: Darasa la saba.
t/l. Umewahi kuhudhuria kozi yeyote ya mambo ya sheria?
wp: Hapana
t/l. Hiyo barua ya chadema uliyosoma, imetaja vifungu vya sheria, mweleze jaji, hayo uliyatoa wapi?
wp: Nilipata toka kwa mheshimiwa tundu lissu, aliyekuwa mgombea wa singida mashariki, aliniomba kuwa katika mawasiliano ya uchaguzi kwa kuwa mambo mengi ni ya kisheria, hivyo kila nilipopata barua niliwasiliana na lissu kabla ya kuandika.
t/l. Kwenye orodha umetaja kuwa kuna wakala wa kituo na wakala mbadala, hayo uliyapata wapi?
wp: Tuliyapata toka kwa msimamizi wa uchaguzi, kwani mawakala wote walipaswa kuapa.
t/l: Kwa vile umesema umeshiriki katika chaguzi nyingi je inaruhusiwa kuwa na wakala mbadala?
wp: Kwa ufahamu wangu, kuwa na wakala mbadala ni sahihi.
t/l, hiyo barua imechapwa, wewe unayeda singida mjini.
wp: Nilichapa katika stationary, na barua zangu zote huwa nachapa hapo
t/l. Mlikuwa na mawakala wangapi katika jimbo la singida mashariki?
wp. Tulikuwa na mawakala 124 wa vituo, na 124 mawakala mbadala.
t/l. Mweleze jaji, je unamfahamu aliyeandika barua hiyo ya cuf?
wp> ni seleman ntandu – katibu wa cuf singida vijijini.
t/l. Unafahamu huyu uliyemtaja?
wp: Ndio, tumewahi kuwa na ushirikiano wa kisiasa na vyama vyote kasoro ccm, kiwilaya na kimkoa, hivyo ninamfahamu
t/l. Umefanya kazi naye kwa muda gani?, na ni kazi gani maana jaji hakuwa pamoja na nyie?
wp:kuhamasisha mikutano ya hadhara vijijini
t/ l. Ilikuwaje barua zenu zikafanana?
wp: Alipoona barua yetu, naye aliomba ili akaandike nayekwa mkurugenzi, na nilimwelekeza pale nilipochapisha kaenda kuchapa ile. Na wengine waliomba ushauri wakaenda kuandika.
t/l. Nimeshtakiwa kuwa barua hizo zote ulizonazo niliziandika mimi, mweleze jaji unajua nini?
wp: Si kweli kwamba wewe umeaziandika
t/l. Wakati mnaziandika mimi nilikuwepo?
wp. Hapana, haukuwepo
t/l :inadaiwa kuwa kwa sababu ya barua hizo, nilikuwa na mawakala 1240, 620 ndani ya vituo na 620 nje ya vituo je ni kweli?
wp: Utaratibu tulioutumia, nilioorodhesha kwenye barua ndio uliotumika.
t/l. Mwambie jaji, je mawakal wa chama chako walikuwa wa chama chako tu? Au ulitumia utaratibu gani kuwapata?
wp: Vigezo tulivyotumia ni kuwaomba makatibu wetu wa kata watuletee majina ya wanachama, na wale wasio wanachama, ambao wanatuunga mkono na tuliothibitisha bila shaka kuwa ni waaminifu, wawe wanajua kusoma na kuandika.
t/l. Kuna ushahidi unasema kuwa mimi niliwafunza mawakala wote isipokuwa wa ccm wewe unajua utaratibu wa mafunzo ya mawakala wenu ulikuwaje?
wp: Kuchukua wanaojua kusoma na kuandika, aliye muadilifu, ili awe wakla
t/l. Unafahamu kama wote waliohudhuria mafunzo kama wote walikuwa wanachama wa chama chako
wp: Siwezi kuwafahamu.
t/l. Hivi wote waliohudhiria mafunzo hayo wote walipata nafasi ya uwakala?
wp: Hapana sio wote.
t/l. Wale ambao ninyi hamkuwachukua nini walienda chama gani?
wp; sijui.
t/l. Ninatuhumiwa kuwa niliwahonga mawakala wa vyama vingine isipokuwa ccm kwa kulipia chakula chao, na usafiri wao. Je utaratibu ulikuwaje?
wp: Kwanza sio kweli. Nilipokea pesa toka makao makuu, kwa ajili ya kusaidia chakula cha mawakala siku ya uchaguzi.
t/l; mweleze jaji ulizitumiaje?
wp: Nilizituma kwa viongozi wetu wa kata, siku tarehe 29/10/2010 walipokuwepo kwenye maeneo ya kula viapo, ikungi na mungaa, na kutoa maelekezo wanunue juice, maji na biskuti. Vyote vina gharama ya shilingi 800/= tukatumia 198,400/-
t/l. Unawafahamu waliogawiwa hivyo vitu?
wp: Kwa ufahamu wangu najua waliogawia ni mawakala wa chama change.
t/l: Kuna ushahidi umetolewa kuwa hayo maji, juice na biskuti viligawiwa pia kwa mawakala wa vyama vingine, wewe unazungumziaje?
wp: Bajeti yenyewe ni ndogo, ina upungufu mkubwa, hiyo haiwezekani. Zilibaki 1600/- tu.
t/l:niambie kama unakumbukumbu au unafahamu juu ya sherehe iliyofanyika makiungu?
wp:nafahaumu
t/l:nambiwa kuwa kwenye sherhe hiyo nilikiri kuwa niliwapa vinywaji na biskuti?
wp:tuliwapa hivo vitu mawakala wa chadema tu
t/l:sema kama tuliwapa mawakala wa vyama vingine?
wp; tuliwapa ni uwingi wa mawakala wa chadema
t/l;ni nani aliyefungua sherehe za makiungu
wp:aliyefungua ni mwenyekiti wa kijiji cha makiungu
t/l;niambie kama ulikuwa unamfahamu paskali halu na shabani selema
wp:nimewafahamia mahakamani
t/l:je, unamfahamu bwana swai ambaye ni katibu tarafa ya mungaa na ambaye alipiga picha za video?
wp: Ndiyo namfahamu
t/l:tangu lini?
wp: Namfamu tangu mwaka 2008 alipokuwa katibu tarafa sepuka
t/l: Je siku ya sherehe ulimwona?
wp:ndiyo nilimwona kwa muda mfupi na baadaye alitoweka
t/l:kulikuwa na chakula na vinywaji je, alikuwepo?
wp:la sikumwona wakwti wa chakula na vinywaji na hata wakati wa hotuba hakuwepo

maswali toka kwa wakili wa walalamikaji: Cross examination:
wakili:unakaa kijiji gani?
wp: Ntunduu, 14 km toka mjini singida.
wakili: Ulisema kuwa mlikuwa na ushirikiano wa vyama ya upinzaji je ilikuwa ni ngazi ipi?
wp: Wilaya na mkoa.
wakili: Mwambie jaji, uliandika barua kwa maelekezo ya nani?
wp: Kwa maelekezo ya tundu lissu.
wakili: Barua ulizoshuhudia zikiandikwa ni zipi na zipi?
wp: Nilishuhudia ya chadema na cuf, vyama vingine sijui.
wakili: Kawaida barua huwa zinaandikwa na nani?
wp: Na makatibu.
wakili: Fedha mlitoa kiasi gani toka makao makuu, zilitumwa na nani?
wp: Zilitumwa na dady igogo, kwa niaba ya antony komu
wakili: Je mnarisiti yeyote pale kwa jaji, kuonyesha kuwa mliwahi kupewa pesa?
wp: Hakuna
wakili: Una nyaraka yeyote sasa kuonyesha kuwa mlitumiwa pesa?
wp: Sina.
wakili: Wewe ndo ulitoa maelekezo ili juice, maji na soda vinunuliwe, je vilinunuliwa wapi?
wp: Hapana
wakili: Ni wewe ndo ulivinunua?
wp: Hapana,
re: Examination
tundu lissu; umeulizwa kama una risiti ya pesa ulizotumiwa au benk statement, mwambie jaji, pesa ulitumiwa kwa njia gani?
wp: Nilitumiwa kwa m-pesa

shahidi wa nne:
selemani mohamed ntandu;
t/l: Nitakuongoza kwenye ushahidi, uzungumze kwa makini,kwa sauti tena taratibu.
t/l: Mweleze jaji, wewe una nafasi gani kisiasa katika wilaya,
wp: Mimi ni katibu wa wilaya
t/l: Tangu lini
wp: 2008, july.
t/l. Kabla ya hapo ulikuwa una kazi gani?
wp: Nilikuwa mtunza hazina wa wilaya, na nilikuwa mjumbe wa kamati tendaji cuf,
t/l. Mweleze jaji, kama unanifahamu mimi, na umenifahamu kwa muda gani?
wp: Nilimfahamu mwaka 2000 dar, kwenye sherehe ya vijana fulani walikuwa namaliza chuo kikuu, wakati huo lissu alikuwa anatoka marekani na alikuwa mgeni mualikwa katika hiyo sherehe, pia namfahamu kwa kuwa tulifanya naye kazi ya siasa, vyama vya chadema, cuf, nccr na tlp vilishirikiana kisiasa mwaka 2008, wilaya ya singida vijijini.
t/l. Hebu tuzungumzie suala la uchaguzi 2010.
wp; mimi nilishiriki kama mgombea wa udiwani, kata ya ikungi. Lakini pia kama katibu wa wilaya nilikuwa mtendaji wa shughuli zote za chama
t/l: Mweleze jaji, kama chama chako kilikuwa na wagombea wengine
wp. Tulikuwa na wagombea 6
t/l. Mwelezi jaji, wewe ulipokuwa mgombea wa udiwani kata ya ikungi, ulitembelea vituo?
wp: Ndio
t/l. Mwambie jaji, unamfahamu husen mwangia,
wp. Nafahamu kama mwislamu mwenzangu, tunasali pamoja, na tumefanya kazi ya siasa naye kwa miaka karibu miwili.
t/l. Ulimwona husein mwangia, kituo namba 4?
ndio
t/l kwanini unasema ulimwona namba 4? ‘nini kilikuwa special’?
wp: Kulikuwa na wakala wangu, ambaye ni mwalimu wa dini
t/l. Kura katika kata ya ikungi, zilipgiwa wapi?
wp: Kura zilipigwa majengo ya shule ya sekondari.
t/l:naomba umweleze muheshimiwa jaji kama inavyonekana kweny kielelezo jina hayo kuanzia 14-18 vinasomekaje?
wp: Vinasomeka vyote ka pamoja vinasomeka shule ya msingi ikungi
t/l: Naomba nimwonyeshe exbit p3 je vituo vya ikungi vinaitwaje?
wp:vinaita ofisi ya kijiji ikungi 1-5
t/l: Naomba umweleze mheshimiwa jaji kama mkanganyiko huo uliathiri upigaji kura
wp: Hakuna aliyeathirika
t/p; naomba umweleze mheshimiwa kama kuna akala aliyekanganyikiwa kwa
wp: Hakuna
t/p: Je chama chako kiliweka mawakala kwenye vituo vya kupigia kura
wp:tuliweka mawakala kwenye vituo vyote
t/l je mlitumia utaratibu gani kuwapata mawakala
wp: Tulitumia viongozi a chama katika ngazi za kata na vijiji
t/l:je hiyo barua na majina aliandaa nani
wp: Niliandaa mimi
t/p:kwa juu kabisa kwenye barua kuna maandishi ya mkono mwambie jaji ni nani aliyeandika hayo maandishi
wp: Niliandika mwenyewe
t/l; ilikuwaje ukaandika kwa mkono
wp:nilisahau wakati wa kuchapa kwa nembo ya chama cha cuf
t/l:je barua ulizonazo kwenye kielelezo kwa ufahamu wako zinafanana
wp: Zinafanana
t/l:ilikuwaje hizo barua zikafananafanana
wp:nilimpigia simu katibu wa chadema nikamwomba ushauri wa namna ya kuandika barua kwa vile nilijua mgombea wao ni mwanasheria
t/l:shahidi mimi nimeshitakiwa kwenye mahakama hii kwa madai kwamba hizo barua na majina ya mawakala niliandika mimi je hiyo ni kweli?
wp: Si kweli ,kila chama kiliandaa jinsi wanavyojua
t/l:je hiyo barua ya cuf iliandikwa na tundu lisu
wp: Hapana niliandika mwenyewe
t/l: Je wakati wa kuandika barua hiyo mimi nilikuepo?
wp: Haukuwepo na wala sikukuona
t/l:naomba umweleze jaji jinsi mafunzo ya mawakala wa cuf walivyofundishwa.
wp: Mawkala wa cuf walifundishwa na makatibu wa chama wa kata
t/l:je unaielezaje mahakama hii kuwa mie nilifundisha mawakala wa vyama vyote
wp: Si kweli kwamba mawakala wote walifundishwa na tundu lisu cuf wallifundisha wao wenyewe
chakula na malipo
t/l:cuf waliwalipaje mawakala wao
wp:kila wakala alitakiwa kuonyesha fomu ya matokeo ndipo alipwe.
t/l:chakula kwa mawakala kiligawiwaje?
wp: Kila wakala alitakiwa kutumia sio chini ya shs 2000 au wabebe chakula kutoka majumbani kwao
t/l:naomba umweleze mheshimiwa jaji kama kuna wakala yeyote wa chama chako aliyehongwa na tundu
wp:hakuna
t/l: Mweleze jaji, kwa vile mlikuwa na mgombea ubunge, na wagombea udiwani 6, je mlishinda nafasi yeyote?
wp: Hatukushinda nafasi yeyote.
t/l. Mweleze jaji, hizo kata 6, walishinda wagombea wa chama gani?
wp: Ccm walishinda katas 5, chadema 1.
t/l. Kwenye ubunge nani alishinda?
wp: Alishinda tundu lissu wa chadema.
t/l. Jaji ameombwa atengue matokeo kwa kuwa uchaguzi haukuwa huru wala wa haki, wewe na chama chako ambao hamkushinda nafasi hata moja unasemaje?
wp: Uchaguzi ulikuwa huru na wa haki, sisi cuf tuliridhika na tukasaini matokeo.
cross examination:
wakili wa walalamikaji:godfery wasonga.
wakili: Naomba kujua elimu yako.
wp: Mimi nina elimu ya darasa la saba.
wakili: Umesema mlikuwa na ushirikiano na vyama vingine vya upinzani? Je wakati wa kuandika barua mlikuwa bado mnashirikiana?
wp: Tulikuwa tunashirikiana baadhi ya vitu si vyote.
wakili:tusaidie barua hiyo ya cuf uliandika tarehe ngapi?
wp; 24/10/2010.
wakili: Kuna shahidi umemtaja hapa husein mwangia, alikuwa kituo gani/
wp: Shule ya msingi, ikungi namba 4.
wakili: Ikungi kulikuwa na vituo vingapi?
wp: Kulikuwa na vituo vitano
wakili: Je kwenye vituo vya ikungi kulikuwa na kituo cha ofisi ya veo?
wp: Hapana.
wakili: Shahidi namba 8, anasema alipewa juice, maji na biskuti, wewe unabisha?
wp: Sijui.
wakili: Unajua kuwa lissu alifundisha mawakala wa cuf?
wp: Sina kumbukumbu yeyote kama lissu aliwahi kufundisha mawakala wa cuf.
wakili: Kwenye vituo mawakala wenu mliwaambia wasitumie gharama ya 2000, je maandishi hayo yapo kwa jaji?
wp: Cuf hawakuwa na kesi mahakamani kuna haja gani kuleta nyaraka za chama.
wakili: Umesema uchaguzi wote ulikuwa huru na wa haki, ulihudhuria vituo vyote?
wp: Sikutembelea, ila mawakala walileta taarifa.

kaka tundu lissu, all my God be with you ameni. Sisi tupo nyuma yako kwa maombi na kufunga tunaamini utashinda hiyo kesi ili uendelee kututetea sisi watanzania maskini.
Ee mwenyezi Mungu mwingi wa rehema uliye umba mbingu na nchi. Wewe ndiye uliye teua na unasimamia mamlaka zote za serikali na kidini. Tunakuomba umwongoze huyu mweshimiwa jaji katika njia ya haki na ukweli ili aweze kutenda haki.
Ameni
 
sina taaluma ya sheria..lakini naweza kusema leo nimeenda darasa la sheria..
Kila la heri TL.
Mkuu Isango, usichoke kutujuza yanayojiri hapo mahakamani!
 
Mungu ameamua kuwaumbua magamba kwa vinywa vyao na mashaidi wao! Mwisho wao upo karibu kuliko jangwani na magomeni!
 
Naomba kujua hayo maswali na majibu huwa unawezaje kujaandika mahakamani?

Mkuu mbona watu siku hizi wana voice recorder nyingi tu. Hata simu zina voice recorder unaweza kunasia mahojiano yote na kukaa chini na kuya-transcribe. Hilo siyo swali la kuuliza ni wastage of time. Badala ya kumpongeza mleta mada unaanza suala la kutaka kujua yaliyo nyuma ya pazia maana sasa utamuuliza mpaka aina ya computer yake etc. Big up Isango
 
Pongezi zako mkuu Isango,na hawa majizi wa haki CcM lazima wataumbuka tuu.
 
Hapa nimegundua kuwa huyu wakili wa serikali anataka kumshikisha T/L na kesi ya rushwa ambayo itamfanya atenguliwe ubunge na kufungiwa, ndiyo maana wakili amekuwa akirudiarudia rushwa ya juice na maji kila anapo muuliza shahidi.
Kwa mtazamo wangu inaonekana kuna mpango umesukwa mahususi wa kumuengua T/L lakini unakwama kwasababu jamaa anaona mbali kisheria
Ngoja tusubiri!
 
Back
Top Bottom